Tafuta

Vatican News
Tarehe 8 Juni Papa Francisko ametoa wito wa kusali kwa dakika moja kwa ajili ya kuombea amani nchi za Mashariki na kwingineko Tarehe 8 Juni Papa Francisko ametoa wito wa kusali kwa dakika moja kwa ajili ya kuombea amani nchi za Mashariki na kwingineko 

Papa Francisko ametoa wito wa kusali kwa ajili ya amani ya nchi za Mashariki!

Wakati wa salam zake Baba Mtakatifu kwa lugha ya kiitaliano ametoa wito ili kusali kwa ya dakika moja kwa ajili ya amani tarehe 8 Juni saa saba mchana masaa ya Ulaya,akikiumbuka kuanzishwa kwa Jukwa la kimataifa la Chama cha Kitume katoliki baada ya mwaka mmoja.Vile vile amekumbusha Dominika 9 Juni ni siku Kuu ya Pentekoste!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mara baada ya katekesi yake tarehe 5 Juni 2019, Baba Mtakatifu Francisko amesalimia mahujaji mbalimbali kutoka duniani wakiwa ni makundi ya maparokia,  na wawakilishi mbalimbali. Zaidi mawazo ya Baba Mtakatifu Francisko yamewaendea vijana, wazee. Wagonjwa na wana ndoa wapya.

Baba Mtakatifu amekumbusha maadhimisho ya Sikukuu ya Pentekoste

“Dominika ijayo tutaadhimisha Siku kuu ya Pentekoste. Bwana  awakute mko tayari kupokea kwa wingi wa mapaji ya Roho Mtakatifu, neema ya zawadi zake iwashukie ndani mwenu na kuwaongeza nguvu mpya katika imani na kuwaimarisha matumaini kwa kuwapatia  nguvu za utendaji wa upendo”.Amesema Baba Mtakatifu.

Wito wa  sala ya dakika moja kwa ajili ya amani tarehe 8 Juni saa saba mchana masaa ya Ulaya

Aidha, “Kutumia dakika moja kwa ajili ya amani kwa sala kwa waamini; kutafakari kwa pamoja na yule ambaye aamini. Wote pamoja kwa ajili ya dunia ya kidugu”. Ndiyo mwaliko wa Baba Mtakatifu Francisko wakati anatoa salamu kwa waamini wa lugha ya kitaliano ambapo kwa kawaida ndiyo wanahitimisha Katekesi yake ya kila Jumatano wakati wa salam. Baba Mtakatifu Francisko anasema kwa ni  tarehe 8 Juni ambayo inakumbusha mwaka wa tano tangu kukutana mjini Vatican na Rais wa Israeli na Palestina, nikiwa pamoja na Patriaki Bartholomew.  Saa saba mchana tunaalikwa kutumia dakika moja kwa ajili ya amani, na wote kwa pamoja kwa ajili ya dunia ya kidugu zaidi. Hata hivyo ni  shukrani kwa Chama katoliki cha vijana kimataifa ambao wanaamasisha mkesho huo wa sala!

Na  katika kukumbuka sikukuu hii ya Pentekeoste, Baba Mtakatifu pia amerudia kuwakumbushia hata makundi ya lugha tofauti. Katika lugha ya kipoland amesema “Tufungue akili zetu na mioyo yetu katika matendo ya Roho Mtakatifundani mwetu ili iweze kututakatifuza na kutufanya tuwe mashuhuda wa Kristo mbele ya dunia ambayo tunaishi”.

05 June 2019, 14:22