Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko ametoa  tafakari yake tarehe 21 Juni 2019 kwenye  hitimisho la Mkutano huko Napoli katika Taasisi ya Kitaalimungu kitengo cha San Luigi Baba Mtakatifu Francisko ametoa tafakari yake tarehe 21 Juni 2019 kwenye hitimisho la Mkutano huko Napoli katika Taasisi ya Kitaalimungu kitengo cha San Luigi  (Vatican Media)

Papa amekazia juu ya majadiliano na makaribisho kwa ajili ya Mediterranea ya amani!

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa hotuba yake iliyokuwa inahitimisha tafakari la mkutano katika Taasisi ya kitivo cha Kitaalimungu huko Kusini mwa Italia ametoa wito kuhusu taalimungu ya makaribisho inayokita juu ya majadiliano na kutangaza Neno.Taalimungu inayochangia kujenga jamii ya kidugu kati ya watu wa Mediterranea.Baada ya hotuba yake amerudi mjini Vatican.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko ametoa  tafakari yake tarehe 21 Juni 2019 kwenye  hitimisho la Mkutano huko Napoli katika Taasisi ya Kitaalimungu kitengo cha San Luigi, uliongozwa na mada Taalimungu baada ya Varitatis gaudium katika mantiki ya Mediterranea. Kwenye hotuba hiyo, hatua ya kuanza inatazama Katiba ya kitume iliyotangazwa tarehe 8 Desemba 2017 ambayo yeye mwenyewe alipendelea kuifafanua katika mafunzo ya kitaalimungu hasa kwa upyaisho, ikiwa na maana ya Kanisa linalo toka nje. Baba Mtakatifu Francisko ameanza na tafakari yake kwa kukumbusha kwamba, Maditerranea daima imekuwa mahali pa kupitia, mahali pa kubadilishana mawazo na wakati mwingine hata uwepo wa   migogoro ambayo leo  hii wote wanaitambua na ni kipeo hasa cha majanga makubwa! Ili kuweza kukabiliana nayo Papa Francisko anasema inahijika Taalimungu ya makaribisho, yenye kujipanua katika maendeleo ya majadiliano ya kweli na wazi, katika ujenzi wa amani ndani ya jamii inayo unganisha na udugu kwa ajili ya kulinda kazi ya uumbaji.

Baba Mtakatifu Francisko ameonesha mambo makuu mawili kuhusu majadiliano na kerygma yaani tangazo la Kristo aliyekufa na kukufuka kama mantiki kwa ajili ya upyaisho wa Kanisa ambao linakita kwa kina cha uinjilishaji. Akifafanua amesema ni majadiliano awali ya yote katika mtindo wa mang’amuzi, wa kutangaza na  yenye uwezo wa kuwa na uhusiano kwa hali ya maisha ya ubinadamu. Ni Mtakatifu Francis wa Assisi ambaye anaonesha ni kwa jinsi gani majadiliano na kutangaza, vinaweza kuleta pamoja na kushuhudia upendo wa Mungu kwa ajili ya watu wote. Hii lakini inahitaji upeo wa Roho kwa maana ya mtindo wa maisha na kutunza bila roho ya kutaka mafao binafsi, bila kuwa na  tamaa ya kufanya upropaganda na bila nia ya kufanya  fujo na kukataa. Inahitaji majadiliano na watu, utamaduni wao ambao unajikita hata kushuhudia hadi kufikia kijisadaka maisha binafsi kama walivyo fanya wengine. Na kati yao amewataja:Charles de Foucauld,  wamonaki wa Tibhirine na  Askofu wa Oran Pierre Claverie (Petro Claveri).

Katika majadiliano hayo Baba Mtakatifu anawatia moyo kwenye  Kitivo cha Kitaalimungu ambacho kina kozi mbalimbali za lugha na utamaduni wa kiarabu hata wa kiyahudi ili kukuza uhusiano wa kiyahudi na kiislam kwa kuzingatia mizizi ya pamoja na tofauti zake. Kwa upande wa waislam anasema, wote  tunaalikwa kujadiliana kwa ajili ya kujenga wakati ujao wa jamii zetu na miji yetu, kufikiria pamoja kama  washiriki kwa ajili ya kujenga amani ya kuishi,  hata kama yapo matukio ya kutisha yenye kuleta usumbufu kwa njia ya makundi ya kushukiwa na  ambayo ni adui wa majadiliano. Na kwa upande wa wayahudi anawataka  waweze kuishi vema hasa kuwa na husiano kwa ajili ya mpango wa dini. Mediterranea, anabainisha Papa ni daraja kati ya Ulaya, Afrika na Asia, ni nafasi ya kujenga hema kubwa la amani  mahali ambapo wanaweza kuishi kama watoto tofauti wa baba Ibahimu.

Akiendelea na hotuba yake Baba Mtakatifu Francisko ametoa wito kwa wataalimungu kwamba, “katika safari hii ya kuendelea kutoka nje yake na kukutana na mwingine ni muhimu kwamba wataalimungu wawe wanawake na wanaume wenye kuwa na huruma, wanaoongoza  maisha ya wengi wenye kuelemewa  na utumwa mamboleo, majanga ya kijamii, ya vurugu na kutumia nguvu, ya vita na ukosefu mkubwa wa usawa ambao unawakumba masikini wengi wanaoishi   pembezoni mwa bahari hiyo ya pamoja. Bila kumunio na bila uhuruma inayoendelea na kuimarishwa na sala, taalimungu inapoteza si tu roho, lakini pia hata inapoteza akili na uwezo wa kutafsiri hali halisi ya kikristo”, Amebainisha Baba Mtakaifu. Na katika hilo  ametaja matukio ya “tabia za fujo na vita”, mazoezi ya kikoloni” ya “kuhalalisha vita”  na “mateso yanayofanywa kwa kutumia jina la dini au madai ya kutumia rangi au mafundisho ya dini”. Mtindo wa majadiliano, unaoongozwa na huruma, unaweza kutajirisha somo dhidi ya uchungu huu wa historia kwa kupinga na  kuleta unabii wa amani ambayo Roho  haikuwahi kushindwa”. Hata hivyo ina maana ya kufanya taalimungu ya mshikamano na manusura wa historia. Kwani somo hilo ambalo wakristo wa Mashariki wamejifunza kutokana na makosa mengi na matokeo ya wakati uliopita, inaweza kurudia katika vyanzo vyao kwa kuwa na matumaini ya kuweza kushuhudia Habari Njema kwa watu wa mashariki na magharibi, wa kaskazini na kusini. Taalimungu (…) inaweza kusaidia Kanisa na jamii ya kiraia kuanza njia mpya na manusra wengi, kuwatia moyo watu wa Kimediterranea ili kuweza kukataa kila aina ya kishawishi cha kutaka faida na kujifungia ndani ya utambulisho binafsi.

Kazi ya Taalimungu ni ile ya kuweka maelewanao na Yesu Mfufuka na kuifikisha  katika sehemu za pembezoni “hata ile ya mawazo”, amesisistiza Baba Mtakatifu Francisko. Kwa maana hiyo, wataalimungu lazima “wakuze makutano ya tamaduni kwa njia ya vyanzo vya Uhusiano na Utamaduni”, lakini pia  Baba Mtakatifu Francisko anaweka taadhali kwamba, “ maonyesho makubwa ya  kitaalimungu ya zamani ni machimbo ya hekima ya Taalimungu”  na mbayo lakini kimsingi hayawezi kutumiwa katika masuala ya sasa. Hii ina maana ya kuifanya taalimungu kuwa ya thamani katika kutafuta njia mpya”. Shukrani kwa Mungu vyanzo vya kwanza vya  taalimungu, yaani Neno la Mungu na Roho Mtakatifu, bado  vinadumu na daima vinazaa matunda, kwa maana hiyo inawezekana, na ni lazima kufanya kazi katika mwelekeo wa “Pentekoste ya kitaalimungu” ambayo inaruhusu wanawake na wanaume wa nyakati zetu kusikiliza kwa lugha binafsi katika tafakari ya kikristo ambayo inaendana na utafiti wa maana yao  na maisha timilifu. Na ili kuweza kufanya hivyo, Baba Mtakatifu Francisko amesema inahitajika “kuanzia na Injili ya huruma” kwa sababu taalimungu inazaliwa katikati ya watu wa kweli, waliokutana na mtazamo wa Mungu anaye kwenda  kuwatafuta kwa upendo. Kadhalika kufanya taalimungu ni tendo la huruma (…): “Hata wataalimungu wema kama vile wachungaji wema, wana harufu ya watu, ya njia na kwa tafakari yao  wanapaka mafuta na kutia divai katika majeraha ya watu. Taalimungu kama kielelezo cha Kanisa ambayo ni Hospitali katika kambi, pia inaishi utume wake wa wokovu na uponyaji katika dunia !”

Baba Mtakatifu Francisko pia amesisitiza kuwa “ ni lazima kuwa na taalimungu huru kwa sababu bila uwezekano wa kufanya uzoefu wa njia mpya, haiwezekani kuwa na  lolote jipya”. Yote hayo yanapaswa yaelekezwe kwa ajili ya kuunda uwezekano wa ushiriki na wale ambao wanatamani mafunzo ya taalimungu! Na zaidi ya waseminari na watawa, hata walei na wanawake, wanaoota Kitivo cha Taalimungu,wanaalikwa kuwa  mahali ambapo ni pa kuishi pamoja na tofauti zao, mahali penye kufanya uzoefu wa taalimungu ya majadiliano na makaribisho; mahali ambapo ni kufanya uzoefu wa mtindo wa maarifa mengi ya kitaalimungu katika  eneo la uwanja wenye msimamo. Mahali ambapo utafiti wa kitaalimungu una uwezo wa kukuza uwajibu lakini pia hata uwezo wa kukuza mchakato unaofaa wa utamadunisho.

Taalimungu baada ya Veritas gaudium, yaani furaha ya ukweli Baba Mtakatifu anahitimisha inajikita kwa dhati katika majadiliano na tamaduni na dini ili kujenga na  kuishi kwa amani kati ya mtu na watu.” Vigezo vya Katiba ya kitume ya Veritatis gaudium ni vigezo vya kiinjili. Kerygma, majadiliano, mang’amuzi ushirikiano, mitandao ni mambo yote ambapo yeye anaongea kusema kuwa ni sauti  ambayo imesemwa kama kigezo chenye  uwezo wa kuwa na kikomo cha  kuvumilia, kuwa na kikomo cha kwenda mbele, na kigezo cha kutafsiri. Vigezo hivyo ndivyo Injili iliishi na kutangaza na Yesu na ambavyo vinaweza pia kupelekwa leo hii na wanafunzi wake! Mediterranea ni mama wa historia ya kihistoria, kijiografia na utamaduni wa kupokea kerygma ambayo ilifanywa na majadiliano na huruma. Katika utafiti wa taalimungu hii, Napoli ni mfano na maabara maalum. Kazi njema! amehitimisha Baba Mtakatifu!

21 June 2019, 13:04