Tafuta

Vatican News
Picha ya pamoja na watawa wa shirika la kifransiskani ( Alcanterine) wakiwa katika fursa ya kuadhimisha mkutano Mkuu wao Papa anawomba watue huduma ya dhati kwa Kanisa Picha ya pamoja na watawa wa shirika la kifransiskani ( Alcanterine) wakiwa katika fursa ya kuadhimisha mkutano Mkuu wao Papa anawomba watue huduma ya dhati kwa Kanisa  (Vatican Media)

Papa Francisko:kwa mfano wa Yesu kuweni karibu na ndugu wote na kujenga dunia ya haki!

Papa Francisko baada ya katekesi yake hakusahau kama kawaidia yake kuwakumbuka vijana,wazee,wagojwa na wanandoa wapya. Anawaomba wafungue mioyo yao katika mahitaji ya Kanisa kwa kufuata mfano wa Yesu wawe karibu na ndugu na wakati huo hu kujenga dunia yenye haki zaidi.

Mara baada ya katesi yake Papa tarehe 15 Januari 2020 iliyokuwa inahusu safari ya mwisho ya Paulo ambayo ilikuwa ni Roma, kwa mujibu wa Kitabu cha Matendo ya mitume amesalimia mahujaji wote kutoka Italia na ulimwengu mzima. Kwa namna ya pekee watawa wa Kifransiskani wa Alcanterine ambao wanafanya Mkutano wao mkuu na kuwatia moyo ili waweze kuweka karama yao katika huduma yao ya  kwanza kwa Kanisa.

Aidha mahujaji wengi wa makundi mengi ya kutoka pande zote za Dunia ambapo hakusahau kama kawaida yake vijana, wazee, wagojwa na wanandoa wapya . Anawaomba wafungue mioyo yao katika mahitaji ya Kanisa kwa kufuata mfano wa Yesu ili wawe karibu na ndugu na wakati huo huo ili kujenga dunia yenye kuwa na haki zaidi.

15 January 2020, 12:47