Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 27 Novemba 2019 amekutana na kuzungumza na wajumbe wa Mfuko wa Azerbaigiani wa Nizani Ganjavi Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 27 Novemba 2019 amekutana na kuzungumza na wajumbe wa Mfuko wa Azerbaigiani wa Nizani Ganjavi  (ANSA)

Papa Francisko akutana na wajumbe wa Mfuko wa Nizami Ganjavi!

Baba Mtakatifu Francisko amewapongeza kwa kujizatiti kujadili changamoto mamboleo ili kujenga na kudumisha amani kwa njia ya majadiliano, kwa kuheshimiana pamoja na kuendelea kuchota utajiri kutoka kwa washairi maarufu kutoka Ghuba ya Uajemi waliowika kwenye karne ya kumi na mbili, ambao ndio asili ya jina la mfuko huu. Tunu msingi za maisha zimwilishwe katika huduma.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 27 Novemba 2019 amekutana na kuzungumza na washiriki wa mkutano wa “Mfuko wa Azerbaijan wa Nizami Ganjavi” wanaofanya mkutano wao mjini Roma. Baba Mtakatifu amewapongeza kwa kujizatiti kikamilifu katika kujadili changamoto mamboleo ili kujenga na kudumisha amani kwa njia ya majadiliano, kwa kuheshimiana pamoja na kuendelea kuchota utajiri kutoka kwa washairi maarufu kutoka Ghuba ya Uajemi waliowika kwenye karne ya kumi na mbili, ambao ndio asili ya jina la mfuko huu.

Wajumbe hawa wanatekeleza dhamana na utume wao kwa kuzingatia umuhimu wa huduma inayotolewa kwa Jumuiya ya Kimataifa kwa kuzingatia tunu msingi za uwajibikaji wao katika mataifa mbali mbali wanamotoka. Baba Mtakatifu amewahakikishia sala na sadaka yake, akitumaini kwamba, mchango wa mawazo yao utasaidia kukabiliana na changamoto za athari za mabadiliko ya tabianchi sehemu mbali mbali za dunia. Baba Mtakatifu ametumia fursa hii kuwatia shime kuendeleza utamaduni wa majadiliano na ushirikiano, ili kuweza kuelewana na hatimaye, kukuza na kudumisha udugu wa kibinadamu kati ya watu wa Mataifa.

Papa: Majadiliano ya Kidini

 

27 November 2019, 16:54