Tafuta

Vatican News
Papa amekutana na wanadiplomasia kama fursa ya kutakiana heri za mwaka mpya ambapo ametoa wito kwa mataifa yenye migogoro kufanya majadiliano ambayo yanaweza kuleta amani Papa amekutana na wanadiplomasia kama fursa ya kutakiana heri za mwaka mpya ambapo ametoa wito kwa mataifa yenye migogoro kufanya majadiliano ambayo yanaweza kuleta amani  (Vatican Media)

Papa Francisko:Migogoro inatatuliwa kwa njia ya majadiliano na kuheshimu sheria Kimataifa!

Hotuba ya Papa Francisko wakati wa kukutana na Mabalozi na wawakilishi wa Vatican kama fursa ya kutakiana heri na baraka za Mwaka Mpya imejikita kutazama hali halisi ya dunia akianza na matumaini na pia kuhusu mivutano kati ya Iran na Marekani,mivutano ambayo ni karibu kila bara na hali nyingine za umaskini,mazingira,ushirikiano.Ametoa wito wa majadiliano hasa katika sehemu zote zenye kinzani.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika  hotuba ya Papa Francisko kwa wanadiplomasia anatoa mtazamo wake wa matumaini hata katika kukabiliana na vipeo vinavyoikabili dunia hii. Anataja migogoro mingi sana hata ile iliyosahulika, lakini pia hata manyanyaso ya watoto, vurugu dhidi ya wanawake na maana ya mshikamano katika Ulaya. Ni nchi 183 ambazo kwa sasa zinashikamamana na kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia na Vatican, ambazo pia zinajumuisha Umoja wa Ulaya na Jimbo la Kijeshi la Kisiwa cha Malta. Kwa kuanza hotuba yake na  matumaini ndiyo anaomba papa ili  yaweze kuwaongoza katika kipindi hiki kinachowasubiri. Amesisitiza hayo kwa wanadiplomasia wote katika fursa ya kiutamaduni ya kutakiana matashi mema ya mwaka mpya , katika mkutano ulifanyika tarehe 9 Januari 2020. Tangu mwanzo wa hotuba yake  amesisitiza kwamba ikiwa matumaini yanatakiwa kuwa ya kweli na kwamba matatizo yaitwe jina hata kama mwaka mpya umeanza na  ishara ambazo hazitii moyo kutokana na na  ufunguzi mivutano na vurugu. Lakini hayo yote, haiwezekani kuacha kamwe kutumainia.  Kwa maana hiyo Papa Francisko anarudia kutoa wito  ili mivutano kati ya Iran na Marekani isiweze kuongeza hatari, huku akiomba wakazie majadiliano na kuheshimu sheria za kimataifa.

Uhalifu wa manyanyaso dhidi ya watoto

Papa Francisko akigusia juu ya Siku ya Vijana Duniani huko Panama na mkutano wake na vijana hao, anakumbuka ni kwa jinsi gani idadi ilivyo kubwa ya watu wazima wakiwemo hata baadhi ya makleri ambao wamehusika na uhalifu mbaya dhidi ya hadhi ya manyanyaso ya vijana na watoto. Huu ni uhalifu ambao unamkashifu Mungu na kusababisha madhara ya mwili, kisaikolojia na kiroho, na kwa maana hiyo Papa anakumbusha hata juu ya mkutano uliofanyika mwezi Februari mwaka jana mjini Vatican na upyaisho wa jitihada zinazofanywa kwa ajili ya kulinda watoto kwa njia ya uchunguzi na usimimamizi mkubwa ili kukabiliana na kesi hizi.

Kuundwa mapatano ya elimu na sifa kuu ya familia

Kwa kuendelea na hotuba Papa anakumbusha kuwa hayo ni majeraha na ambayo kwa hakika ni dharura na kuhitaji zoaezi la elimu. Na kwa maana hiyo anakumbusha juu ya tukio lijalo la tarehe 14 Mei  mwaka huu litakaloongozwa na mada: “Kuunda mapatano mapya ya ulimwenguni”. Neno kueleimisha  si kwamba linaishia darasani tu, bali ni kuhakikisha wanaongeza misingi ya nguvu ya haki, msingi wa familia katika kuelimisha na haki ya Makanisa na masharika ya kijamii katika kushirikiana  pamoja. Tunaishi katika dunia mahali ambamo tunataka kujifungua sisi wenyewe, kwa kulinda haki zilizo patikana bila kujali  wazee  na bila  kutoa nafasi tena kwa maisha  asili yanayozaliwa. “tendo la kuzeeka kwa jumla katika sehemu kubwa ya  watu ulimwenguni, hasa nchi za Magharibi, inawakilisha masikitiko anasema Papa kutokana na suala la utamaduni wa kibaguzi kwa wazee na watoto.

Uongofu wa ekolojia fungamani

Ni vijana kwa hakika ambao wanaweza kutoa mambo mengi kwa sababu ya shauku zao hasa katika mwonekano wao unaojionesha katika jitihada za sasa za kuhamasisha viongozi wa kisiasa juu ya masuala ya mazingira, anasema Papa  katika sulala lautunzaji wa nyumba yetu ya pamoja na ambayo  iwe ndiyo wajibu wa wasiwasi wa wote” na isiwe ni kitu kubishana na wala itikadi. Kwa hakika Papa anatoa wito wa dharura katika “Uongofu wa kiekolojia” kwa namna fungamani japokuwa  amebainisha masikitiko yake ya kutopatikana suluhisho la matokeo ya mkutano wa 25 wa wanachama kuhusu mabadiliko ya tabianchi, COP25, ambao ulifanyika katika mji mkuu Madrid nchini Hispania, mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka jana. Na kwa maana hiyo matokeo hayo yanawakilishadharura kubwa hasa ya kukabiliwa kwa namna ya hekima kwa upande wa Jumuiya ya kimataifa kufuatia na ongezeko la joto ulimwenguni.

Ukosefu wa usawa na ugonjwa sugu wa ufisadi kama mzizi wa mgogoro Amerika ya Kusini

Papa Francisko katika hotuba yake mtazamo wake pia umeangalia Bara la Amerika ya Kusnini na zaidi akitazama juu ya Sinodi ya  Amazoni na wasiwasi mkubwa kwa sababu ya viepo vingi na kinzani za kisiasa kuongezeka katika nchi hizo. Katika moyo wake Papa Francisko anataja nchi ya Venezuela  kwa matumaini ya kuweza kutafuta suluhisho la haraka. Kwa ujumla migogoro ya Kanda la Amerika ya Kusini pamoja na kuwa na miziz yake tofauti anasema nchi zinafafana kwa kika hasa katika masuala ya ukosefu wa haki na magonjwa sugu ya rushwa, ufisadi pamoja na mitindo ya umasikini ambao unaondoa hadhi ya mwanadamu. Hali hii inahitaji kwamba viongozi wa kisiasa wajibidishe  kuwa na msimamo hasa katika utamaduni wa majadiliano kwa ajili ya kutafuta wema wa pamoja  pia jitihada za taasisi mbalimbali za kidemokrasia katika kukuzaheshima kufuata sheria ili kuzuia  matukio hayo.

Majadiliano ya kidini na wito kwa ajili ya Yerusalem

Ziara ya pili ya Papa  kwa mwaka 2019 ilikuwa katika Nchi za Falme za Uarabuni. Katika ziara hiyo ya kitume ,lengo pia lilikuwa ni kutoa sahihi ya Mkataba juu ya Udugu wa Kibinadamu na Imam Mkuu wa Al-Azhar, na ili kusisitizia juu ya mantiki ya uzalendo, heshima ya uhuru wadini kwa kupinga kila aina za ubaguzi wa kidini , na kwa ajili ya kuundia wakati endelevu wa kizazi katika majadiliano mema ya kidini. Amani na matumaini pia yalikuwa ndiyo kauli mbiu ya Ziara ya Papa Francisko nchini Morocco na pia kutoa wito juu ya Yerusalemu, ili kutambua umoja na utakatifu na ambao ulitiwa a sahini na Mfalme Re Mohammed VI.  Katika hili Papa Francisko mawazo pia ni kwa ajili ya Nchi Takatifu akiomba msaada wa Jumuiya ya Kimataifa  kuendeleza mchakato wa amani kati ya Israeli na Palestina. Hata hivyo jitihada hizo pia ni dharura sana katika maeneo mengine ya nchi za Mashariki.

Hatari zitokanazo na ukimya wa vita nchini Siria

Ukimya hasa huo unahatarisha na kufunika vitaambavyo bado vinaendelea kuyumbisha nchi ya Siria kwa miaka 10 amesema Papa. na kwa mujibu wake anasema dharura hii ipate suluhisho la ujenzi wa amani kwa watu wa siria ambapo pia Papa anatoa pongezi wa nchi zile kama vile Yordani na Lebanonwanaoendelea kubeba mzigo  na ukarimu wa maelfu ya wakimbizi.

Mivutano ya Iran na Marekani

Akiendelea na mtazamo zaidi juu ya vurugu, bado mtazamo wake ni juu ya mivutano ya sasa. Ameabainisha wasi wasi wake juu ya kanda hizo zenye mivutano kati ya Iran na Marekani na pia ambayo inaunganisha hata Iraq , kwa maana hiyo anapyaisha  wito wake kwa  wahusika wote ili waepusha kuibua mzozo na kujikita katika  mijadala ya mazungumzo na kujithibiti ili kuzuia  moto, kwa heshima kamili ya sheriza za kimataifa

Manyanyaso dhidi ya wanaokimbia migogoro

Wasiwasi mkubwa wa Papa pia ni wa nchi ya Yemen ambayo inatishia maisha ya kibinadamu. Ameonesha bayana juu ya sintofahamu za Jumuiya ya Kimataifa, vile vile hata hali ya nchini Libya  iliyozidishwa na uchochezi wa uhalifu na kuwa ni ardhi yenye rutuba kwa janga la biashara ya wanadamu, ikichochewa na watu wasio na adabu ambao hunyonya umaskini na mateso ya wale wanaokimbia. Ulimwenguni kuna watu elfu kadhaa "ya watu walio na maombi halali hifadhi na  mahitaji ya kibinadamu na ulinzi wa  kuhakikishia watu na usalama. Na zaidi ameonesha ni kwa jinsi gani Bahari ya Mediterranea bado inabaki kuwa makaburi ya watu wengi na wakatihuo kuwa matumaini ya watu wengi na hivyo anazidi kusisitiza juu ya mataifa kutafuta suluhisho la kweli na la kudumu.

09 January 2020, 14:26