Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu ameathimisha Ibada ya Misa kwa ajili ya Mrehemu wote katika Makatakombe ya Priscilla Roma Baba Mtakatifu ameathimisha Ibada ya Misa kwa ajili ya Mrehemu wote katika Makatakombe ya Priscilla Roma   (Vatican Media)

Baba Mtakatifu:hata leo hii yapo makatakombe mengi duniani!

Tarehe 2 Novemba ni siku ya kukumbuka Marehemu wote ambao wamepitia katika dunia hii.Katika fursa hiyo Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi jioni,meadhimisha MisaTakatifu kwa ajili ya kuwakumbuka Marehemu wote kwenye Makatakombe ya Priscilla Roma.Katika mahubiri anakumbusha kuwa hata leo hii yapo bado makatakombe mengi duniani!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Siku ya kumbu kumbu ya  waamini marehemu wote ambao wamepitia katika maisha haya ya dunia, yaadhimishwa kila tarehe 2 Novemba yak ila Mwaka. Katika fursa hiyo Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi jioni, meadhimisha Misa Takatifu kwa ajili ya kuwakumbuka Marehemu wote kwenye Makatakombe ya Priscilla. Katika mahubiri yake bila kuandika, Baba Mtakatifu Fracisko amesema  maadhimisho ya kumbu kumbu ya marehemu wote katika Katakomba hiyo, kwake yeye ni kwa mara ya kwanza ameingia na ni mshangao kwake; na makaakombe hayo yanajifafanua mambo mengi. Ni kufikiria maisha ya watu wale ambao walikuwa wanajificha na ambao walikuwa na utamaduni huo wa kuzika watu wao na kuadhimisha Ekaristi ndani humo. Ilikuwa ni kipindi kibaya cha kihistoria , lakini ambacho hakijaisha. Hata leo hii bado ni zaidi. Makatakombe  ni mengi katika Nchi mahali ambamo wanaingia utafikiri  wanafanya sikukuu au ya kuzaliwa ili waweze kuadhimisha Ekaristi  kwa sababu katika maeneo hayo hawaruhusiwi ibada. Hata leo hii wakristo wanateseka zaidi kuliko karne za kwanza. Kufuatana na makatakombe, kuteswa, wakristo na masomo yaliyosomwa, yamemfaya Baba Mtakatifu Francisko kufikiria maneno matatu ya kutafakari ambayo ni: kitambulisho, mahali  na matumaini.

Akianza kufafanua maana ya 'kitambulisho' amesema

 Watu hao walikuwa wanakusanyika hapo kuadhimisha Ekaristi na kwa ajili ya kusifu Bwana ndiyo sawa sawa na ndugu zetu wengi leo hii katika Nchi ambamo tendo la kuwa Mkristo ni kama uhalifu na wanazuiwa, kwa maana hawana haki. Utambulisho ambao umesikika katika Injili ndiyo “Heri”. Utambulisho wa kikristo ndiyo huo wa heri. Baba Mtakatifu Francisko amethibitisha kuwa hakuna mwingine. Iwapo unafanya hivyo na kuishi namna hiyo wewe ni Mkristo. Akitoa mfano amesema hakuna sababu ya kujitetea kama wewe ni mmoja wa chama kimoja au kingine…. Ndiyo ni mambo mazuri, lakini yote hayo ni dhana mbele ya ukweli huo. Kadi yako ya kitambulisho ni hiyo, na ikiwa hauna hiyo, harakati au mambo mengine hayahitajiki.  Ama unaishi kama hivyo, au wewe siyo Mkristo, n ahata hivyo  kiurahisi Bwana alisema!

Baba Mtakatifu aidha ametoa mfano kwamba mwingine anaweza kujitetea: “Ndiyo, lakini siyo rahisi, sijui kuishi kama hivi…”, lakini kuna sehemu nyingine ya Injili ambayo inatusaidia kuelewa vyema jambo hili hata kifungu hicho cha Injili kitakuwa Protokali kuu na ambayo tutahukumiwa. Kifungu hicho ni kutoka Mathayo 25. Pamoja na vifungu hivi viwili vya Injili, Heri za mlimani na Protokali  kuu, sisi  tutaona, huko tukishi hivyo, kitambulisho chetu kama Wakristo. Bila hiyo, hakuna kitambulisho. Kuna udanganyifu wa kuwa Mkristo, lakini siyo utambulisho.

Neno la pili ni 'mahali'

Baba Mtakatifu Francisko akifafanua maana ya neno mahali anasema wakristo wa kwanza walikuwa wanakwenda  mahaliili kujificha na kuwa na usalama hata kuwazika wafu; watu hao ambao walikuwa wanaadhimisha Ekaristi, na hivyo  hata leo hii wapo watu  wanaojificha katika nchi mahali ambamo wanakatazwa. Amemfikiria Sr. Mmoja wa Albania ambaye alikuwa katika kambi ya mateso ya wakomunisti na ilikuwa ni  marufuku kwa makuhani kutoa sakramenti, lakini huyu mtawa, hapo, akabatiza kwa siri. Na watu, wakristo walijua kuwa mtawa huyo alibatiza na mama wengi walimwendea na watoto wao; lakini yeye  hakuwa na glasi, yaani kitu cha kuwekea maji ...Yeye alitumia viatu kutafuta maji kutoka katika mto  na akabatiza kwa kutumia viatu.  Kwa maana hiyo sehemu ya Mkristo ni  mahali popote, amethibitisha Baba Mtakatifu Francisko na kuongeza  kusema kuwa: kwa maana hatuna nafasi mwafaka maishani.

Wengine wanataka kuwa nayo na ni wakristo waliohitimu. Lakini hawa wanakimbilia  hatari ya kubaki na elimu yao na  kuangusha ukristo. Je nafasi ya mkristo ni ipi? Kwa kujibu swali hili amesema:  “Roho za wenye haki ziko mikononi mwa Mungu”. Nafasi ya Mkristo iko mikononi mwa Mungu mahali ambamo anataka Yeye. Mikono ya Mungu ambayo imejaa majeraha na ambayo ni mikono ya mwanae aliyetaka kubeba majeraha kwa ajili ya kufanya tuone Baba na kutuombea sisi. Nafasi ya Mkristo iko katika maombi ya Yesu mbele ya Baba. Ni katika mikono ya Mungu ambapo ni mahali pa usalama. Potelea mbali  na kitakachotoke kitokee, hata Msalaba. Pia, kitambulisho chetu kinasema kwamba tutashukuru ikiwa watatutesa na  wanatusingizia ; lakini ikiwa tuko mikononi mwa Mungu, yenye madonda ya upendo na tuna uhakika. Hapa ndiyo mahali petu. Baba Mtakatifu Francisko amewataka waamini watafakari na kujiuliza: Je mini ninahisi kuwa na uhakika? katika mikono ya Mungu na dhamana zingine ambazo tunakodisha lakini baadaye zitaanguka na ambazo hazina msimamo? Wakristo hawa walio na kadi ya kitambulisho na ambao waliishi na kuishi mikononi mwa Mungu, ni wanaume na wanawake wa matumaini: na hii ndilo neno la tatu ambalo limemjia Baba Mtakatifu Francisko.

Neno la tatu ni 'matumaini'

 Katika somo la pili, kuna maono ya mwisho ya kila kitu kilichofanyika na kuumbwa,  na nyumbani kwetu tutakapokwenda! Na ili kuingia huko, hatuitaji vitu vya kushangaza, hatuitaji mitindo ya kisasa: tunahitaji kuonyesha kadi ya kitambulisho. Ukiwa nacho basi ni sawa, endelea mbele anasema Baba Mtakatifu. Matumaini yetu yako Mbingu, tumaini letu limesimamishwa huko na sisi, tunapaswa kuwa na kamba mikononi mwetu, tujisimamie  kwa kutazama ile ng’ambo ya forodha  ya mto ambayo tunaikatisha kupitia ili kufika. Kwa kuhitimisha amesema: Kinacho hitajika ni “Kitambulisho cha heri na Injili ya Mathayo 25;  Kuwa na mahali pa salama zaidi mikononi mwa Mungu, hata yenye majeraha ya upendo; kuwa na tumaini katika  siku sijazo; aidha ile  nanga, na kuangalia kule ng’ambo katika forodha nyingine, lakini kwa kushikilia vema kamba. Mambo hayo   ni muhimu. Daima ni kushikamana na kamba. Mara nyingi sana tutaona kamba tu, na siyo nanga hata forodha nyingine. Lakini wewe, shikilia kwa kamba na mbayo itakufikisha salama”

 

02 November 2019, 16:50