Tafuta

Vatican News
Tarehe 8 Januari 2020 Papa Francisko kwa mara nyingine tena ametoa tafakari ya katekesi katika ukumbi wa Paulo VI Tarehe 8 Januari 2020 Papa Francisko kwa mara nyingine tena ametoa tafakari ya katekesi katika ukumbi wa Paulo VI  (Vatican Media)

Papa Francisko:jifunze kukarimu dhidi ya sintofahamu

Sala ya mwisho ya Papa Francisko wakati wa kumaliza tafakari ya kateksi ameomba Bwana ili atusaidie kuishi kila jaribu kwa kusaidiwa na ile nguvu ya imani;kuwa makini na watu wengi manusuru wa historia za meli ambao hufika wamechoka kwenye miambao na hata sisi tutambue namna ya kuwakaribisha na upendo kidugu unatokana na kukutana na Yesu.Hii ndiyo inayookoa dhidi ya ubaridi wa kutojali na sintofahaamu za ubinadamu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Matatizo, imani, wema ulijaribiwa ambao unafanya moyo ufunguke na kuwa makini katika mshikamano kwa wengine ndiyo mada kuu iliyowekwa wazi na Papa Francisko wakati wa Tafakari ya Katekesi yake kwa waamini na mahujaji waliokusanyika katika Ukumbi wa Paulo VI Vatican tarehe 8 Januari 2020. Papa Francisko ameongozwa na sehemu ya Somo la Matendo ya Mitume linalohusu kupotea katika merikebu. “Merikebu iliposhikwa, na kutoweza kushindana na upepo, tukaiacha tukachukuliwa. Na walipokuwa wamekaa wakati mwingi bila kula chakula, Paulo akasimama katikati yao, akasema, Wanaume, iliwapasa kunisikiliza mimi na kutokung'oa nanga huko Krete, na kupata madhara haya na hasara hii. Sasa nawapeni shauri, iweni na moyo mkuu, kwa maana hapana hata nafsi mmoja miongoni mwenu itakayopotea, ila merikebu tu. Kwa maana usiku huu wa leo malaika wa Mungu yule ambaye mimi ni wake, naye ndiye nimwabuduye, alisimama karibu nami, akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe” (Mdo 27, 15.21-24.

Mwanzo wa safari ya Paulo katika bahari haukuwa mzuri

Papa Francisko akianza amesema katika Kitabu cha Matendo ya Mitume, sehemu ya mwisho inasimulia kuwa Injili inaendelea na mbio yake na si tu katika ardhi, lakini hata baharini, katika merikebu iliyokuwa imemchukua Paulo gerezani kutoka Kaisari kuelekea  Roma (Rej Mdo 27,1–28,16), katika Moyo wa Falme ili kutimiza Neno la Mfufuka lisemalo “ninyi mtakuwa mashahidi wangu…() hadi miisho ya dunia( Mdo1,8). Kufuatia hilo Papa Francisko ameshauri kusoma kitabu cha Matendo ya Mitume na kwamba wataona ni jinsi gani Injili na nguvu ya Roho Mtakatifu inavyo wafikia watu wote ulimwengu. Tangu mwanzo wa safari yao haukuwa mzuri kwa sababu ya upepo mkali. Safari ilikuwa na hatari na Paulo anashauri kutoendelea na safari hiyo, lakini akida akawasilikiliza nahodha na mwenye merikebu zaidi ya yale aliyosema Paulo.

Hatari ya upepo na dhoruba katika safari ya Paulo

Safari ikaendelea lakini upepo wa nguvu kwa namna ya tufe merikebu ikashikwa na kushindwa kuendelea na kuwaacha pwani. Kifo kilipokuwa kinakaribia na mahangaiko kuwapata wote, ndipo Paulo akaikingilia kati na kuwahakikishia wenzake kwamba “hapana hata nafsi mmoja miongoni mwenu itakayopotea, ila merikebu tu” . Kwa maana usiku huu wa leo malaika wa Mungu yule ambaye mimi ni wake, naye ndiye nimwabuduye, alisimama karibu nami, akaniambia, Usiogope, Paulo, huna budi kusimama mbele ya Kaisari; tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe. (Mdo 27,23-24). Papa Francisko ameongeza kusema hata katika majaribu Paulo hakosi kuwa mlinzi wa maisha ya wengine na kuwatia moyo wa matumaini. Luka anatuonyesha namna hii ya ishara inayomwongoza Paulo kulekea Roma na kumwokoa si Mtume peke yake lakini hata wenzake anaosafiri nao, dhidi balaa na kuigeuza kuwa fursa ya msaada wa Mungu kwa ajili ya kuhubiri Injili.

Kisiwa cha Malta kilionesha ukarimu kwa kundi la Mtakatifu Paulo

Manusuru hao sasa waliendelea katika kisiwa cha Malta mahali ambapo wakazi walionesha ukarimu na kuwapokea. Watu wa Malta ni wema na wapole wanajua kukarimu tangu mwanzo, Papa Francisko amewapongeza. Kuna mvua na baridi sana wanawasha moto kwa ajili ya manusuru na kuwapa joto kidogo na faraja. Hata hapa Paulo kama mfuasi wa kweli wa Kristo, anajikita katika kutoa huduma kwa ajili ya kuongeza moto kwa kutumia vijiti anavyo viokota. Katika harakari hizo zote Paulo akaumwa na nyoka, lakini haikumdhuru. Watu, wakitazama ishara hiyo walianza kujiuliza na kusema hivi huyu lazima atakuwa mhalifu mkubwa kwa sababu anajiokoa kutoka kwenye meli iliyoanguka na anaishia kuumwa na nyoka. Tulikuwa tunasubiri kwa muda yeye afe, lakini hakuguswa na uharibifu wowote na kwa maana hiyo Papa anaongeza kusema: Paulo anageuzwa hata jina la kuwa mhalifu. Na kumbe kiukweli wokovu huo unatoka kwa Bwana Mfufuka ambaye anamsadia kwa mujibu wa ahadi aliyo itoa kwa waamini wake kabla ya kupaa mbinguni kwamba: “Mtashika nyoka mikononi na hata kama mtakunywa sumu hamtadhurika; mtawawekea juu mikono yenu na hawa watapona” (Mc 16,18).  Kuhusiana na historia hiyo inasemekana kwamba, tangu wakati huo nchini Malta hakuna nyoka na hii ni baraka ya Mungu kwa sababu ya ukarimu wa watu hawa wema amebainisha Papa Francisko.

Fursa ya ugeni wa Mtakatifu Paulo unatoa mwafaka wa kutangaza neno na huduma ya huruma

Kwa hakika kukaa kwa Paulo katika kisiwa cha Malta ilikuwa ni fursa na muafaka wa kutoa neno ambalo lilitangazwa kwa njia ya huduma ya huruma katika uponyaji wa wagojwa. Hii ni sheria ya Injili. Ikiwa mwamini anafanya uzoefu wa wokovu hawezi kuuhifadhi peke yake, bali anauweka katika mzunguko. Wema daima una tabia ya kuwasilishwa. Kila uzoefu wa kweli na uzuri unatafuta njia yake ya kujipanua na kila mtu anayeishi kwa kina uhuru wa ndani anapata hisia kubwa mbele ya mahitaji ya wengine ( Rej, Wosia Evangelii gaudium, 9). Mkristo aliyejaribiwa anaweza kwa mara nyingie kuwa na ukaribu zaidi na yule anayeteseka kwa sababu anatambua nini maana ya mateso na kuwa na moyo ulio wazi na umakini zaidi katika mshikamano kwa ajili ya wengine. Paulo anatufundisha kuishi majaribu huku tukimfumbata Yesu, ili kukomaa ule uhakika kwamba Mungu anatenda kila kitu hata katikati ya mambo yanayoonekana kushindwa na uhakika ambao kwa yule anayeteseka na kujitoa kwa Mungu kwa upendo na kwa hakika yatakuwa na matunda.

Upendo kwa Mungu unatoa matunda

Upendo daima una matunda na upendo kwa Mungu daima unatoa matunda, ikiwa wewe unajiachia kuchukuliwa na Bwana na ikiwa wewe unapokea zawadi ya Bwana hiyo itakufanya kuwapatia hata wengine kwa maana zawadi inakwenda zaidi ya mambo mengine yote. Tuombe Bwana leo hii atusaidie kuishi kila jaribu kwa kusaidiwa na ile nguvu ya imani; kuwa makini na watu wengi manusuru wa historia za meli ambao hufika wamechoka kwenye miambao yetu ili hata sisi tutambue namna ya kuwakaribisha kwa upendo huo wa kidugu ambao unatokana na kukutana na Yesu. Hii ndiyo inayookoa dhidi ya ubaridi ya kutojali na sintofahaamu sisizo za kibinadamu na zisizo na ubinadamu.

KATEKESI

 

08 January 2020, 13:34