Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu amekutana na sekretarieti ya Vatican kwa ajili ya Matashi mema ya Kuzaliwa kwa Bwana ambapo katika hotuba amesisitizia juu ya mageuzi ya Vatican Baba Mtakatifu amekutana na sekretarieti ya Vatican kwa ajili ya Matashi mema ya Kuzaliwa kwa Bwana ambapo katika hotuba amesisitizia juu ya mageuzi ya Vatican   (Vatican Media)

Papa Francisko:mageuzi ni kwa ajili ya kutoa huduma bora ya binadamu!

Katika utamaduni wa kukutana kwa ajili ya matashi mema ya kila mwaka katika Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana,PapaFrancisko amezungumza na Sekretarieti kuu ya Vatican,Jumamosi 21 Desemba 2019. Katika mazungumzo amejikita kuhusu mageuzi yanayondelea katika taasisi za Vatican na kusisitizia umuhimu na lengo la mabaraza mapya.Tunafanya mageuzi anasema Papa ili kushinda ule ugumu na hofu na kuweza kutangaza Injili vema katika dunia inayokwenda mbali na ukristo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Jumamosi tarehe 21 Desemba 2019 wakati wa mkutano kwa ajili ya kutakiana matashi mema ya Sherehe za Kuzaliwa kwa Bwana, Kardinali Angelo Sodano, Dekano wa Makardinali kwa niaba ya viongozi na wafanyakazi wa Sekretarieti kuu ya Vatican, amemtakia heri, baraka na afya njema, Baba Mtakatifu Francisko wakati huu wa maadhimisho ya kuzaliwa kwa Bwana. Na Baba Mtakatifu Francisko akianza hotuba yake pia amemshukuru Kardinali Sodano kwa hotuba yake na kuwatakia kila la heri wote ya Sikukuu hizi. Na katika ulimwengu unaobadilika, Sekretarieti ya Vatican haibadilishwi kwa sababu ya kufuata  mkumbo wa mitindo ya kisasa. Maendeleo na ukuaji wa Kanisa unakua pale ambapo yapo matazamio ya Mungu na historia ya Biblia ni kila kitu katika kuendelea na kuanza kwa upya. Na ndiyo maana hata watakatifu wapya kama Kardinali Newman anapozungumza juu ya wmabadiliko kwa hakika alikuwa na maana ya uongofu, amesema Baba Mtakatifu Francisko.

Changamoto na kuacha kila kitu kilivyo

Hata hivyo kabla ya kuwanza hotuba yake juu ya mada yenyewe iliyoko moyoni mwake, Baba Mtakatifu Francisko amewaandaa wasikilizaji wake katika Chumba cha Mkutano cha Clementina ili kuwatakiwa matashi mema kama wahudumu wake wa kwanza wa Sekretarieti kuu Vatican ambao wanamsaidia kwa karibu kuleta ule upamoja, maelewano na uhakika wa kile ambacho kinahitajika kwa  kisindikizwa tangu mwanzo wa utume wake.  Lakini pia  ni nyakati za mabadiliko ya sasa ambayo siyo rahisi  ambayo ni mageuzi ya wakati huu. Baba Mtakatifu Francisko amesema kwamba tabia iliyo bora ni ile hasa ya  kuacha kujiuliza juu ya changamoto za sasa na ili kuweza  kufanya mang’amuzi na ujasiri zaidi kuliko kudanganywa na hali nzuri na kuacha kila kitu kibaki jinsi kilivyo. Baba Mtakatifu Francisko amesema, hiyo inatokea mara nyingi ya kuishi mageuzi huku wanajizuia kuvaa nguo iliyo mpya na badala yake kutaka kubaki katika hali halisi kama ilivyokuwa mwanzo. Kwa kutaka kufafanua zaidi Baba Mtakatifu Francisko ametumia mfano wa kulalamika kama alioutumia mwandishi wa kitabu mwitaliano “ Il Gattopardo” cha Giuseppe Tomasi wa  Lampedusa asemaye kuwa: “iwapo tunataka kila kitu kibaki jinsi kilivyo, ni lazima kila kitu kibadilike”.

Katika mapya na kumbu kumbu

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na hotuba yake amejikita katika mada ya mageuzi kwa dhati ya Sekretarieti kuu ambayo anathibitisha kwamba  haijawahi kujidai kufanya kana kwamba hakuna kilichokuwapo tangu mwanzo na kinyume chake imeweza kuthamanisha kile kilicho chema na imeweza kutengeneza historia ya sekretarieti kwa ujumla wake. Ni muhimu sana kuthamanisha historia kwa ajili ya kujenga wakati ujao wenye msimamo na ambao una mizizi, amesisitiza Baba Mtakatifu na hivyo kuufanya uweze kuzaa matunda! Katika kutoa wito juu ya kufanya kumbu kumbu hakuna maana ya kushikilia  hifadhi, bali ni katika  kutoa wito katika maisha na uhai wa michakato inayoendelea ya maendeleo. Kumbu kumbu haisimami, badala yake iko katika mwendo. Hii ina maana ya asili yake katika mwendo.

Kubadilisha kwa ajili ya kutangaza

Baba Mtakatifu Francisko aidha amejikita kufafanua kile kinachojieleza kwa baadhi ya mambo  mapya ya Mabaraza ya kipapa kama ile ya kuzaliwa kwa kitengo cha tatu cha Ukatibu kwenye Makao makuu Vatican  (Kitengo katika nafasi ya kidiplomasia ya Vatican), mwishoni mwa mwaka 2017, pamoja na mabadiliko mengine ambayo yalitokea. Amekumbusha  uhusiano kati ya Sekretarieti na Kanisa mahalia  na katika muundo wa baadhi ya Mabaraza ya Kipapa kwa namna ya pekee ya Makanisa ya Mashariki na kwa ajili ya Mazungumzo ya kiekuemene na kidini, kwa namna ya “Kiyahudi”. Vile vile zaidi mtazamo  huo, anasema ulikuwa tayari upo katika kipindi cha Mtakatifu Yohane Paulo II na ambapo Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI aliuelezea kwamba ni ulimwengu wa sasa ambao hautambui Injili tena kama zamani na kwa maana hiyo Baba Mtakatifu Francisko amefafanua juu ya muundo wa kina wa Mabaraza ya kihistoria na  ushauri wa kuzaliwa kwa mambo mapya.

Akigusia juu ya Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na Baraza la Kipapa la Uinjilishi wa watu, amebainisha kuwa tangu yalipoanzishwa kwa wakati ule yalikuwa ni rahisi sana kutofautisha kati ya pande mbili zilizofafanuliwa kwa usawa. Kwa sehemu ya  kwanza ulikuwa kama “ dunia ya kikristo na upande mwingine ulionekana kama dunia ambayo bado inapaswa kuinjilishwa”. Lakini kwa sasa hali hiyo haipo tena. Watu ambao bado hawajapata tangazo la Injili hawaishi tena katika Mabara ya magharibi tu, bali wanaishi kila mahali, hasa katika mkusanyiko wa viwango vikubwa vya mijini ambavyo vinahitaji utunzaji maalum sawa sawa wa kichungaji. Katika miji mikubwa tunahitaji dhana nyingine ili iweze kutusaidia kuweka upya njia zetu za fikra na mitazamo yetu. Amesistiza Baba Mtakatifu Francisko!

Injili na utamaduni wa kidigitali

Kwa maana hiyo ili kuunda mfumo wa taasisi za Vatican ilikuwa na msukomo wa kupyaisha tangazo la Injili. Yote ni kama kawaida, mitindo, muda, lugha, kama alivyokuwa amekwisha sema  Baba Mtakatifu katika Waraka wa 'Evangelii gaudium'  ya kwamba “ tunapaswa kuwa mkondo unaostahili wa uinjilishaji katika dunia ya sasa zaidi ya kujiokoa”. Katika hili, Baba Mtakatifu Francisko anasema kuzaliwa kwa Baraza la Kipapa la Mawasiliano, ni chombo ambacho kinaunganisha  pamoja vyombo tisa vya  habari vya Vatican, vilivyokuwapo  awali. Na siyo kikundi cha uratibu wa idadi, bali kwa namna ya kuweka pamoja ili kuelekeza katika obora zaidi wa huduma ya pamoja na ambayo ni  utamaduni mkubwa wa kidigitali. Utamaduni mpya, unaojikita na mambo mengi ya kuunganishwa na vyombo vya habari, unahitaji kutoa jibu linalostahili kwa upande wa Makao ya Kitume Vatican kwenye muktadha wa mawasiliano. Leo hii kulingananisha na huduma mbalimbali, inaonesha wazi mfumo wa vyombo vya habari vilivyo vingi ,  hiyo inaashiria njia ya kutambua, kufikiria na kutekeleza. Yote hayo yanahitaji mabadiliko ya pamoja  ya utamaduni, uongofu wa taasisi na wafanyakazi ili kubadili kazi katika vyumba vyao kwa kesi za kuboresha na ambayo uratibu wake  wa kazi inaunganika kwa ndani, katika umoja na mkakati.

Muundo mmoja na huduma nyingi

Mabadiliko hayo pia yaligusa Baraza la Kipapa la Huduma fungamani ya watu iliyoundwa kwa dhati na umoja wa kazi na kuungana na Baraza la kipapa la Haki na Amani na Cor Unum, Uchungaji wa Wahamiaji na wahudumu wa Afya. Kanisa kwa maana hiyo linaitwa kukumbusha kwa wote kuwa, hii siyo masuala ya kijamii au uhamiaji, bali ya watu kibinadamu, ya ndugu kaka na dada ambao leo hii ni ishara kwa wote wanaobaguliwa na jamii iliyobobea malimwengu. Kanisa linaalikwa kushuhudia ya kwamba “kwa Mungu hakuna aliye mgeni au kubaguliwa”. Kanisa linaalikwa kuamsha dhamiri zilizolala katika sintofahamu mbele ya hali halisi ya Bahari ya kimediterranea ambayo kwa wengi sana imekuwa eneo la makaburini.

Upendo unashinda uchovu

Kati ya changamoto na ulazima wa kuwa na msimamo, kwa maana ya kile kinachohesabiwa ni Kanisa Baba Mtakatifu anabainisha  na Sekretarieti kwanza inatazama ubinadamu ambao sisi sote ni wana wa Baba mmoja. Aidha  hakukosa kubanisha juu ya matatizo ya mageuzi makubwa, hata ulazima wa kwenda hatua kwa hatua, kwa maana ya makosa ya kibinadamu  ambayo amesema: haiwezekani na siyo haki kutozingatia. Kuhusiana na matatizo hayo ya mchakato wa kihistoria ambao daima kumekuwa na unyanyapaa  na vishawishi  vya kutaka kurudi nyuma katika wakati uliopita (hata kwa kutumia mitindo mipya) kwa sababu inaimarisha zaidi, inajulikana na kwa hakika, haina migogoro mingi.

Inahitaji umakini na kuwajibika dhidi ya ugumu

Inahitaji kuwa na umakini zaidi wa kuwajibika dhidi ya tabia za ugumu, amebainisha Baba Mtakatifu. Ugumu unazaliwa kutokana na hofu ya kuwa na mabadiliko na kuishia kujitengeneza vigenzo  kwa kutoa au vizingiti chini ya ardhi ya wema wa pamoja na kuifanya kuwa ugumu na uwanja  wa chuki na kutengwa. Siku zote tukumbuke kuwa nyuma ya kila ugumu unalala uongo katika kutokuwa na msimamo. Ugumu na ukosefu wa msimamo unakuzwa kwa pamoja kwenye duara mbaya. Neno la mwisho la Baba Mtakatifu Francisko amewaachia takafakari ya Kardinali Martini ambaye katika mtazamo wa kifo alithibitisha kuwa: Kanisa limebaki nyuma kwa miaka miambili. Ni kwanini halitikisiki? Tuna hofu? Hofu kinyume chake ni ujasiri? Kwa maana hiyo imani ni msingi wa Kanisa. Ili kusaidia, imani na ujasiri (…) ni upendo tu unaoshinda uchovu!

 

 

21 December 2019, 12:19