Tafuta

Vatican News
Mkutano Mkuu wa Mwana wa Baraza la Mabaraza ya Maaskofu Ulaya (CCEE) unafanyika huko Santiago ya Compostela Mkutano Mkuu wa Mwana wa Baraza la Mabaraza ya Maaskofu Ulaya (CCEE) unafanyika huko Santiago ya Compostela 

Ushauri wa Papa kwa maaskofu Ulaya:kuweni na bidii ya upendo:ni njia kuu dhidi ya migawanyo na mizozo!

Katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Barza la Mabaraza ya Maaskofu Ulaya ulioanza jioni tehe 3 Oktoba 2019 huko Santiago ya Compostela,Baba Mtakatifu Francisko amewatumia ujumbe wake akiwashauri wawe na bidii ya upendo ambao ni njia kuu dhidi ya migawanyiko na mizozo.Pia waimarishe njia za kujitolea kwa ajili ya ubinadamu mpya barani Ulaya.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Baba Mtakatifu Francisko ametuma ujumbe wake kwa Maaskofu walioanza  Mkutano wao Mkuu wa Baraza la Mabaraza ya Maaskofu Ulaya, barua aliyomwelekeza Kardinali Angelo Bagnasco, Rais wa Baraza la Mabaraza ya Maaskofu Ulaya (CCEE). Mkutano huo umeanza jioni tarehe 3 Oktoba 2019 huko Santiago ya Compostela,nchini Hispania  ukiongozwa na mada “Ulaya ni kipindi cha kuamka tena? Ishara ya Matumaini”. Hii ni mada ambayo kwa mujibu wa Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa washiriki hao kuwa ni muhimu na inawawajibisha kutafakari juu ya safari za michakato  mzima ambayo wanapaswa waifuate ili kuweza kuipatia kwa upya kile ambacho utafakiri Bara la kizamani limepoteza. Baba Mtakatifu Francisko anawaalika maaskofu kutafuta ishara hata zile ndogo za matumaini ambazo ni sawa na kusema maisha mapya na mbazo zipo nyingi na mara nyingi zimejificha, wakati mwingine kuna shughuli nyingi zinazo pelekea kutotambua ishara hizo. Ishara hizi zinaonekana ni kama  upweke wa ndugu ambao wanateseka na wenye kuwa na mahitaji, hasa wagonjwa, wafungwa, masikini, wahamiaji na wakimbizi; aidha ni kama vile hata jitihada katika nyanja za kiutamaduni kwa upande wa elimu kwa walio wadogo zaidi ambao ndiyo wakati endelevu wa Ulaya.

Upendo wa dhati ni njia mwalimu kwa ajili ya ukristo

Hata hivyo Baba Mtakatifu Francisko akizingatia njia ambazo zinawezekana, anashauri tena juu ya kuwa na upendo wa dhati na kwamba ndiyo njia mwalimu ya kikristo huku akibainisha zaidi dhidi ya tabia ya nyakati zetu zilizojaa na migawanyo na upinzani. Upendo una maana ya kutazama mwenzako kama mtu, kumkimbilia anapokuwa na shida, kama Yesu anavyofundisha: nilikuwa na njaa, mlinipatia chakula, nilikuwa na kiu mkaninywesha, nilikuwa mgeni mkanikaribisha, nilikuwa sina nguo mkanivalisha, mgonjwa mkaja kunitazama. Aidha Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe huo anasisitiza kwamba upendo wa dhati  unatufanya  kupumua, na haupingi watu, lakini huona mahitaji ya kila mmoja wetu na hasa wale wa mwisho wenye kuhitaji zaidi yetu kwa maana sisi sote ni watu maskini, wote wadhaifu  na wote tunayo mahitaji ya utunzwaji.

Kupyaisha jitihada za kuikarabati Ulaya

Baba Mtakatifu Francisko aidha ameomba wawe hata mashuhuda wa imani ambayo hajishabikii au kuitangaza binanafsi, badala yake iwe kivutio, iwe wazi kwa ajili ya kupokea yaliyo mapya kutoka kwake Roho na bila kurudia miundo ya kizamani. kadhalika akitazama eneo la Santiago, amesema ni  mahali pa ishara sana kwa ajili ya kugunduwa kwa upya utajiri mkubwa wa umoja wa Ulaya katika utamaduni wake wa kidini na kitamaduni, Baba Mtakatifu Francisko ameshauri kutazama sura tatu za watakatifu ambao Mtakatifu Yohane Paulo II kunako mwaka 1999 aliwatangaza kuwa watakatifu wasimamizi wa Ulaya: nao ni Brigitta wa Sweden, Mtakatifu Caterina wa Siena na Mtakatifu Teresa Benedetta wa Msalaba (Edith Stein) ambao anasema, wanaonesha upendo wa kuishi katika familia, ulio msingi kwa kila jamii ya binadamu na kama jinsi ilivyo huduma ya upendo na sadaka kuu. Ni kwa njia hiyo ya  kuinamia majeraha ya wale waliopotea tu, wasio kuwa na mlinzi na waliotupwa pembezoni  kama walivyo fanya wao, ndipo Kanisa linaweza kupyaisha jitihada zake kwa ajili ya ukarabati wa Ulaya.

Ubinadamu mpya

Kufanya jitihada kwa ajili ya ubinadamu mpya wenye uwezo wa kujadiliana, kufungamanisha na kuthamanisha kile ambacho ni kizuri zaidi cha utamaduni wa Bara ndiyo ushauri wa mwisho wa Baba Mtakatifu Francisko na  ambaye pia ameelekeza kama  injini tatu za kufuata kwenye  safari ya kuifanya Ulaya iweze kuwa  familia ya watu na ardhi yenye amani na matumaini. Injini hizi ni Ulinzi wa maisha na hadhi ya kibinadamu, pili uhamasishaji wa familia na mwisho ni  heshima ya haki msingi wa binadamu.

04 October 2019, 10:44