Tafuta

Vatican News
Tunaadhimisha Sikukuu ya Tokeo la Bwana,kwa kukumbuka Mamajusi waliotoka Mashariki kwenda Betlehemu,wakiongozwa na nyota ili kumwona mtoto mchanga Masiha. Tunaadhimisha Sikukuu ya Tokeo la Bwana,kwa kukumbuka Mamajusi waliotoka Mashariki kwenda Betlehemu,wakiongozwa na nyota ili kumwona mtoto mchanga Masiha.   (ANSA)

Papa Francisko:Mungu anatupatia uhuru wakati miungu ya ulaghai inatufunga!

Kila uzoefu wa kukutana na Yesu kama ilivyo watokea Mamajusi unatuongoza katika njia tofauti kwa sababu kutoka kwake hutokea nguvu nzuri inayoponya moyo na kukutopndolea ubaya.Kati ya Mungu na wale ambao wameahidi kutoa miungu yao kama vile wachawi,wa bahati nasibu,waganga wa kienyeji kuna utofauti mkubwa.Tofauti ni kwamba miungu inatufunga kwaona kutufanya kuwa miungu tegemezi ambayo huwezi kuwamiliki wao.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 6 Januari 2020 wakati Mama Kanisa anaadhimisha sikukuu ya Tokeo la Bwana, Papa Francisko kabla ya sala ya Malaika wa Bwana kwa mahujaji na waamini wote waliokusanyika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro ametoa tafakari. Tunaadhimisha Sikukuu ya Tokeo la Bwana, kwa kukumbuka Mamajusi waliotoka Mashariki kwenda Betlehemu, wakiongozwa na nyota  ili kumwona mtoto mchanga Masiah. Mwisho wa simulizi ya kiinjili inasema kuwa: “ kwa kuonya katika ndoto wasirudi kwa Erode walishika njia nyingine na kurudi kwao” .

Wenye hekima walimpata yule waliye kuwa wanatamani

Wenye hekima hawa walikuwa wanatoka kanda za mbali sana na  mara baada ya kisafiri sana walimpata yule waliyekuwa wanatamani kumjua, baada ya kumtafuta kwa muda mrefu na bilashake hata kwa ugumu na kupotea. Na hatimaye walipofika katika upeo wao, walimsujudia Mtoto, walimwabudu na kumpatia zawadi zao zenye thamani. Baadaye walianza safari tena bila kukawia ili kurudi katika nchi zao. Lakini Mkutano huo na Mtoto uliwabadilisha. Mkutano na Yesu haukuwakawiza Mamajusi, bali uliwapa msukumo mpya wa kuweze kurudi kwako ili  waweze kusimulia kile ambacho walikiona na furaha waliyohisi. Katika hii kuna maonyesho ya mtindo wa Mungu na ya njia yake ya kujidhihirisha katika historia, amethibitisha Papa Francisko.

Mungu hatuzuiii anatupatia uhuru wa kurudi katika maeneo ya kawaida

Uzoefu wa Mungu hautuzuii, lakini hutuokoa; haituingizi gerezani na kutufanga, japokuwa huturudisha barabarani na kutufanya kurudi katika maeneo ya kawaida ya uwepo wetu. Maeneo yatakuwapo yenyewe, Papa amesisitiza, lakini sisi baada ya kukutana na Yesu, hatutakuwa kama wale wa kwanza. Mkutano na Yesu unatubadilisha na kutugeuza. Mwinjili Matayo anasisitiza kuwa, Mamajusi walirudi kwa kupitia njia nyingine. Hawa waliongozwa ili kugeuza mwelekeo kwa kuonywa na malaika, ili wasipitie kwa Herode na viwanja vyake vya madaraka. Kila uzoefu wa kukutana na Yesu unatuongoza katika njia tofauti kwa sababu kutoka kwake hutokea nguvu nzuri inayoponya moyo na kutondoa na ubaya, meeleza Papa Francisko.

Nguvu ya busara kati ya mwendelezo na mambo mapya

Ipo nguvu ya busara kati ya mwendelezo na mapya. Ni kurudi “katika nchi yao”, lakini “kwa kupitia njia nyingine”. Papa Francisko anabainisha kwamba hii inaonyesha kuwa, ni sisi ambao tunapaswa kubadilika, kubadilisha njia yetu ya maisha hata katika mazingira ya kawaida, kubadilisha vigezo vya kuhukumu ya hali halisi inayotuzunguka. Na ndiyo utofauti uliopo kati ya Mungu wa kweli na miungu ya hila kama vile ya fedha, ya nguvu na mafanikio… vile vile  kati ya Mungu na wale ambao wameahidi kutoa miungu yao kama vile wachawi, watu wa bahati nasibu, waganga wa kienyeji, kuna utofauti mkubwa! Tofauti ni kwamba miungu inatufunga kwao na kutufanya tuwe miungu tegemezi ambapo hatuwezi kamwe kuwamiliki wao. Mungu wa kweli hatuzuii wala kuturuhusu kushikwa na sisi. Yeye anafungua njia za mambo mapya na huru, kwa sababu Yeye ndiye Baba ambaye yuko pamoja nasi kila wakati ili kutufanya tukue.

Ukiwa unakutana na Yesu lazima hurudi sehemu ile ya kawaida

Ikiwa utakutana na Yesu, ikiwa una mkutano wa kiroho na Yesu kumbuka kamba ni lazima hurudi kwenye sehemu zile zile za kawaida daima, lakini kwa njia nyingine na mtindo mwingine. Ni hivyo, ni Roho Mtakatifu,ambayo Yesu hutupatia na ambaye hubadilisha mioyo yetu. Kwa kuhitimisha Papa Francisko anasema, “tumwombe Bikira Mtakatifu ili tuweze kuwa mashuhuda wa Kristo mahali tulipo kwa mambo mapya ya maisha, kwa kugeuzwa na upendo wake!.

06 January 2020, 14:36