Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko anawashukuru sana watu wa Mungu nchini Madagascar na tayari ameanza hija yake ya kitume nchini Mauritius Baba Mtakatifu Francisko anawashukuru sana watu wa Mungu nchini Madagascar na tayari ameanza hija yake ya kitume nchini Mauritius  (Vatican Media)

Hija ya Kitume ya Papa Francisko Mauritius: Mauritius kumekucha!

Baba Mtakatifu akiwa njiani kuelekea nchini Mauritius amemwandikia ujumbe wa salam na matashi mema Rais Andry Rajoelina wa Madagascar, huku akitoa shukrani zake za dhati kabisa kwa Serikali na familia ya Mungu nchini Madagascar kwa mapokezi ya kukata na shoka pamoja na ukarimu. Baba Mtakatifu ametumia fursa hii kuwapatia wananchi wa Madagascar baraka zake za kitume.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Kauli mbiu inayoongoza hija ya Baba Francisko nchini Mauritius kuanzia Jumatatu tarehe 9 hadi Jumanne 10 Septemba 2019 ni “Hujaji wa amani”. Tangu mwanzo na kwa asili yake, Kanisa Katoliki limetumwa kwa watu wote na linazungumza lugha zote za ulimwengu huu. Lakini, ikumbukwe kwamba, lugha ya Injili ni upendo. Kwa njia ya maombezi ya Bikira Maria, anamwomba Mwenyezi Mungu aweze kumkirimia nguvu za Roho Mtakatifu ili kuwatangazia na kuwashuhudia Injili, wote waweze kuifahamu na kuipokea kwa moyo mkunjufu!

Baba Mtakatifu akiwa njiani kuelekea nchini Mauritius amemwandikia ujumbe wa salam na matashi mema Rais Andry Rajoelina wa Madagascar, huku akitoa shukrani zake za dhati kabisa kwa Serikali na familia ya Mungu nchini Madagascar kwa mapokezi ya kukata na shoka pamoja na ukarimu. Baba Mtakatifu ametumia fursa hii kuwapatia wananchi wa Madagascar baraka zake za kitume pamoja na kuendelea kuwaombea amani na utulivu. Baba Mtakatifu alipowasili Uwanja wa ndege wa Port Louis nchini Mauritius amelakiwa na viongozi wa Serikali na Kanisa pamoja na umati mkubwa wa familia ya Mungu. Amesikiliza nyimbo za mataifa haya mawili, akakagua gwaride na baadaye kuelekea kwenye Mnara wa Bikira Maria. Malkia wa amani, kwa ajili ya kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa heshima ya Mwenyeheri Jacques Dèsirè Laval.

Papa: Mauritius

 

09 September 2019, 19:06