Tafuta

Mantiki ya maisha ya dunia hii siyo fursa ya pekee kwa maana inahitaji subira na kuwa na upeo mwingine zaidi hapo! Mantiki ya maisha ya dunia hii siyo fursa ya pekee kwa maana inahitaji subira na kuwa na upeo mwingine zaidi hapo! 

Baba Mtakatifu Francisko:mahali penye ubinafsi hakuna uhai!

Wakati wa kutafakari Injili ya siku katika Liturujia ya Jumapili,Baba Mtakatifu kabla ya sala ya Malaika wa Bwana amezungumza juu ya ufufuko.Mantiki ya kidunia siyo njia pekee,badala yake ni lazima kutazamia ufufuko wa wafu na uzima ujao.Ametoa pendekezo la kuwa na subira zaidi.Mungu anapenda maisha na uhai mahali penye uhusiano wa kweli na vifungo vya uaminifu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko akitafakari sehemu ya Injili ya Siku katika Liturujia ya Dominika ya 32 ya kipindi cha Mwaka kwa waamini walio kusanyika katika kiwanja cha Mtakatifu Petro Vatican, tarehe 10 Novemba 2019  kabla ya kusali sala ya Malaika wa Bwana amezungumzia juu ya ufufuko. Mantiki ya maisha ya dunia hii siyo fursa pekee, maana inahitaji subira na kuwa na upeo mwingine zaidi hapo. Mungu anapenda maisha na uhai mahali penye uhusiano wa kweli na vifungu vya uaminifu.

Waliofufuka watakuwa sawaswa na malaika

Ni imani katika  ufufuko wa wafu na maisha ya milele ambavyo ni kiini cha maneno ya Baba Mtakatifu Francisko. Na hii ni kwa sababu katika Injili ya siku imewakilisha Yesu akizungumza na baadhi ya masadukayo kuhusiana na ufufuko ambao wao walikuwa awaamini.  Kwa maana hiyo walipendekeza kesi moja ngumu. Je katika ufufuo atakuwa mke wa yupi? Maana aliolewa na wote saba. Yesu akawaambia, Wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa; lakini, wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na kule kufufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi, wala hawawezi kufa tena; kwa sababu huwa sawasawa na malaika. Baba Mtakatifu Francisko amesema katika jibu hili, Yesu awali ya yote anawaalika watesi  wake na hata sisi kufikiria kwamba mantiki  ya kidunia ambayo tunaishi sasa, siyo mantiki pekee, na badala yake kuna nyingine zaidi. Na hiyo ina maana kwamba  siyo kitu tena chini ya kifo ambacho kitaonyeshwa wazi kuwa sisi ni watoto wa Mungu.

Maisha yetu  yatakuwaje ?

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea kufafanua matazamio ya mwisho amethibitisha kwamba, kutokana na  faraja kubwa na matumaini ya kusikiliza maneno hayo  rahisi na wazi ya Yesu juu ya maisha baada ya kifo ni muhimu na kwa maana  tunahitaji sana hasa katika wakati wetu wenye utajiri wa fahamu za ulimwengu, japokuwa yenye umasikini wa hekima juu ya maisha ya milele. Hata hivyo uhakika wa Yesu juu ya ufufuko wa wafu juu ya uaminifu wa Mungu ambaye ni Mungu wa maisha na kwa hakika nyuma ya swali la Wasadukayo walikuwa wanaficha swali jingine la kina kuhusu huyo mwanamke atakuwa wa nani? Hatakuwa na kitu baada ya ufufuko?

Maisha yapo mahali penye uhusiano wa kweli.

Yesu anajibu  kuwa, maisha ya Mungu anatupenda na kusumbuka sana na sisi, hata  kuwa na mfungamano kwa njia ya jina lake na sisi. Ni Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka,na Mungu wa Yakobo. Naye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai; kwa kuwa wote huishi kwake na  kwa maana wote wanaishi kwa njia yake. Kinyume chake, hakuna maisha mahali penye madai ya kuishi binafsi na kuishi kama visiwa. Na kama ni mitazamo hii kifo kinatawala. Ni ubinafsi! Kwa maana ya mimi ninaishi mwenyewe na kupanda kifo ndani ya moyoni wangu , amesitiza. Kwa kuhitimisha, Baba Mtakatifu anamwomba Bikira Maria ili atusaidie kuishi kwa kutazamia ufufuko wa wafu na uzima ujao. Ametoa pendekezo la kuwa na subira zaidi.

11 November 2019, 10:33