Tafuta

Vatican News
Tuache tushangazwe na uchaguzi wa Mungu wa kukaa upande wetu,hasa wa kuwa na mshikamano na sisi wadhambi na kuokoa ulimwengu dhidi ya mabaya, na ambaye alibeba mwenyewe dhambi zetu Tuache tushangazwe na uchaguzi wa Mungu wa kukaa upande wetu,hasa wa kuwa na mshikamano na sisi wadhambi na kuokoa ulimwengu dhidi ya mabaya, na ambaye alibeba mwenyewe dhambi zetu  (Vatican Media)

Papa Francisko:uchaguzi wa Mungu ni wa kiajabu sana!

Uchaguzi wa Mungu kuwa upande wetu ni wa kiajabu sana, na kama Yohane Mbatizaji,tuache tushangazwa na mapya ambayo hayajawahi kusikika ya Mungu katika Yesu anayejifanya kuwa na mshikamano nasi na kuokoa ulimwengu huku akibeba dhambi zetu.Amethibitisha hayo Papa katika Tafakari ya sala ya Malaika wa Bwana tarehe 19Januari 2020.Na mwisho amewatakia ufanisi mwema wa Mkutano wa Berlin kuhusu Libya.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika Tafakari ya Papa Francisko tarehe 19 Januari 2020 kwa waamini na mahujaji wote waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Vatican, Papa ameanza kusema: Katika Dominika ya Pili ya kipindi cha mwaka,  bado mada inapendekeza mwendelezo wa Maonyesho na Ubatizo wa Yesu. Injili ya Siku kutoka (Yh 1,29-34 ) bado inazungumzia juu ya maonyesho ya Yesu. Kwani baada ya kubatizwa katika Mto wa Yordani, Yeye aliwekwa wakfu na  Roho Mtakatifu aliyeshuka Juu yake na kusikika sauti ya Baba Mwenyezi ikitangaza kuwa ni Mwanaye mpendwa ( Mt 3,16-17).

Mwinjili yohane anatofautiana na wengine watatu

Mwinjili Yohane tofauti na wengine watatu, haelezei matukio, bali anapendekeza ushuhuda wa Yohane Mbatizaji. Yeye alikuwa shuhuda wa kwanza wa Kristo. Mungu alikuwa amwemwita na kumwandaa kwa ajili ya hilo.Mbatizaji hasingeweza hata hivyo kujizuia kuelezea ile shauku yake  ya kutoa ushuhuda kwa Yesu na kuthibitisha kuwa:“mimi niliona na nilishuhudia (Yh 1, 34). Yohane aliona jambo la kushngaza, yaani Mwana Mpendwa wa Mungu mwenye kuwa na mshikamano na wadhambi; na Roho Mtakatifu alimfanya atambue hayo mapya ambayo hayajawahi kusikika, na mapinduzi ya kweli, Papa Francisko amefafanua.

Katika dini zote hakuna aliyejisadaka isipokuwa ni Mungu

Kwa hakika katika dini zote, mtu ambaye anajitoa na kujisadaka jambo kwa Mungu katika muktadha wa  Yesu ni Mungu ambaye anatoa Mwanae wa Pekee kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu. Yohane anaonesha shauku na mshangao, kwa maana ya mapya hayo yaliyoletwa na Yesu! Kwa njia ya kielelezo ambacho kinaadhimishwa kila Misa katika kutamka: “Tazama, huyu ndiye Mwana kondoo wa Mungu aondoaye dhambi za ulimwengu” ( Yh 1,29). Ushuhuda wa Yohane Mbatizaji, unatualika kuanza daima kwa upya ile safari yetu ya imani kuanzia kwa Yesu Kristo Mwanakondoo na mwenye wingi wa  huruma na ambaye Baba alitukabidhi. Tuache tushangazwe na uchaguzi wa Mungu wa kukaa upande wetu,hasa wa kuwa na mshikamano na sisi wadhambi na kuokoa ulimwengu dhidi ya mabaya, na ambaye alibeba mwenyewe dhambi zetu mwenyewe.

Tujifunze kutoka kwa Yohane Mbatizaji ambaye hakujifanya kujua kila kitu 

Tujifunze kutoka kwa Yohane Mbatizaji ambaye hakujifanya tayari kumjua Yesu na kujifanya  kujua kila kitu ( Yh 1,31). Siyo hivyo. Papa anasisitiza na  kwamba ni vema kusimama na kujikita kutafakari Injili na labda kwa kutafakari mbele ya Picha  ya Yesu au Uso Mtakatifu. Tutafakari kwa macho ya  kina na  zaidi  kwa moyo: tuache tujengwe na kufundishwa na Roho Mtakatifu ambaye ndani mwetu anasema: Ni Yeye! Ni Mwana wa Mungu aliyefanywa kondoo wa kuchinjwa kwa ajili ya upendo.

Ni Yesu aliyebeba, aliyeteseka na kuondoa dhambi za ulimwengu

Ni yeye tu aliyebeba, ni Yeye tu aliyeteseka, aliondoa adhambi za ulimwengu na  hata dhambi za wote. Yeye alichukua na aliziondoa dambi zetu na ili hatimaye tuwe huru na siyo  kuwa watumwa wa  mabaya. Aidha amesema: “Ndiyo sisi bado ni maskini wa dhambi, lakini siyo watumwa, bali watoto wa Mungu”. Na kwa kuhitimisha amesema: “Bikira Maria atujalie nguvu ya kuwa mshuhuda wa Mwanae Yesu katika kutangaza kwa furaha ya  maisha yanayotoa uhuru dhidi ya dhambi na ujazo wa Neno la imani ya kushangaza na kwa shukrani.

        

19 January 2020, 13:00