Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko akiwa njiani kurejea kutoka katika hija yake ya 32 Kimataifa, amewashukuru watu wa Mungu nchini Japana pamoja na kutuma salam, matashi mema na baraka kwa wakuu wa Serikali. Baba Mtakatifu Francisko akiwa njiani kurejea kutoka katika hija yake ya 32 Kimataifa, amewashukuru watu wa Mungu nchini Japana pamoja na kutuma salam, matashi mema na baraka kwa wakuu wa Serikali. 

Hija ya Papa Francisko nchini Japan: Salam, baraka na matashi mema kwa viongozi wa serikali

Baba Mtakatifu amewatumia salam na matashi mema wakuu wa nchi ya Japan, Urussi, Finland, Estonia, Latvia, Lithuania, Poland, Jamhuri ya watu wa Czech, Slovenia, Croatia pamoja na Italia. Kwa namna ya pekee kabisa, Papa amemshukuru Mfalme Naruhito wa Japan na watu wote wa Mungu nchini humo, kwa mapokezi ya makubwa na ukarimu waliomwonjesha wakati wa hija yake Japan.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko kuanzia tarehe 19-26 Novemba 2019 amefanya hija ya 32 ya kitume Barani Asia kwa kutembelea: Thailand na Japan kama sehemu ya mchakato wa Kanisa wa kutaka kudumisha majadiliano ya kidini na kitamaduni ili kulinda: utu, heshima, haki msingi za binadamu, ustawi, maendeleo, mafao ya wengi, haki na amani duniani na kwa namna ya pekee Barani Asia. Akiwa njiani kurejea mjini Vaticam, Baba Mtakatifu Francisko, Jumanne tarehe 26 Novemba 2019 amewatumia salam na matashi mema wakuu wa nchi mbali mbali wakati alipokuwa anapita kwenye anga la nchi zao. Baba Mtakatifu amewatumia salam na matashi mema wakuu wa nchi ya Japan, Urussi, Finland, Estonia, Latvia, Lithuania, Poland, Jamhuri ya watu wa Czech, Slovenia, Croatia pamoja na Italia.

Kwa namna ya pekee kabisa, Baba Mtakatifu amemshukuru Mfalme Naruhito wa Japan na watu wote wa Mungu nchini humo, kwa mapokezi ya makubwa na ukarimu waliomwonjesha wakati wa hija yake ya kitume nchini humo. Baba Mtakatifu Francisko amewahakikishia sala na sadaka yake na hatimaye, akawapatia baraka zake za kitume. Viongozi wengine amewaombea: baraka, amani, furaha, ustawi na maendeleo kwa ajili ya watu wao. Alipowasili kwenye anga la Italia, Baba Mtakatifu amemtumia salam na matashi mema Rais Sergio Mattarella wa Italia, akimwambia kwamba, anarejea kutoka Thailand na Japan, ambako amepata fursa ya kuweza kuwaimarisha ndugu zake katika imani, ili waendelee kujizatiti katika ujenzi wa jamii inayosimikwa katika ukarimu na amani. Anamshukuru Rais Sergio Mattarella pamoja na watu wa Mungu nchini Italia na anawatakia maendeleo ya kiroho, kiutu na kijamii.

Papa: Salam

 

26 November 2019, 16:22