Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wajumbe wa chama cha Kitaifa cha wafanyakazi wazee Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wajumbe wa chama cha Kitaifa cha wafanyakazi wazee  (Vatican Media)

Baba Mtakatifu Francisko:Wazee katika ngazi kijamii wasidhaniwe kama mzigo!

Watu wazee,katika ngazi kijamii hawapaswi kufikiriwa kama mzigo na badala yake ni rasilimali na utajiri wa kweli.Hiyo inajionesha katika uhusiano wao wa shughuli za kujitolea ambayo ni fursa mwafaka na thamani jwa ajili ya kuishi ukuu wa kujitoa bure.Ni hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 16 Desemba 2019 alipokutana na wajumbe wa Chama kitaifa cha wafanyazi wazee ikiwa ni fursa ya kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Chama hiki.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 16 Desemba 2019 amekutana na wajumbe wa Chama kitaifa cha wafanyazi wazee ikiwa ni fursa ya kuadhimisha miak 70 tangu kuanzishwa kwa Chama hiki. Katika hotuba yake ametaka kuanzia juu ya mkazo wa hotuba ya Rais wa Chama hicho aliyotoa kuhusu suala la uzee kama kipindi mwafaka cha zawadi,  hata kipindi cha majadiliano. Watu wazee, Baba Mtakatifu amesema katika ngazi kijamii hawapaswi kufikiriwa kama mzigo na badala yake kama rasilimali na utajiri wa kweli. Hiyo inajionesha katika uhusiano wao wa shughuli za kujitolea ambayo ni fursa mwafaka na thamani kubwa  kwa ajili ya kuishi ukuu wa kujitoa bure. Wazee ambao wako katika hali nzuri ya afya wanaweza kutoa muda wao kuwasaidia watu wengine ambao wanahitaji msaad,na kwa maana hiyo kujitajirisha hata wenyewe binafsi. Tendo la kujotolea ni uzoefu ambao unaleta wema kwa yule anayepokea lakini pia hata anayejitoa.

Jitihada ya kujitolea zinapinga tabia ya upweke na kubaguliwa

Kwa hakika jitihada ya kusaidia wengine ina uwezo wa kupingana na tabia ya upweke na kuboresha hali halisi ya ustawi wa wema na wa kiakili. Kwa maneno mengine jitihada za kujitoa zinahamasisha kile ambacho kinaelezwa kuwa ni uzee hai kwa kuchangia kuboresha hali ya maisha na kwa mara nyingine  tena mahali ambapo panakosekana ukuu wa umuhumu wa utambulisho kama nafasi ya wazee au taaluma ya waliostaafu.

Miaka hii, jitihada za wazee wa kujitolea zimeongezeka

Baba Mtakatifu Francisko anabinisha kwamba kwa miaka hii imejionesha ukuaji wa jitihada za wazee katika kujitolea na kuundwa kwa vyama vingi, kama kipaumbembe cha ujenzi wa jumuiya ya mshikamano. Kwa miaka 70 ya Chama chao kimeonesha wazi kama wazee wenye kuwa  na uwezo wa kujitosheleza kukua  na kushirikishana. Hata hivyo changamoto kubwa kwa wakati endelevu itakayojionesha ni kuhamasisha kwa dhati na daima rasilimali za kibinadamu ambazo zinapelekea wazee ndani ya jumuiya. Hii inatakiwa kuanzisha katika maeneo mahalia, mitandao ya mshikamano ambayo ipo kama kiongozi kwa wazee ambao ndiyo wako mstari wa mbele na si tu kama vitu vya kusaidia. Itakuwa ni muhimu wazee waweze kufikiriwa kama wahukusika na siyo wahitaji kwa maana  ndiyo wali  mstari wa mbele au kama isemavyo Biblia ( waota ndoto ( Gl 3,1).  Hizo ni doto  zilizo beba na kumbukumbu na siyo zilizo tupu, sisizo na maana kama vile baadhi ya matangazo ya biashara, Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza. Ndoto za wazee zina thamani kubwa ya kumbukumbu na kwa maana hiyo ni msingi katika safari ya vijana.

Uzee ni kama kipindi cha majadiliano

Baba Mtakatifu Francisko akifafanua mantiki ya pili ya uzee kama kipindi cha majadiliano amesema,  wakati endelevu wa watu unahitaji majadiliano na makutano kati ya wazeee na vijana kwa ajili ya kujenga jamii yneye ya haki, nzuri, yenye mshikamano zaidi na ya kikristo zaidi. Vijana ni nguvu ya safari ya watu na wazeee wanaimarisha nguvu kwa njia ya kumbu kumbu na hekima. Uzee ni kipindi cha neema ambacho Bwana anapyaisha na wito wake. Bwana anatuita kuwa na uvumilivu na kurithisha imani, analika kusalia hasa kwa kuomba, anatuosha kuwa karibu na wale wote wanaohitaji. Wazee, babu wanao uwezo wa pekee na maalum wa kupokea hali halisi ya matatizo. Wakati wanaposali, kwa ajili ya hali hizo sala zao zina nguvu na sana. Kwa maana hiyo  babu zetu waliopokea baraka ya kuona watoto wa watoto wao (Zab 128,6) na kukubidhiwa kazi kubwa ya kurithisha uzoefu wa maisha, historia ya familia katika jumuiya na katika watu. Kwa kufikiria na kuishi na uzee kama kipindi cha zawadi na kipindi cha majadiliano, itapingana na mazoea  na kasumba ya kiutamaduni kuhusu mzee, mgonjwa, mlemavu, anayetegemea, aliye na upweke, aliyejaa hofu, kwa utambulisho wa udhaifu wa kupoteza nafasi katika jamii.  Na wakati huo huo itasaidia kuzuia ule umakini kwa ujumla unaojitokeza kuhusiana na gharama na hatari na zaidi kuona rasilimali na nguvu za wazee.

Mara nyingi upo hata ubaguzi kwa vijana kwa sababu hawana ajira

Kuhusiana na hilo Baba Mtakatifu Francisko ameonesha kwamba kwa bahati mbaya mara nyingi wanabagua hata vijana kwa sababu hawana ajira, wanabagua wazee kwa kusingizia namna ya kuwatunza katika mfumo wa uchumi uliotengemaa ambao kiini chake hakuna nafasi ya ubinadamu na  badala yake ni kufikiria fedha tu. Wote kwa pamoja tunaalikwa kupingana na sumu hii ya utamaduni wa ubaguzi. Tunaalikwa kujenga kwa pamoja jamii tofauti, yenye kukaribisha zaidi, ya kibinadamu zaidi, inayounganisha zaidi na ambayo haina haja ya kubagua aliye mdhaifu katika mwili na katika akili, badala yeke jamii ambayo inajipima katika hatua njema ni ile ambayo inaangaikia watu hao! Baba Mtakatifu Francisko amehitimisha kwa kuwashukuru kwa kile ambacho wanafanya katika nyanja ya kuhamasisha watu wazee. Anawatakia kila mahali walipo wawe ni furaha na hekima; kuwa na hali ya hekima na uzoefu wa wazee ili kuweza kujenga dunia ambayo inaheshimu zaidi haki za wote. Waendelee kwa ujasiri kuupeleka katika mazingira mbalimbali ambamo wanafanya ushuhuda wa thamani. Kwa upande wake anawasindikiza kwa sala na kuwabariki  kwa Baraka ya Bwana juu ya mapendekezo na mipango yao ya wema.

16 December 2019, 15:00