Tafuta

Vatican News
Papa Francisko katika hija yake nchini Thailand ameombea miito mitakatifu, ili vijana wa kizazi kipya waweze kujisadaka kwa ajili ya huduma kwa watu wa Mungu nchini Thailand. Papa Francisko katika hija yake nchini Thailand ameombea miito mitakatifu, ili vijana wa kizazi kipya waweze kujisadaka kwa ajili ya huduma kwa watu wa Mungu nchini Thailand. 

Hija ya Papa Francisko nchini Thailand: Sala ya Kuombea Miito

Baba Mtakatifu anasema Mwenyezi Mungu ndiye Bwana wa mavuno, apende kuwabariki vijana wa Thailand kwa zawadi ya ujasiri ili waweze kujibu wito wa Mungu katika maisha yao. Awasaidie kufungua nyoyo zao ili kupokea mambo makubwa katika maisha. Awajalie mitume wake wote upendo wa dhati na sadaka kwa ajili ya kukoleza mbegu ya miito katika maisha ya waamini. MIITO!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko baada ya kukutana na kuzungumza na wakleri, watawa, waseminari na makatekista kwenye Parokia ya St. Peter, Jimbo kuu la Bangkok nchini Thailand, Ijumaa tarehe 22 Novemba 2019 kwa kukazia umuhimu wa kushukuru; kudumu katika uaminifu kwa Roho Mtakatifu; ushuhuda maisha na utume wao kwa Kristo Yesu na Kanisa lake kwa njia ya huduma kwa maskini na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii, ameungana nao kusali kwa ajili ya kuombea miito mitakatifu nchini Thailand. Baba Mtakatifu anasema Mwenyezi Mungu ndiye Bwana wa mavuno, apende kuwabariki vijana wa Thailand kwa zawadi ya ujasiri ili waweze kujibu wito wa Mungu katika maisha yao.

Mwenyezi Mungu awasaidie kufungua nyoyo zao ili kupokea mambo makubwa katika maisha. Awajalie mitume wake wote upendo wa dhati na sadaka kwa ajili ya kukoleza mbegu ya miito katika maisha ya waamini. Baba Mtakatifu anaombea ili Mwenyezi Mungu aweze kuwajalia neema na ujasiri watawa wanaojisadaka kwa ajili ya huduma parokiani pamoja na familia ili kuwahamasisha watu wa Mungu kuitikia maisha ya kuwekwa wakfu. Awaunganishe na Kristo Yesu kwa njia ya sala na Sakramenti, ili waweze kushirikiana na Mwenyezi Mungu katika katika ujenzi wa Ufalme wenye huruma, ukweli, haki na amani. Amina.

Papa: Sala ya Miito
22 November 2019, 15:21