Tafuta

Jumapili tarehe 12 Januari 2020 Papa Francisko wakati wa tafakari kabla ya sala ya Malaika wa Bwana amekazia juu ya Ubatizo katika maji kwa nguvu ya Roho Mtakatifu unaotufanya kuwa wana wa Mungu Jumapili tarehe 12 Januari 2020 Papa Francisko wakati wa tafakari kabla ya sala ya Malaika wa Bwana amekazia juu ya Ubatizo katika maji kwa nguvu ya Roho Mtakatifu unaotufanya kuwa wana wa Mungu 

Papa Francisko:Sakramenti ya Ubatizo ni wajibu wa haki kwa Bwana

Katika tafakari ya Papa Francisko wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana,anawalika waamini kushuhudia na kuwatangazia watu wengine ule upendo usio na mipaka wa Baba na kuadhimisha Sakramenti ya Ubatizo kama tendo la wajibu wa haki kwa Bwana.Kila mbatizwa anashauriwa kukumbuka tarehe ya kubatizwa kwake na kuifanyia sherehe ya kila mwaka!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 12 Januari 2020 Mama Kanisa akiwa anaadhimisha Sikukuu ya Ubatizo wa Bwana, wakati wa tafakari kabla ya sala ya Malaika wa Bwana  Papa Francisko amegusia juu ya maadhimisho aliyofanya ya Sakramenti ya Ubatizo kwa watoto 32 na kuwaomba wasali kwa ajili ya watoto hao na familia zao. Papa Francisko amesema, “Katika sikukuu ya Ubatizo wa Bwana, ninayo furaha kwa mara  nyingine tena  kuwabatiza watoto. Leo walikuwa ni 32. Tusali kwa ajili yao na kwa ajili ya familia zao . Katika Liturujia ya siku ya mwaka huu inapendekeza tukio la ubatizo wa Yesu kwa mujibu wa simulizi ya Injili ya Matayo (3,13-17) Mwinjili anafafanua mazungumzo kati ya Yesu ambaye anaomba kubatizwa na Yohane Mbatizaji, anayetaka kukataa akisema: “je wewe unakuja kwangu? ni mimi hasa ninayehitaji kubatizwa nawe”. Uamuzi wake Yesu unamshangaza Yohane Mbatizaji, kwa maana, kiukwli Masiha hana haja ya kutakaswa; ni Yeye anayetakasa. Lakini Mungu ni Mtakatifu, njia zake siyo njia zetu na Yesu ni Njia ya Mungu, njia ambayo isiyotarajiwa na tukumbuke kuwa Mungu ni Mungu wa mishangao.

Yohane anadhibitisha umbali uliokuwapo kati yake na Yesu

Yohane alikuwa akithibitisha kwamba kati yake na Yesu palikuwapo na umbali mkubwa sana, kwani alikuwa amesema: “mimi ninawabatizeni kwa maji kuonesha mmetubu. Lakini anayekuja baada yangu ana nguvu kuliko mimi; mimi sisitahili kubeba hata viatu vyake (Mt 3,13).  Papa ameongeza kusema: “lakini Mwana wa Mungu alikuja kwa sababu hii, hasa ya kuondoa umbali huo kati ya mwanadamu na Mungu. Ikiwa Yesu mzima alikuja kutoka kwa upande wa Mungu, ni wazi kwamba alikuwa yeye mzima haya kwa ajili ya   upande wa Mwanadamu na anaunganisha kile ambacho kilikuwa kimegawanyika. Na ndiyo maana Yesu akajibu na kusema “acha tu iwe hivyo kwa sasa maana ndivyo inavyo faa tuyatekeleze yale yote Mungu anayotaka” (Mt 3,15). Masiha anaomba kubatizwa kwa sababu ya kutimiza kila haki, kutumiza ile ishara ya Baba ambaye anapitia kwa njia ya utiii wa mtoto na wa mshikamano na mwadamu aliye mdhaifu na mdhambi. Ni njia ya unyenyekevu na ukaribu mtimilifu wa Mungu kwa wana wake… Hata Nabii Isaya anatangaza haki ya Mtumishi wa Mungu anayetimiza utume wake ulimwenguni kwa mtindo kinyume na roho ya ulimwengu.  Nabii Isaya anasema: “Hatalia, wala hatapaza sauti yake, wala kuifanya isikiwe katika njia kuu. Mwanzi uliopondeka hatauvunja, wala utambi utokao moshi hatauzima; atatokeza hukumu kwa kweli. (Is 42,2-3).

Yesu anatufundisha unyenyekevu,upole,urahisi,heshima,kiasi na kujificha

“Hii ndiyo tabia anayo tufundisha Yesu ya  upole wake na nyenyekevu, tabia ya kuwa rahisi, kuwa na heshima na kiasi na katika kujificha, mambo ambayo leo hii Papa amesema yanaombwa yatendwe  hata kwa wafuasi wa Bwana. Ni kwa jinsi gani ilivyo na huzuni hata kusema, kwani kuna  wafuasi wa Bwana, wanaojiona kuwa ni wafuasi wa Bwana. Siyo mfuasi mwema ambaye anajiona. Mfuasi mwema ni mnyenyekevu na mpole ambaye anatenda mema bila kujifanya aonekane” amebainisha Papa. Katika matendo ya kimisionari na katika jumuiya za kikristo zote, zinaalikwa kwenda kukutana na wengine daima huku wakipendekeza na siyo kushurutisha, kwa kutoa ushuhuda na kushirikishana maisha ya dhati ya watu.

Kama Yesu ni mpendwa wa Baba nasi kwa kuzaliwa katika maji ni wapendwa wa Baba

Mara baada ya Yesu kubatizwa katika mto ya Yordani, mbingu zikapasuka na kushuka Roho kama hua na wakati huohuo ikasikika sauti ikitoka mbinguni  na kusema :“Wewe ndiwe Mwanangu  mpendwa wangu, nimependezwa nawe”Mt 3,17). Katika Sherehe  ya Ubatizo wa Bwana,Papa anasisitiza kuwa, tugundue kwa upya ubatizo wetu. Kama Yesu ni Mwana Mpendwa wa Baba, hata sisi kwa kuzaliwa kwa Maji na Roho Mtakatifu, tutambua kuwa ni wana wapendwa, nasi ni sehemu ya kupendezwa na Mungu kwa  ndugu wengi na ambao wanajikita katika utume mkubwa wa kushuhudia na kutangaza kwa watu wote upendo wa Baba usio na mipaka.

Roho Mtakatifu anabaki ndani mwetu na hivyo ni vema kujua tarehe ya ubatizo wetu

Na sherehe za Ubatizo wa Bwana zinatufanya tukumbuke ubatizo wetu. Hata sisi tumezaliwa katika Ubatizo. Katika Ubatizo amekuja Roho Mtakatotu na anabaki ndani mwetu. Kwa maana hiyo ni vyema kabisa kujua tarehe ya Ubatizo wetu. Sisi mara nyingi tunajua tarehe ya kuzaliwa kwetu, lakini hatujuhi tarehe ya kubatizwa. Papa amebainisha pia kwamba wengi wao hawajuhi na hivyo ni zoezi la kufanya na  hasa watakaporudi kwao waulize walibatizwa lini? Na waweze sherehe katika moyo wa tarehe ya ubatizo kila mwaka. Akisisitiza amesema Papa Francisko, hata huo ni wajibu wa haki kuelekeza kwa Bwana ambaye amekuwa mwema sana kwetu sisi.  Bikira Maria Mtakatifu atusaidie kutambua daima na zaidi ya Ubatizo na kuuishi kwa dhati katika hali zozote zile za kila siku. 

PAPA - MALAIKA
12 January 2020, 13:30