Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko asikitishwa sana na kifo cha Martinez Ramirez na Binti yake Valeria waliokuwa wanatafufa hifadhi ya kisiasa nchini Marekani! Papa anawakumbuka wahamiaji na wakimbizi! Baba Mtakatifu Francisko asikitishwa sana na kifo cha Martinez Ramirez na Binti yake Valeria waliokuwa wanatafufa hifadhi ya kisiasa nchini Marekani! Papa anawakumbuka wahamiaji na wakimbizi!  (AFP or licensors)

Papa aguswa na kusikitishwa na kifo maji cha baba na binti yake!

Martinez Ramirez na binti yake Valeria, kutoka nchini Salvador, wamekufa maji, Jumapili tarehe 23 Juni 2019, kwenye Mto wa Rio Grande, mpaka unaotenganisha Marekani na Mexico, wakiwa kwenye harakati za kutafuta: usalama, hifadhi na maisha bora zaidi. Katika mkasa huu, amesalimika Vanessa Avalos, Mama wa familia hii ambayo kwa sasa imegubikwa na majonzi makubwa. Inasikitisha!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameguswa na kusikitishwa sana na picha ya Bwana Martinez Ramirez na binti yake Valeria, kutoka nchini Salvador, waliokufa maji, Jumapili tarehe 23 Juni 2019, kwenye Mto wa Rio Grande, mpaka unaotenganisha Marekani na Mexico, wakiwa kwenye harakati za kutafuta: usalama, hifadhi na maisha bora zaidi. Katika mkasa huu, amesalimika Vanessa Avalos, Mama wa familia hii ambayo kwa sasa imegubikwa na majonzi makubwa. Bwana Martinez Ramirez na binti yake Valeria wamefariki dunia hata kabla ya Mahakama nchini Marekani kuanza kusikiliza ombi lao la kutaka kupewa hifadhi ya kisiasa nchini humo.

Mashuhuda wanasema, Bwana Ramirez alifanikiwa kumvusha binti yake na kumweka mahali pakavu upande wa Marekani, akaamua kurejea tena ili kumchukua mke wake, mtoto Valeria alipoona baba yake amerudi mtoni, akamfuata na alipogeuka kutaka kumwokoa binti yake, wakakumbwa na mkondo mzito wa maji; wote wawili wakapoteza maisha! Baba Mtakatifu anamkumbuka na kumwombea marehemu Martinez Ramirez pamoja na binti yake, waliopoteza maisha, kama ilivyo hata kwa wakimbizi na wahamiaji wengi kutoka sehemu mbali mbali za dunia, wanaoendelea kufa maji, kiu na utupu na wala hawana tena watu wa kuomboleza juu ya vifo vyao!

Papa: Masikitiko
27 June 2019, 15:09