Tafuta

Vatican News
Papa Francisko anawataka waamini kuyatolea mahangaiko yao kwa Kristo Yesu ili aweze kuwatia nguvu na kuwafariji! Papa Francisko anawataka waamini kuyatolea mahangaiko yao kwa Kristo Yesu ili aweze kuwatia nguvu na kuwafariji!  (Vatican Media)

Hija ya Kitume Romania: Mateso na mahangaiko ya wagonjwa!

Baba Mtakatifu Francisko amewataka waamini wote hawa kuyatolea mahangaiko yao kwa Kristo Yesu, ili aweze kuwatia nguvu na kuwafariji katika mahangaiko yao ya kila siku. Mwishoni, kwa pamoja wamesali na kuwaomba waendelee kumkumbuka katika sala na sadaka yao, ili aweze kutekeleza vyema dhamana na utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi, tarehe 1 Juni 2019 mara tu baada ya maadhimisho ya Ibada ya Misa Takatifu kwa heshima ya Bikira Maria kwenye Madhabahu ya “Șumuleu Ciuc” yaani Bikira Maria mfariji wa wanaoteseka, alipata nafasi ya kutembelea Kanisa kuu la Bikira Maria Malkia wa mbingu lililoko Iasi, huko Romania. Kanisa hili lilitabarukiwa kunako mwaka 2005 baada ya kazi kubwa ya ujenzi uliodumu miaka kumi na miwili. Kanisa hili linahifadhi masalia ya Mwenyeheri Anton Durcovici, Askofu wa Ias na shuhuda wa imani aliyeuwawa kikatili kunako mwaka 1951.

Itakumbukwa kwamba, hija hii ya kitume inaongozwa na kauli mbiu “Twende pamoja” ili kujenga na kudumisha umoja na mshikamano wa kitaifa; kwa kufuata nyayo za mashuhuda wa imani, waliomimina maisha yao kwa ajili ya Kristo na Kanisa lake! Akiwa Kanisani hapo, Baba Mtakatifu ametoa baraka zake za kitume pamoja na kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyemwezesha kutembelea Kanisa hili pamoja na kusalimiana na wagonjwa na wazee. Baba Mtakatifu, amewataka waamini wote hawa kuyatolea mahangaiko yao kwa Kristo Yesu, ili aweze kuwatia nguvu na kuwafariji katika mahangaiko yao ya kila siku. Mwishoni, kwa pamoja wamesali na kuwaomba waendelee kumkumbuka katika sala na sadaka yao, ili aweze kutekeleza vyema dhamana na utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro!

Papa: Kanisa
02 June 2019, 15:59