Tafuta

Vatican News

Papa Francisko:Ujumbe kwa njia ya video kuhusu nia za mwezi Juni

Nia za sala ya Baba Mtakatifu kwa mwezi Juni 2019 anasema,tuombe ili mapadre kupitia unyenyekevu wa maisha yao wakubali wajibu wa kuwa na mshikamano na zaidi ya yote na wale walio masikini kabisa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika nia za maombi ya Baba Mtakatifu kwa njia ya video kwa mwezi wa Juni 2019 yanajikita katika mtindo wa maisha ya mapadre na hivyo Baba Mtakatifu Francisko anasema: “ ninapenda kuwaomba kuwa na mtazamo wa  kuwaangalia mapadre ambao hawajakamilika, lakini wengi wao wanajitoa mpaka mwisho kwa unyenyekevu na furaha.

Mapadre walio karibu na watu na utayari wa kufanya kazi kwa bidii

Ni mapadre ambao wapo karibu na watu na wapo tayari kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya kila mmoja. Tunawashukuru kwa mfano wao na ushuhuda wao.Tuombe ili mapadre kupitia maisha yao wakubali wajibu na kuwa na mshikamano na zaidi ya yote na wale walio masikini kabisa.

06 June 2019, 16:33