Tafuta

Vatican News
Katika mchezo ni bora kuepuka njia za mslahi binafsi na ushindani wa kukithiri Katika mchezo ni bora kuepuka njia za mslahi binafsi na ushindani wa kukithiri  (ANSA)

Papa Francisko:mazoezi ya mchezo yanasaidia kukuza thamani za maisha!

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 28 Septemba amekutana na kuzungumza na Shirikisho la Gymnastics nchini Italia ambapo amewashauri wagundue ukuu wa mchezo unaoongoza mazoezi ya michezo kueleweka kama ujasiri,uzuri na kujituma kwa matumaini.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Vyama vya michezo vinaalikwa hata kukuza hisia ambazo kwa njia ya michezo zinahamasisha maendeleo fungamani ya watu na upendo kijamii. Ni maneno ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 28 Septemba 2019 alipokutana na wajumbe wa Shirikisho la Gymnastics nchini Italia ambapo amewaelekeza thamani ambazo zinapaswa ziwe msingi wa kila shughuli ya mchezo. Hizi ni ni kuhusu uelewa na mchezo wa kuishi na sio tu kama chanzo cha ustawi wa mwili, bali kama mawazo ya maisha ya ujasiri, uchanya na uzuri. Kwa maana hiyo michezo unakuwa ni uzoefu wa kielimu ambao husaidia vizazi vipya kukuza thamani ya maisha ambayo ni upendo wa hali halisi na haki, uzuri na wema na wakati huo utafutaji wa uhuru na wa mshikamano.

Ukosoaji na  ushindani uliozidi

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na hotuba yake kwa wanamichezo hao pia ametoa onyo juu ya mfumo wa sasa wa michezo na hali halisi inayojikita katika mantiki ya kutaka faida  na roho ya ushindani iliyozidi na ambayo anasema, kwa bahati mbaya kuna tabia za kutumia hata nguvu na vurugu. Ni mambo matatu mabaya ya kutafuta faida, ya kufanya ushindani uliozidi kiasi na wakati mwingine tabia za kutumia nguvu. Na tabia zote hizi tatu mbaya Baba Mtakatifu anasisistiza kuwa zinakosa kitu kimoja hasa cha kuwa na ukuu wa upendo katika mchezo. Ndani ya mchezo ikikosekana ukuu wa upendo, tabia kama hizo zinaonekana na kuchusha thamani ya mchezo.

Kushuhudia Injili katika mchezo

Mbele ya mantiki zinazo elezeka kama hasi, Baba Mtakatifu Francisko anashauri wakuu na wanamichezo kuongozwa na imani kikristo katika kushuhudia nguvu ya kibinadamu kwa kutumia  Injili, hata katika mazingira ya michezo kwa namna ya kuchangia kujenga jamii ya kindugu. Amehitimisha akiwatakia Jumuiya ya Gymnastics iwezeshe mchezo kila wakati kwa uaminifu na roho nzuri ya ushindani, kuwa tayari na  roho ambayo inapaswa kukabiliana na mashindano ya maisha kwa ujasiri na ukarimu, furaha na imani kwa siku zijazo.

28 September 2019, 14:25