Tafuta

Katika fursa ya  Siku ya Ugonjwa wa Kumbu kumbu duniani, bado inakumbukwa ziara ya Baba Mtakatifu katika Kituo cha wagonjwa hao huko Bufalotta Roma kunako Apri 12 Mwaka huu Katika fursa ya Siku ya Ugonjwa wa Kumbu kumbu duniani, bado inakumbukwa ziara ya Baba Mtakatifu katika Kituo cha wagonjwa hao huko Bufalotta Roma kunako Apri 12 Mwaka huu 

Papa:Wito kuhusu Siku ya Ugonjwa wa Kumbu kumbu duniani!

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya tafakari ya Katekesi,tarehe 18 Septemba 2019 ameomba watu wote kusali kwa kwa ajili ya uongofu wa mioyo kwa wagonjwa wote walio poteza kumbu kumbu(Alzheimer),kwa ajili ya familia zao na wale wanao watunza kwa upendo.Aidha maombi yake ni kwa ajili ya wote wanaoteseka na saratani za aina nyingi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Wagonjwa mara nyingi ni waathirika wa utamaduni wa kibaguzi unaopelekea hata Baba Mtakatifu Franciko anakumbuka kwamba wagonjwa pamoja na maendeleo yake mara nyingi wanakumbwa na hali ya ubaguzi ambapo amesisitizia juu ya kusali kwa ajili yao kwa ajili ya upatikanaji wa tiba ya kuzuia ugonjwa ya aina ya saratani. Amesema hayo mara baada ya tafakari ya Katekesi, huku akiomba kusali kwa  kwa ajili ya uongofu wa mioyo kwa wale wote  wagonjwa waliopoteza kumbu kumbu(Alzheimer), kwa ajili ya familia zao na wale wanao watunza kwa upendo.

Ni katika kuelekea kilele  siku ya   Kimataifa ya wagonjwa wa kupoteza kumbukumbu au Alzheimer  inayoadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 21 Septemba. Hata hivyo Baba Mtakatifu Francisko amekumbuka kwa namba ya pekee siku maalum ya tarehe 12 Aprili katika ziara yake ya kitume kwa mantiki ya Ijumaa ya huruma ambapo alitembelea Kijiji cha Emanuale. Katika fursa hiyo Baba Mtakatifu Francisko alikutana na wageni wanaotunzwa katika majengo yaliyopo kwenye mtaa wa Bufalotta Roma, ambapo wanaoishi humo ni watu walioshambuliwa na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimers).

Kampeni ya kimataifa kwa ajili ya kuongeza elimu: Mashirika yanayojihusisha na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu na wadau wote duniani kote, mara kwa mara wanaandaa kampeni za makongamano, utoaji wa taarifa, vile vile matembezi ya kuaadhimisha ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu, kwa kuhusisha vyombo vya habari, kuanda siku za harambe za kuchangisha hela, manufa ya kampeni hizi inazidi kukua lakini, ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu pamoja na taarifa potofu zinazohusu ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu baado ni tatizo hapa duniani kote. Hii ni kutokana na Ugonjwa wa kupoteza kumbu kumbu au Alzheimer kuongezeka kwa kiwango cha kutisha duniani kote.  Watu wengi wenye Alzheimer wana umri wa miaka 65 au zaidi. Inasadikika kuwa mwaka wa 2030, idadi ya watu wenye Alzheimer inaweza kufikia milioni 8; na kama wanasayansi hawawezi kupata njia ya kutibu au kuzuia Alzheimers, idadi hii inaweza kuanzia kati ya milioni 11 na milioni 16 kwa mwaka wa 2050.

 

18 September 2019, 13:30