Tafuta

Vatican News
Papa Francisko amekutana mjini Vatican na Taasisi ya Kipapa ya Ethiopia katika fursa ya Maadhimisho ya miaka 100 tangu uwepo wa taasisi hiyo katika kuta za mjini Vatican Papa Francisko amekutana mjini Vatican na Taasisi ya Kipapa ya Ethiopia katika fursa ya Maadhimisho ya miaka 100 tangu uwepo wa taasisi hiyo katika kuta za mjini Vatican   (Vatican Media)

Papa Francisko:uhuru wa Kanisa katika kuhudumia nchi za Ethiopia na Eritrea!

Papa Francisko alipokutana na Taasisi ya Kipapa ya Ethiopia tarehe 11 Januari 2020 amejikita katika mada kuu tatu msingi kwenye hotuba yake.Amegusia vita na umwagaji damu na jitihada za kichungaji zinazotakiwa kutendewa wale ambao wanaacha nchi zao.Kanisa Katoliki nchini Ethiopia na Eritrea lipate kuwa huru katika kutoa huduma kwa ajili ya ustawi wa wote nchini mwao.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Papa Francisko tarehe 11 Januria 2020 amekutanta na Jumuiya ya Kiethiopia wakiwa katika maadhimisho ya Jubilei ya miaka 100 tangu uwepo wa Taasisi ya Kipapa ndani ya Mji wa Vatican. Ametoa salam  kwa Maaskofu kutoka Ethiopia na Eritrea na miongoni mwao wakiwepo maaskofu wakuu wawili Kardinali, Berhaneyesus, Askofu Mkuu Menghesteab Tesfamariam, M.C.C.I. wa Jimbo Kuu katoliki la Asmara nchini Eritrea, jumuiya ya wanafunzi na viongozi wakuu wa mashirika kwa namna ya pekee Gombera na Makamu wake, watawa ambao wanatoa huduma katika katika taasisi hiyo ya kipapa  na wafanyakazi walei. Salam pia kwa Kardinali Leornardo Sandri, Rais wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki na Askofu Basil na kuwashukuru Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki linaloshughulikia Taasisi hiyo. Papa amewashukuru wafadhili na kuwa na utambuzi  wa namna ya pekee kwa ukarimu wao. Jumuiya ya watawa wakapuchini, wakiwepo Mkuu wa shirika hilo na wawakilishi wa Taasisi ya Kipapa ya nchi za Mashariki na idadi kubwa ya mapdre na mafrateli wa Ethiopia na Eritrea.

Miaka 100 ya historia ya uwepo wa waethiopia mjini Vatican

Papa ameanza kueleza historia ya uwepo wa Waethiopia katika kuta za Vatican na wakiwa ni jumuiya ya   kwanza kikaribishwa na kuendelea na ukarimu huo kwa miaka 100  sasa wakipeleka mbele neno ukarimu. Katika Kaburi la Mtume Petro kwa karne nyingi wamepata nyumba na ukarimu  kama watoto kutoka mbali ya Roma na kama kuwa na ukaribu wa imani ya mitume katika kukiri Yesu Kristo.  Na Maneno mazuri ya kueleza hivyo, Papa ametaja kuwa  yanatoka kwa kwa Mmonaki mkubwa Tesfa Sion, Petro  wa Ethiopia ambaye amezikwa katika Kanisa la Mtakatifu Stefano wa Ethiopia, mahali ambapo wao kwa siku mbili nwaadhimisha Liturujia zao. Yeye alisema: “mimi ni mwethiopia, mhujaji kutoka mahali na kwenda mahali(…). Lakini hakuna eneo zaidi ya Roma nimewahi kupata utulivu wa roho na mwili; utulivu wa roho kwa sababu hapa kuna imani ya kweli; na  utulivu wa mwili kwa sababu hapa nimepata Mfuasi wa Petro ambaye anatusaidia katika mahitaji yetu”. Mmonaki huyo aliweza kutajirishwa na hekima yake ndani ya makao makuu ya Roma na katika  kujikita k kutafsiri na kutangaza Biblia ya Agano jipya katika lugha ya kiethiopia, Papa Francisko amefafanua.

Wanafunzi mapadre wadumishe utajiri wa historia ya nchi yao watakaporudi kwao

Papa Francisko akiendela na hutuba yake amewaangazia wanafunzi, mapadre kutoka Ethiopia na Eritrea, ambayo anasema ni Makanisa mawili yaliyoungana kwa utumaduni unaofanana, na kwa hiyo anawaomba leo hii wapeleke katikati yao ule utajiri wa historia ya nchi zao hasa  wa kuendeleza utamaduni wa kizamani na kuuishi kwa pamoja kati ya wanaume na wanake unaotokana  na dini ya kiyahudi na ile ya kiislam, zaidi ya upamoja wa ndugu wengine wengi  wa Kanisa la Kiorthodox Tewahedo. Aidha Papa amekumbuka jinsi alivyoweza kukutana mjini Roma na Patriaki Mathiasi wa Ethiopia ambaye amemtumia salam kindugu.

Fursa ya kuwakumbuka ndugu wengi wa Ethiopia na Eritrea wanaoteseka na umaskini na vita iliyopita

Papa Francisko amesema, kwa kukutana nao, umempa hta  ya kukumbuka ndugu wengi, kaka na dada wa Ethiopia na Eritrea ambao wanaishi katika umaskini na zaidi miezi michache iliyopita walikuwa wanaishi vita na misuko suko, ambayo kwa kuhitimisha kwake  ni shukrani kwa Bwana na wale ambao katika nchi wamekuwa mstari wa mbele katika harakati za mktadha wa amani na mapatano. Anawaombea sehemu zote mbili kutokana na uchungu waliouishi na kwamba usiweze kurudiwa tena mgawanyiko kati ya kabila na kati ya nchi katika mizizi yao inayowaunganisha. Kwa njia hiyo wanaweza kweli kuelimisha na kukuza zawadi ya Mungu kwa waamini ambao watakabidhiwa na kuhudumia majeraha ya ndani na nje ambayo wataweza kukutana na kutafuta kusaidia michakato ya mapatano  na kwa ajili ya watoto endelevu na kizazi cha vijana katika nchi zao.

Kanisa la Ethiopia na Eritrea lihakikishiwe uhuru wa kuhudumia kwa ajili ya ustawi wa wote.

Papa Francisko amewatia moyo wa kuhifadhi tunu msingi za utamaduni wa Kanisa, na  daima wakiungana na upeo wa kimisionari. Ni matashi mema kwamba Kanisa katika mataifa yao  mawili yanaweza kuhakikishiwa ule uhuru wa kuhudumia kwa ajili ya ustawi wa wote,  ikiwa ni kuruhusu pia wanafunzi waweze kwenda na  kumalizia masomo yao Roma au sehemu nyingineyo, wakati wakilinda Taasisi za elimu, afya na hduma zote za utunzaji, kwa uhakika kwamba, Wachungaji na waamini wanatamani pamoja na wengine kuchangia wema na matarajio ya mataifa yao. Kama watoto wa Makanisa ya Ethiopia na Eritrea, wazidi kumpenda Mtakatifu Bikira Maria  Mama wa Mungu, ambaye kama utamaduni wao wa kumwita  Mama Maria ( Resta Maryam feudo” na katika kila mwezi wanayo liturujia iitwayo (Kidna Mehrat) maana yake (mapatano ya huruma) watambue kumkabidhi kila maombezi na kila sala. Na kwa maana hiyo katika sala hizo wasisahau kumwombea hata Papa.

11 January 2020, 14:45