Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake kwa washiriki wa Tamasha la Mafundisho Jamii ya Kanisa linalofanyika kuanzia tarehe 21-24 Novemba 2019 mjini Verona,Italia Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake kwa washiriki wa Tamasha la Mafundisho Jamii ya Kanisa linalofanyika kuanzia tarehe 21-24 Novemba 2019 mjini Verona,Italia 

Kutazama,kusimama na kugusa ina maana ya uwepo na sauti moja ya kijamii!

Katika ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa washiriki wa Tamasha la IX la Mafundisho Jamii ya Kanisa,huko Verona nchini Italia tarehe 21 Novemba kuhusu mada ya kuwapo:sauti moja ya jamii, amewashauri maana hiyo kwa maneno matatu:kutazama,kusimama na kugusa.Anawaalika wasuke kitambaa cha kijamii.Kutatua tatizo hakuhitaji meneja mkuu bali ni kubaki wameungana katika jitihada bila kuangukia katika sintofahamu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake kwa njia ya video  katika Tamasha la IX la Mafundisho Jamii ya Kanisa linalofanyika kuanzia tarehe 21-24 Novemba 2019 katika Kituo cha Kikatoliki huko Verona nchini Italia. Tamasha hilo kwa mwaka huu linaongozwa na  kauli mbiu isemayo,“kuwapo:sauti moja ya kijamii.” Katika ujumbe wake Baba Mtakatifu Francisko anasema kwammbaNinaanza kuwasalimia washiriki wote katika toleo hili la tisa la Tamasha la Mafundisho jamii ya Kanisa. Mada mliyoichagua mwaka huu ni  “Kuwepo:sauti moja ya kijamii”. Uwepo siyo jambo  la kinadharia, bali kimwili na kwa dhati. Uwepo wa uamuzi ni mwafaka na  ambao kila mmoja alijaribu kwa sababu wote tunatambua utofauti uliopo kati ya kuwa peke yako na kuwa na mtu mwingine karibu. Kuwepo maana yake ni kutoa ule upweke na kufanya joto la kibinadamu lifike ambalo linatoa ari na sababu ya kuishi kwa wale tunaokutana nao. Uwepo unasaidia kumwona mwingine na kumfanya yeye akuone na kutoa chachu katika mahusiano ambayo yanatia joto katika maisha. Kuwepo maana yake ni kubaki macho wazi ili kuzuia mwingine hasibaki kabaguliwa kwa mtazamo wetu. Mtu hasiyeonekana na yoyote, anawekwa katika mzunguko wa wale wasio onekana na ambao ni kama vile wagonjwa waliobaguliwa, masikini, waliotengwa na wanaonyonywa.

Tendo la kutowatazama ni namna ya kufanya haraka ili kuondokana na matatizo, japokuwa wao wapo, na  hata kujifanya kutowaona wao wakati wanaishi anasisitiza Baba Mtakatifu Francisko. Kuwepo maana yake ni kuchukua jukumu la kuanzisha kutembea hatua moja ili kwenda kukutana katika makona ya njia, mahali ambapo wengi wanapatikana  na waliobaguliwa. Ni vema kufikiria uwepo ambao umeenezwa na ambao unakaa katika maeneo mengi ili kupeleka huruma na kazi kama ile ya chachu. Chachu ikichanganywa katika unga wa kibinadamu aliye tayari ili kuchukua majukumu ya kumtunza ndugu. Kutokana na hiyo Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kwamba, maana ya uwepo tunaweza kwa namna ya pekee kuitazama katika maneno matatu: kutazama, kusimama na kugusa. Baba Mtakatifu Francisko akianza kufafanua juu ya neno la kwanza ambalo ni kutazama anasema:Kutazama ni hatua ya kwanza ambayo inasaidia kutoka ndani mwetu  binafsi ili kuweza kutazama uso kwa uso maisha kwa namna hiyo yanavyojiwakilisha. Yale ambayo tunaona yanaweza kutuogopsha na kutufanya tutoroke na kukataa kile ambacho tumekiona.

Kutazama mahali pengine, vile vile inahitaji kusimama: Uwepo maana yake siyo wa kukimbia, badala  yake ni kukaa na mwingne. Kukimbia hakufanyi utambue sura nyingi na mitazamo mingi. Je ni watu wangapi katika maisha wametambua wakiwa wamechelewa kwamba walikuwa wanakimbia na hawakupata muda wa kuweza kusimama na kucheza na watoto wao binafsi, hawakuweza kujadiliana na wazazi wao wazee, kuwatunza kwa upendo, kuwajibika kwa kuwatunza. Unapomtakia mtu mwingine mema unahisi shauku ya nguvu ya kukaa naye na siyo kukimbilia mahali pengine.

Na hatimaye, uwepo wa mtu unajieleza hata katika kugusa, ili kuweza kuonfoa ule umbali na mwingine, kumwonesha lile joto na kubeba mzigo na katika kutunza. Uwepo kwa namna ya  utambuzi ni upole na majadiliano pia ni kwa ajili ya wote. Ili kutatua matatizo, haina  haja ya kutafuta meneja mkubwa au watu wenye nguvu, lakini ni lazima kuunganisha jitihada bila kubaki na sintofahamu. Kila mmoja na ubora wake na zawadi zake anaweza kugeuka kuwa mjenzi wa udugu. Dunia inabadilika na siyo mtu anafanya miujiza, bali ikiwa wote kila siku wanafanya kile ambacho wanapaswa kutenda. Mabadiliko ya kudumu yanaanzia daima chini, hayajawahi kuanzia na kazi juu. Kuna haja ya wote katika kujenga maisha ya kijamii na kutambua nguvu ya nini maana ya kuwa watu. Katika mtazamo huo watu wote ni muhimu. Kuanzia wagonjwa, masikini, watoto, wazee, wafanyakazi, wataalam, wajasiliamali, wenye maarifa na wasio elimika.

Baba Mtakatifu Francisko aidha anasisitiza kwamba ni dharura na msizuie uhuru wa kutenda wema. Katika nchi yetu inamtunza mwenye kuhitaji. Ninawatakia ninyi nyote washiriki wa Tamasha la Mafundisho Jamii ya Kanisa kuwa wasukaji wa kitambaa cha kijamii ambacho uwepo wake unageuka kuwa zawadi inayofanya kung’aa kwa uzuri wa kindugu. Baba Mtakatifu Francisko anahitimisha kwa kusema kuwa: Ninapyaisha salam zangu za dhati kwa washiriki wa Tamasha la Tisa la Mafundisho Jamii ya Kanisa na kwa namna ya pekee watu wengi wa kujitolea ambao wanajitoa uwezekano wao bila kujibakiza. Anamsalimia Askofu wa  Verona, Askofu  Giuseppe Zenti, ambaye amekaribisha tukio hili na kumshukuru Padre Vincenzi kwa ajili ya huduma aliyofanya kwa ajili ya kuendza, utambuzi na kufanya uzoefu wa mafundisho Jamii ya Kanisa.

PAPA VIDEO-VERONA
22 November 2019, 11:23