Tafuta

Vatican News
Katika kipindi cha Mwaka 2018-2019: Makardinali 13 na Maaskofu 147 wamefariki dunia: Kutoka AMECEA ni: Maaskofu:  J.Jenga, E.M. Chengula, G. Mmole na E. Mapunda. Katika kipindi cha Mwaka 2018-2019: Makardinali 13 na Maaskofu 147 wamefariki dunia: Kutoka AMECEA ni: Maaskofu: J.Jenga, E.M. Chengula, G. Mmole na E. Mapunda.  (ANSA)

Makardinali na Maaskofu waliofariki dunia 2018-2019

Baba Mtakatifu tarehe 4 Novemba 2019 amewakumbuka na kuwaombea Marehemu Makardinali na Maaskofu waliofariki dunia katika kipindi cha Mwaka 2018-2019. Takwimu zinaonesha kwamba, katika kipindi hiki, Makardinali 13 wamefariki dunia pamoja na Maaskofu 147. Kanisa Barani Afrika limewapoteza Maaskofu 21 kati yao kuna Maaskofu wanne kutoka katika nchi za AMECEA.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 4 Novemba 2019 ameadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican kwa ajili ya kuwakumbuka na kuwaombea Marehemu Makardinali na Maaskofu waliofariki dunia katika kipindi cha Mwaka 2018-2019. Takwimu zinaonesha kwamba, katika kipindi hiki, Makardinali 13 wamefariki dunia pamoja na Maaskofu 147 kutoka sehemu mbali mbali za dunia. Kanisa Barani Afrika limewapoteza Maaskofu 21 kati yao kuna Maaskofu wane kutoka Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati, AMECEA. Hawa ni Askofu mstaafu John Njenga wa Jimbo kuu la Mombasa, Kenya, Askofu Evarist Marcus Chengula wa Jimbo kuu la Mbeya, Tanzania, Askofu Mstaafu Gabriel Mmole wa Jimbo Katoliki la Mtwara pamoja na Askofu Emmanuel Mapunda wa Jimbo Katoliki Mbinga, Tanzania. Katika orodha hii yumo pia Askofu mkuu Léon Kalenga Badikebele, aliyekuwa Balozi wa Vatican nchini Argentina ambaye alifariki dunia, tarehe 12 Juni 2019 huko nchini Argentina.

Ifuatayo ni Orodha ya Majina ya Maaskofu waliofariki dunia kati ya Mwaka 2018-2019 kutoka Barani Afrika: Askofu Valentin Masengo Nkinda wa Jimbo Katoliki la Kabinda, DRC. Askofu Roger Victor Solo Rakotondajao wa Jimbo Katoliki la Mahanga, nchini Madagascar. Askofu Mstaafu John Njenga wa Jimbo kuu la Mombasa, Kenya. Askofu Evaristo Marcus Chengula wa Jimbo Katoliki la Mbeya, Tanzania. Askofu Patrick Daniel Koroma wa Jimbo Katoliki la Kenema, Sierra Leone. Askofu Boniface Tshosa Setlalekgosi wa Jimbo Katoliki Gabrone, Botswana. Askofu Joachim Mbadu Kikhela Kupika wa Jimbo Katoliki la Boma, DRC. Askofu Paul Kouassivi Vieira wa Jimbo Katoliki la Benin, nchini Benin. Askofu mstaafu Michele Russo, M.C.C.J., wa Jimbo Katoliki la Doba, Ciad. Katika Orodha hii kuna: Askofu mstaafu Gabriel Mmole wa Jimbo Katoliki la Mtwara, Tanzania. Askofu mstaafu Emmanuel Alex Mapunda wa Jimbo Katoliki Mbinga, Tanzania. Askofu Francisco Lerma Martinez, IMC wa Jimbo katoliki la Guruè, Msumbiji.

Orodha hii inapambwa na: Askofu Antoine Konè wa Jimbo Katoliki la Odiennè, Pwani ya Pembe. Askofu mstaafu Kevin J. Aje wa Jimbo Katoliki Sokoto, Nigeria. Askofu Giuseppe Sandri, M.CC.J.,  wa Jimbo Katoliki la Witbank, Afrika ya Kusini. Askofu mstaafu Lèonard Dhejju wa Jimbo katoliki Bunia, DRC. Askofu mkuu Léon Kalenga Badikebele, Balozi wa Vatican nchini Argentina. Wengine ni Askofu mstaafu Joseph Bolangi Egwaya Ediba Tasana wa Jimbo Katoliki la Budjala, DRC. Askofu Adel Zaki, OFM wa Jimbo la Alexandria, Misri. Askofu mstaafu Paolo Mandlate, S.S.S., wa Jimbo Katoliki Tete, Msumbiji. Orodha hii hadi tarehe 3 Novemba 2019 inahitimishwa na Askofu mstaafu Athanase Bala, C.S.Sp., wa Jimbo Katoliki la Bafia nchini Cameroon. Mama Kanisa anapenda kuwasindikiza viongozi wake waliotangulia kwenye usingizi wa amani wakiwa na imani na matumaini katika ufufuko, uzima na maisha ya milele, ili sasa waweze kupumzika kwenye usingizi wa amani baada ya kuwafundisha, kuwaongoza na kuwatakatifuza watu wa Mungu, Barani Afrika.

Papa: Makardinali na Maaskofu

 

04 November 2019, 14:19