Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko asikitishwa sana na maafa yanayoendelea kujitokeza kutoka na mvua za Moonson huko nchini India. Baba Mtakatifu Francisko asikitishwa sana na maafa yanayoendelea kujitokeza kutoka na mvua za Moonson huko nchini India.  (AFP or licensors)

Papa asikitishwa na maafa ya mvua za Monsoon nchini India

Mvua za Monsoon zimesababisha majanga katika maeneo mengi nchini India. Lakini sehemu zilizoathirika zaidi ni: Kerala, Karnataka, Maharashtra pamoja na Mkoa wa Gujarat. Takwimu zinaonesha kwamba, kuna watu zaidi ya 178 wamefariki dunia kutokana na mafuri na watu zaidi ya milioni moja hawana makazi ya kudumu. Athari ni kubwa zaidi kwenye maeneo ya vijijini na mabondeni.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

India imekuwa ikikabiliwa na ukame wa muda mrefu, lakini hali ya hewa kwa sasa imebadilika na kwamba, mvu za Monsoon zinaendelea kunyeesha kwa kiwango kikubwa kuliko hata ilivyokuwa imetarajiwa. Hali hii tayari imesababisha majanga asilia katika maeneo mengi nchini India. Lakini sehemu zilizoathirika zaidi ni: Kerala, Karnataka, Maharashtra pamoja na Mkoa wa Gujarat. Takwimu zinaonesha kwamba, kuna watu zaidi ya 178 wamefariki dunia kutokana na mafuriko pamoja na watu zaidi ya milioni moja hawana makazi ya kudumu. Taarifa zinabainishwa kwamba, athari ni kubwa zaidi kwenye maeneo ya vijijini.

Baba Mtakatifu Francisko ameguswa na mahangaiko pamoja na mateso ya wananchi wa India wanaoendelea kupambana na mafuriko katika kipindi hiki. Baba Mtakatifu katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kwenda kwa viongozi mahalia anasema anapenda kutuma salam zake za rambi rambi  kwa wale wote walioguswa na msiba huu mzito kwa kuondokewa na ndugu, jirani na marafiki. Anawaombea wale wote waliopata majeraha, ili waweze kupona na hatimaye, kuendelea na shughuli zao za kawaida. Baba Mtakatifu anaendelea kuwatia shime wale wote wanaoendelea kujisadaka kwa ajili ya huduma makini kwa watu wa Mungu walioathirika kwa mafuriko makubwa nchini India pamoja na kutoa baraka zake za kitume kwa India katika ujumla wake.

Papa: India

 

13 August 2019, 13:40