Tafuta

Vatican News
Tukio la tamasha liitwalo Usiku wa nyota kwa ajili ya Bambino Gesù,likiwa ni mshikamano wa ufadhili kwa ajili ya watoto wadogo wa Hospitali ya Kipapa Tukio la tamasha liitwalo Usiku wa nyota kwa ajili ya Bambino Gesù,likiwa ni mshikamano wa ufadhili kwa ajili ya watoto wadogo wa Hospitali ya Kipapa   (ANSA)

Mshikamano wa Usiku wa Nyota kwa ajili ya Bambino Gesu’!

Tukio linalotaka kuhamasisha wafadhili ili kuweza kusaidia Hospitali ya watoto ya Kipapa ya Bambino Gesù na katika mwaka 2019 inaadhimisha miaka 150 tangu kuanza kutenda huduma yake kunako mwaka 1859 imefanyika usiku wa tarehe 21 Novemba katika Ukumbu wa Paulo VI na Baba Mtakatifu hakukosa kuwatumia ujumbe kwa njia ya video.

Na Sr. Angela rwezaula – Vatican

Tarehe 20 Novemba 2019 mjini Vatican katika Ukumbi wa Paulo VI usiku saa 2.30 majira ya Ulaya limefanyika tukio la mshikamano, uliopewa jina “usiku wa Nyota kwa ajili ya Mtoto Yesu”. Hili ni tukio linalotaka  kuhamasisha wafadhili ili kuweza kusaidia Hospitali ya watoto ya  Kipapa ya Bambino Gesù ambayo katika mwaka huu 2019 inaadhimisha miaka 150 tangu kuanza kutenda huduma yake kunako mwaka 1859. Katika tukio hili, Baba Mtakatifu Francisko hakukosa kuwatumia ujumbe kwa njia ya video.

“Nimekuwa na fursa nyingi ya kukuta na watoto na vijana wadogo katika Hospitali ya Bambino Gesu’. Na nimekuwa na hisia ya haraka katika jitihada na upendo wa madaktari, wauguzi, watafiti na wale wote ambao wako karibu na  wadogo walio wagonjwa, amesema Baba Mtakatifu Francisko. "Nimekuwa nikiona huruma katika mitazamo na joto la mkumbatio katika maeneo ambayo kwa hakika nia ya uchungu na mateso japokuwa  kuna hata ujasiri na matumaini makubwa."

Baba Mtakatifu Francisko amesema: Hospitali ya Bambino Gesù ilianza miaka 150 kama zawadi ya upendo, na ukusanyaji wa  sadaka ndogo ndogo kwenya makopo kwaajili ya kutibu watoto wadogo katika mji wa Roma. Kwa kipindi kirefu cha karne na nusu ya historia, madawa yameweza kufanya maendeleo makubwa na hospitali imetambua kuwekeza juu ya utafiti na kuweka sayansi katika huduma ya upendo. Bambino Gesu imekua sana katika uwezo wake wa kitaaluma na utambuzi na kugeuka kuwa moja ya kituo kikubwa muhimu cha watoto barani Ulaya na duniani.

Kimefanya hatua kubwa na kuvuka mipaka yake kwa kujikita katika matendo yake na kuwapokea watoto wadogo wagonjwa ambao hawawezi kutibiwa katika nchi zao wanazoishi na kusaidia zile nchi ili ziweze kukua katika sayansi ya madawa, huku wakito huduma ya dhati ya upendo na  utambuzi ambao ni muhimu sana aliokuwa anapenda Mtakatifu Papa Paulo VI. Baba Mtakatifu Fracisko aidha kwa kuhitimisha amesema  mateso ya watoto yanabaki kama ugumu wa kupokea na kukubali. Lakini kwa yule anayewatunza watoto wadogo kwa hakika yuko upande wa Mungu ambaye anashinda utamaduni wa ubaguzi. Kwa namna hiyo Hospitali ya Gesu' Bambino katika matendo yake ya kutibu kila siku imekuwa ishara ya upendo wa Kanisa zima ambalo linajikita katika huduma ya wadhaifu na walioathirika zaidi.

PAPA-BAMBINO GES'
22 November 2019, 16:49