Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko akiwa njiani kurejea kutoka katika hija yake ya kitume, ametuma salam na matashi mema kwa viongozi wa Barani la Afrika na watu wao. Baba Mtakatifu Francisko akiwa njiani kurejea kutoka katika hija yake ya kitume, ametuma salam na matashi mema kwa viongozi wa Barani la Afrika na watu wao. 

Baba Mtakatifu Francisko: Ujumbe kwa viongozi Barani Afrika!

Baba Mtakatifu akiwa njiani, ametuma salam, matashi mema pamoja na baraka kwa Marais wa Madagascar, Tanzania, Kenya, Sudan ya Kusini, Ethiopia, Sudan Kongwe, Misri, Ugiriki na hatimaye Italia. Baba Mtakatifu amemshukuru sana Rais Andry Rajoelina wa Madagascar kwa wema na ukarimu wao kwake, anawatakia heri na baraka tele. Muhimu: Amani, Upatanisho & Mazingira!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Hija ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko Barani Afrika kuanzia tarehe 4 hadi 10 Septemba 2019, pamoja na mambo memngine, ilipania kukuza: amani na upatanisho wa kidugu; utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote, sanjari na ujenzi wa utamaduni wa watu kukutana katika ukweli na uwazi kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu Barani Afrika. Kauli mbiu iliyoongoza hija ya Baba Mtakatifu nchini Msumbiji ni: matumaini, amani na upatanisho. Kwa upande wa Madagascar, ni “Mpanzi wa amani na matumaini” na kauli mbiu ya familia ya Mungu nchini Mauritius ni “Hujaji wa amani”. Baba Mtakatifu kabla ya kuanza safari ya kurejea tena mjini Vatican, Jumanne, tarehe 10 Septemba 2019, amepata nafasi ya kukutana na kusalimiana na wazee wanaohudumiwa na Ubalozi wa Vatican nchini Madagascar kama kielelezo cha Injili ya upendo na mshikamano na maskini ambao ni amana na utajiri wa Kanisa katika mchakato wa uinjilishaji wa kina

Baba Mtakatifu akiwa njiani, ametuma salam, matashi mema pamoja na baraka kwa Marais wa Madagascar, Tanzania, Kenya, Sudan ya Kusini, Ethiopia, Sudan Kongwe, Misri, Ugiriki na hatimaye Italia. Baba Mtakatifu amemshukuru sana Rais Andry Rajoelina wa Madagascar kwa wema na ukarimu wao kwake, anawatakia heri na baraka tele. Baba Mtakatifu amemhakikishia Rais John Pombe Magufuli na watanzania katika ujumla wao, sala zake. Amemtakia Rais Uhuru Kenyatta na familia ya Mungu nchini Kenya: baraka, amani na ustawi. Akiwa kwenye anga la Ethiopia, amewatakia heri na baraka pamoja na kuwahakikishia sala na sadaka yake kwao. Baba Mtakatifu amewahakikishia wananchi wa Sudan ya Kusini sala na maombezi yake ya daima.

Baba Mtakatifu amemtumia ujumbe wa matashi mema Abdel Fattah Abdelrahama Burhan, Mwenyekiti wa Baraza linalotawala Sudan Kongwe, akimtakia baraka na amani kwa watu wa Mungu nchini Sudan. Baba Mtakatifu katika salam na matashi mema kwa Rais wa Misri na watu wake, amewaombea furaha, amani na utulivu na kwa wananchi wa Ugiriki amewatakia neema na baraka tele. Baba Mtakatifu alipoingia kwenye anga la Italia amemtumia salam na matashi mema Rais Sergio Mattarella wa Italia akimwelezea kwamba, amehitimisha hija yake ya kitume Barani Afrika, aliko bahatika kutembelea Msumbiji, Madagascar pamoja na Mauritius. Baba Mtakatifu anasema, akiwa Barani Afrika amekutana na watu wenye imani thabiti, wenye kiu na ari ya kutaka ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Anawatakia wananchi wote wa Italia amani na utulivu pamoja na kuwahakikishia sala zake za daima.

Papa: Viongozi Afrika

 

11 September 2019, 06:43