Tafuta

Maadhimisho ya Misa takatifu Jimboni Albano Roma tarehe 22 Septemba 2019 Maadhimisho ya Misa takatifu Jimboni Albano Roma tarehe 22 Septemba 2019 

Baba Mtakatifu Francisko:Imani isiwe ya malimwengu na Kanisa ni nyumba ya huruma ya Mungu!

Usitazame mtu kamwe kama hakimu,bali kama ndugu kwa maana sisi siyo wakaguzi wa maisha ya wengine bali ni wahamasishaji wa wema wa wote.Ndiyo sauti nguvu muhimu katika mahubiri ya Baba Mtakatifu Francisko aliyotoa huko Albano,Roma tarehe 21 Septemba 2019 jioni ambapo ametoa ushauri kwa waamini wawe imani thabiti na zaidi wawe jumuiya iliyofunguliwa wazi na Kanisa ni mahali pa kukutana na upendo wa Mungu.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Usitazame kamwe mtu kama hakimu bali kama ndugu, maana sisi siyo wakaguzi wa maisha ya wengine bali wahamasishaji wa wema wa wote. Maneno ya Baba Mtakatifu Francisko yamesikika katika mahubiri yake jioni ya tarehe 21 Septemba 2019 akiwa katika ziara yake kichungaji kwenye Jimbo la Albano Roma. Katika mahubiri anawashauri wawe na imani thabiti, kuepuka mateto na kutokuwa na jumuiya iliyofungwa badala yake wakumbuke kwamba Kanisa ni mahali pa kukutana na upendo wa Mungu.Baba Mtakatifu amesema, Kanisa lipo kwa ajili ya kutangazia waamini hata wale walio mbali au waliosahau kwamba  Mungu anatupenda akiwa wa kwanza. Maneno yote ya mahuburi ya Baba Mtakatifu yenye utajiri na kuongeza hata mengine bila kusoma kwenye karatasi  yamejikita juu ya utume wa Kanisa na wakristo katika dunia hii, hasa kwa kutazama maisha ya Zakayo kutoka Injili ya siku iliyosomwa, kwani Kanisa mama lilikuwa pia linakumbuka sikukuu ya Mtakatitfu Matayo.

Hata hivyo kabla ya maadhimisho ya misa  Takatifu hiyo katika uwanja wa Pia, Baba Mtakatifu Francisko amekuwa ndani ya  Kanisa Kuu la Mtakatifu Pankrasi na kusali na mapadre wa jimbo la Albano. Miaka 12 iliyopita, katika tarehe kama hiyo Baba Mtakatifu msataafu Benedikto XVI alitabaruku Kanisa Kuu hilo. Baba Mtakatifu Francisko katika mahubiri yake kuhusu Injili ya Siku anakumbuka Zakayo japokuwa na kuwa na kimo kidogo aliweza kukwea mti ili amtazame Yesu ambaye alikuwa anapitia njia ya Yeriko. Mbele ya macho ya wazalendo, Zakayo hakuwa anaonekana au kupendwa kwa sababu alikuwa ni mtoza ushuru wakati wa imaya ya kirumi. Licha ya hayo Yesu anainua mtazamo wake juu na kumwalika ashuke kwa haraka kwa sababu Yeye anataka kuingia na kukaa nyumbani mwake. Pamoja na vizingiti, vikwazo vya dhambi, na tetesi, Mungu anamkumbuka mdhambi mkuu, Baba Mtakatifu amebainisha. Aidha ameuliza swali pia kulijibu  kwamba ni kitu gani kinaelezwa katika Injili hiyo kwenye maadhimisho ya Kanisa lao Kuu? Ni kwamba kila Kanisa, kwa elfu kubwa mno ni hai katika moyo wa waaamini kutokana na kuwa na kumbu kumbu ya kuwa Mungu anawapenda!

Kanisa lipo kwa maana ya kuthibitisha kwamba kila mtu hata aliye mbali anapendwa kwa jina la Yesu; na hii ina maana kuwa “Mungu hakusahau, wewe upo moyoni mwake”! Amesisitiza Baba Mtakatifu na huku akitumia maneno ya Yesu anawatia moyo waamini wote  wasiwe na hofu ya kuendeleza maisha ya mji wao, hasa kwenda kwa yule aliyesahaulika, kwa yule aliyejificha nyuma ya matawi ya aibu, ya hofu, ya upweke na kwenda kumwambia kwamba “Mungu anakukumbuka”. Na hii ni kutokana na kuwa Mungu anabadili maisha, hivyo hakuna kutupia maisha yako bure. Ni muhimu kuzingatia kuwa, wakati Zakayo alikuwa anatafuta kujua ni aina ipi ya ualimu wa Yesu, ni Bwana mwenyewe anatangulia, Yesu alimtazama akiwa wa kwanza na kuzungumza naye. Maisha mara nyingi yanabadilika tu, unapogundua ukuu wa Mungu, na upendo wake ambao unatufikia ukiwa wa kwanza kuliko yote. Iwapo wewe ni kama Zakayo unatafuta maana ya maisha, lakini bila kuyapata, ina maana upo unatafuta upendo mahali pasipo pake, kama vile utajiri, mafanikio na  ustawi binafsi na kumbe jiachie utazamwe na Yesu, maana ni Yesu peke yake tu utagundua daima umekuwa ukipendwa.

Aidha Baba Mtakatifu Francisko kwa maana hiyo anawaalika  wakristo wote kujiuliza, kama Kanisa iwapo wanatanguliza kwanza Yesu au majengo. Kila uongofu unazaliwa na huruma kwanza, unazaliwa kutokana na wema wa Mungu ambao unaoingia ndani ya moyo.  Iwapo kila chochote tufanyacho hakianzii na mtazamo wa huruma ya Yesu , kuna hatari ya imani kubobea katika malimwengu na kuikwanza au kuijaza mambo mengi kama vile zenye mada za kiutamaduni, maono madhubuti, chaguzi za kisiasa, uchaguzi wa chama ... Lakini huku kukasahau umuhimu zaidi hasa wa unyenyekevu wa kiimani, na kwamba  kinachotangulia  kwanza ni kukutana huruma hai ya Mungu. Na ikiwa hilo siyo kitovu,na  ikiwa hakiwekwi  mwanzoni, mwisho wa shughuli zetu zote, kuna hatari ya kumweka Mungu nje ya nyumbani, ambayo ni Kanisa na  ambalo ni nyumba yake, lakini siyo pamoja nasi. Baba Mtakatifu kwa maana hiyo anatoa mwaliko kwa wote ili kujiachia katika huruma ya Mungu iweze kuingia katika nyumba, maana yeye anaingia na huruma yake, amesisitiza Baba Mtakatifu Francisko. Yesu alipomwambia Zakayo kuwa anataka kukaa katika nyumba yake alimfanya ahisi upendo na kwa namna hiyo Zakayo anathibitisha kutoa kwa haraka mali yake kwa maskini na kama ameibia yeyote anaahidi kumrudishia mara nne zaidi, kwa maana ya kwenda zaidi ya Sheria ambayo ilikuwa inataka urudishe hadi kufikia moja ya tano, Baba Mtakatifu anasisitiza kuwa anafanya hivyo kwa sababu  Zakayo amekutana na upendo, anahisi kuwa nyumbani.

Ni kwa jinsi gani watu wa karibu yetu wangefurahi kusikia Kanisa linakuwa  kama nyumba yao. Inatokea kwa bahati mbaya, jumuiya zetu zinageuka kuwa tofauti  na hilo kwa wengi na  makanisa ya kuvutia ni machache.  Mara nyingi hata sisi tunakumbwa na kishawishi cha kutafuta vyama vilivyofungwa, au kuingia sehemu nyeti kati kati ya walioteuliwa. Tunahisi kuchaguliwa na kuhisi ukuu …. Na wakati huo huo wapo  ndugu wengi zaidi ambao wanahamu ya kupata nyumba na ambao hawana ujasiri wa kuikaribia, labda kwa sababu hawakuhisi kukaribishwa; na labda walikutana na padre ambaye hakuwapokea vuzuri au kuwafukuzia mbali, pengine walilazimika kulipia sakramenti fulani jambo ambalo ni baya sana na wakaenda mbali baba Mtakatifu amebainisha. Lakini Bwana anatamani Kanisa leo liwe nyumba kati ya nyumba ambayo inakarimu kila mtu, msafiri katika maisha na aweze kukutana naye, “Yeye  aliyekuja kuishi katikati yetu”(Yh 1,14). Baba Mtakatifu FRancisko aidha amesisitiza kuwa katika Kanisa  ambamo hawainui mtazamo kamwe kutoka juu kwenda chini, na badala yake kuinua mtazamo wao kutoka chini kuelekea juu kama Yesu alivyomtazama Zakayo, bado hawajatambua. Nafasi iliyo mwafaka tu ya kumtazama mtu kutoka juu kwenda chini ni ile ya kumsaidia kuamka, la sivyo hairusiwi! Ni kipindi hicho tu cha kutazama mtu kwa sababu ameanguka. Tusitazama watu kamwe kama hakimu, na badala yake tuwatazame kama ndugu. Sisi siyo wakaguzi wa maisha ya wengine, badala yeke ni wahamasishaji wa wema wa wote.

Na ili kuwa wahamasishaji wa wema wa wote jambo moja linalosaidia ni kufunga ulimi, bila kuteta wengine. Lakini hata hivyo Baba Mtakatifu amebainisha kwamba, kila mara anaposema mambo hayo, anasikia  wengine,“Baba tazama ni jambo baya sana, lakini ninapoona jambo fulani, ninahisi mara noja kuteta”. Kutokana na hili Baba Mtakatifu ametoa ushauri kwamba kuna dawa kuhusiana na hilo, mbali na sala: dawa hiyo  mwafaka  ni kuuma ulimi. Ndiyo utavimba mdomoni na hautaweza kuteta! Injili Inahitimisha ikisema kuwa Mwana wa Mungu alikuja kutafuta na kuokoa aliyepotea (Lk 19,10) . Iwapo tunakwepa ambaye unafikiri amepotea, sisi siyo watu wa Yesu. Tuombe neema ya kwenda kukutana na kila mtu kama ndugu na siyo kumwona kama adui. Iwapo alitutendea vibaya, tumrudishie wema. Mitume wa  Yesu siyo watumwa wa ubaya uliopita, bali waliosamehewa na Mungu na wanawaita kama Zakayo. Wanafikiri mazuri tu wanayoweza kufanya na hivyo tutoe bure, tupende maskini na wale ambao hawawezi kuturudishia chochote kwa maana tutakuwa matajiri machoni pa Mungu. Baba Mtakaifu Francisko amehitimisha kwa kuwatakia mema kuwa Kanisa la Kuu linaweza kuwa Kanisa ambalo kila mmoja anahisi kukumbukwa na Bwana, aliyetangulia kupokea katika nyumba. Na kwa namna hiyo Kanisa, liweze kutokea  jambo zuri  kwamba, “furahi kwa sababu wokovu umeingia nyumbani mwako” (Lk 19, 9).

22 September 2019, 10:30