Tafuta

Baba Mtakatifu akisalimiana na mahujaji wakati wa katekesi ya tarehe 19 Juni 2019 Baba Mtakatifu akisalimiana na mahujaji wakati wa katekesi ya tarehe 19 Juni 2019 

Papa anakumbusha sikukuu ya Mtakatifu Alois Gonzaga!

Mara baada ya katekesi tarehe 19 Juni 2019,Baba Mtakatifu Francisko amesalimia mahujaji na waaamini wote na kuwakumbusha juu ya sikukuu ya Mtakatifu Alois Gonzaga ya tarehe 21 Juni.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mara baada ya Katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko tarehe 19 Juni 2019, amewasalimia mahujaji na waamini wote kutoka pande zote za dunia. Aidha bila kuwasahahu vijana, wazee, wagonjwa na wanandoa wapya hasa wanaotoka katika Jimbo katoliki la Tivoli Italia waliosindikizwa na Askofu wao.

Papa kukumbusha Sikukuu ya Mtakatifu Alois Gonzaga

Baba Mtakatifu Francisko amekutambusha kuwa tarehe 21 Juni ni maadhimishao ya Mtakatifu Luigi Gonzaga, mwenye mfano wa kweli  wa kuigwa na usafi wa kiinjili. Anawaomba waamini wote kumwomba  Yeye ili aweze kuwasadia kujenga urafiki wa kina na Yesu  aweze kuwafanya wawe na uwezo wa kukabiliana kwa utulivu maisha yao.

Historia ya Mtakatifu Alois

Mtakatifu Aloysius Gonzaga alizaliwa  katika ngome ya familia yake huko Castiglione delle Sitivniere katikati ya Brescia na Mantova Kaskazini Italia kunako tarehe 9 Machi 1568 na kifo chake tarehe  21 Juni 1591. Yeye  alikuwa mtoto wa kwanza kati ya watoto sabaa wa  mfalme mdogo nchini Italia aliyeitwa , Ferrante de Gonzaga (1544-1586), Mtawala wa Castiglione, na Marta Tana di Santena, binti wa baron wa familia ya Piedmont Della Rovere. Kama mtoto wa kwanza, alikuwa na haki ya kurithi cheo cha baba yake (Marquis). Baba yake alidhani kwamba Aloysius atakuwa askari, kama ilivyokuwa kawaida kwa wana wa familia maarufu zilizohusika mara nyingi na katika vita vidogo vya kipindi hicho.

Hivyo mafunzo yake ya kijeshi yalianza wakati akiwa mdogo mno, lakini pia alipata elimu katika lugha na sanaa. Alipokuwa na umri wa miaka minne, Luigi alipewa bunduki ndogo na alitumwa na baba yake kwenye safari za mafunzo ili mtoto huyo aweze kujifunza "sanaa ya mapigano". Alipokuwa na umri wa miaka mitano, Aloysius alipelekwa kambi ya kijeshi ili kuanza mafunzo yake. Baba yake alifurahia kumwona mwanawe akizunguka kambi akiwa kama mkuu wa askari. Mama yake na mwalimu wake hawakufurahia sana na maneno yake na misamiati aliyochukua huko.

Maisha yake baadaye yalianza kubadilika na baadaye kuwa mjesuiti

Aloysius alianza kufikiria kwa bidii kuhusu kujiunga na utawa. Alifikiri kujiunga na shirika fulani, lakini alivutwa na uaminifu wa Wajesuiti huko Madrid na aliamua badala yake kujiunga nao. Mama yake alikubali ombi lake, lakini baba yake alikasirika na kumzuia kufanya hivyo. Na  alikataa kabisa kuurithi utawala akawa mtawa katika shirika la Wajesuiti. Yeye alipata mauti bado kijana akihudumia wagonjwa wa tauni mjini Roma, na kukuiacha kumbukumbu bora hasa ya usafi wa moyo na malipizi. Kunako mwaka 1726 Mama Kanisa alimtangaza kuwa mtakatifu. Na Sikukuu yake  ya kila mwaka inaadhimishwa ifikapo  tarehe 21 Juni kila mwaka.

19 June 2019, 13:16