Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko alipokutana na washiriki wa Mkutano wa kimataifa wa Yes to life amekazia umuhimu wa madaktari kutambua wito wao, kusindikiza na kufariji Baba Mtakatifu Francisko alipokutana na washiriki wa Mkutano wa kimataifa wa Yes to life amekazia umuhimu wa madaktari kutambua wito wao, kusindikiza na kufariji  (ANSA)

Papa Francisko:Utoaji mimba siyo jibu kwa familia wanaotafuta kufanya hivyo!

Akikutana na washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Yes to life,tarehe 25 Mei 2019 Baba Mtakatifu amebainisha jambo muhimu linalofaa kwa madaktari hasa wakati wa kusindikiza wagonjwa kuwa ni uwezo wa kufanya mahusiano ya dhati na kubeba maisha ya wengine hasa mbele ya uchungu na uwezo wa kufariji wakati huo kutafuta suluhisho daima kulingana na kila maisha ya binadamu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Utaalam wa udaktari ni utume wito wa maisha na muhimu kwa madaktari kuwa na uwezo wa kujitambua kuwa wao ni zawadi kwa familia ambazo wanakabidhiwa. Amesema hayo Baba Mtakatifu kwa washiriki wa Mkutano wa kimataifa ulioandaliwa na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha wakiogozwa na mada "Yes to life –Utunzaji wa thamani ya zawadi ya maisha katika udhaifu, tarehe 25 Mei 2019. Baba Mtakatifu Francisko  amesisitiza kwamba utoaji wa mimba kamwe siyo jibu kwa wanafamilia wanaotafuta kufanya hivyo!

Kuwa makini na kutambua kupokea hali halisi kwa ajili ya upendo wa familia

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na hotuba yake na washiriki wa “Yes to life” ameelezea juu ya kuwa na mtazamo makini unao tambua kupokea maana ya dhati na  jitihada kuelekeza utimilifu wa upendo wa familia hasa zile zinazo jikuta katika hali ngumu ya kumpokea mtoto mdhaifu au mlemavu. Amesema yote hayo yanajionesha katika  ulazima hasa mbele ya watoto ambao kwa sasa katika utambuzi wa kisayansi wamehukumiwa kufa hata mara baada ya kuzaliwa au muda mfupi baadaya ya kuzaliwa.

Katika kesi hii, tiba inaweza kufikiriwa labda haina maana ya kutumia rasilimali na mateso makubwa kwa wazazi wao. Lakini Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza kuwa  moja ya mtazamo makini unaotambua ni  kupokea maana ya dhati na kuwa na  jitihada katika kuelekeza utimilifu wa upendo wa familia. Kutunza watoto hao unasaidia kwa hakika kuanza kuandaa hata maombolezo na kutambua kuwa siyo kupoteza, bali ni hatua ya safari ya mchakato wa pamoja. Watoto hao watabaki daima katika maisha yao, amesisitiza Baba Mtakatifu. Na wao wangeweza kupendwa na wazazi wao. Hata hivyo  Baba Mtakatifu Francisko ameongeza kusema, masaa machache ambayo mama angeweza kusaidia mtoto wake, ni dhahiri kwamba unamwachia  uzoefu wa ishara ndani ya moyo wa mama huyo na  ishara ambayo hataweza kamwe kuisahau. Na yeye anahisi kwa hakika kukamilika na kuhisi kuwa ni mama.

Maisha ya binadamu ni matakatifu na hayawezi kukiukwa hadhi yake hata katika matumizo ya utafiti

Baba Mtakatifu Fancisko akiendelea na hotuba yake anabainisha kwamba  utamaduni wa sasa  ambao hauhamasishi mkakati huo kwa ngazi ya kijamii kwa kuogopa ugumu mbele ya ulemavu na ambao mara nyingi unapelekea uchaguzi wa kutoa mimba, kwa kufikiria kuwa ndiyo suala la kuzuia. Lakini Mafundisho ya Kanisa Katoliki kuhusiana na hili inaonesha wazi kwamba “maisha ya binadamu ni matakatifu na hayawezi kukiukwa hadhi yake  na matumizi ya utambuzi wa ujauzito kabla ya kujifungua yasiwe ni matokeo ya kukatisha tamaa kwa nguvu, kwa sababu ni kielelezo cha mawazo yasiyo ya kibinadamu ambayo huondoa familia ule uwezekano wa kukaribisha, kukumbatia na kupenda watoto wao dhaifu!

Ni halali kuonda maisha ya binadamu kwa ajili ya suluhisho ma tatizo?

Mara nyingi, Baba Mtakatifu amebainisha kwamba unasikia wanasema: " ninyi wakatoliki hamkubali utoaji wa mimba, ni matatizo ya imani yenu”. Lakini amebainisha Baba Mtakatifu kwamba sehemu hii  siyo tatizo la dini. Imani haiingiliani na hilo. Inakuja baadaye, lakini haiingiliani. Tatizo ni la kibinadamu. Ni tatizo ambalo linalikuja kabla ya dini. Kwa maana hiyo ameonya Baba Mtakatifu kwamba: Tusibebeshe imani jambo ambalo halisitahili kuwa hivyo. Ni tatizo la kibinadamu. Kutokana na hiyo ametoa maswali mawili ya kuweza kusaidia ili kutambua vizuri. Swali la kwanza : Ni halali kuondoa maisha ya binadamu kwa ajili ya suluhisho la tatizo? Swali la pili: ni halali kukodisha muuaji ili kutatua tatizo? “Jibu ni lenu”. “Hii ndiyo hatua”. Amesema Baba Mtakatifu na kuongeza: Usiingilie katika dini kutokana na kitu ambacho kinahusisha mwanadamu. Haikubaliki. Haikubaliki kamwe kuondoa maisha ya mtu au kukodisha mtu wa kuua ili  kutatua tatizo. Amesitiza Baba Mtakatifu Francisko!

Utoaji mimba siyo jibu kwa mwanamke na familia wanaotafuta kufanya hivyo

Utoaji wa mimba kamwe siyo jibu kwa wanawake na familia wanaotafuta kufanya hivyo ameonya Baba Mtakatifu Francisko. Zaidi ni hofu ya ugonjwa na upweke ambao unawakumba wazazi hao. Matatizo ya kila siku ya kibinadamu na kiroho hayawezi kukataliwa, anasema Baba Mtakatifu, lakini ndiyo hatua inayohitaji matendo ya kichungaji na nyeti ili kukabiliana na dharura hiyo na ulazima wa kusaidia wale wote wanaokubali kuwapokea watoto wagonjwa. Ni lazima kuunda nafasi na eneo na mitindo ya upendo ambayo familia zenye matatizo, wanaweza kwenda kama vile  hata kutumia muda kuwasindikiza familia hizo, ametoa ushauri.

Historia ya msichana wa miaka 15 mwenye Mtindio wa ubongo

Aidha Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na hotuba yake amependelea kuta mfano kwa kusimulia historia  moja ya kusisimua kutoka katika jimbo fulani. Kulikuwa na kijana msichana wa umri wa miaka 15 mwenye Mtindio wa ubongo ambaye alibeba mimba na wazazi wake wakaenda kwa hakimu kuomba ruhusa ya kutoa mimba. Hakimu alikuwa ni mwenye busara, anasema Baba Mtakatifu na kwamba alikuwa ameelimika kwa maana alijibu kuwa: "ninataka kumuuliza mtoto mwenyewe, na wazazi wakajibu mtoto mwenyewe haelewi… lakini hakimu akasema hapana, ni lazima aje. Msichana huyo alipelekwa na kukaa mbele na kuzungumza na hakimu.

Hakimu: hivi unajua kile ambacho kimetukia kwako?  Mtoto akajibu: “ndiyo mimi ni mgonjwa…” Hakimu: ugonjwa wako ni upi?  Mtoto akajibu: “nimeambiwa kuwa ndani nina mdudu anayekula tumbo, hivyo wanataka kufanifanyia operesheni”.  Hakimu akamwambia: “hapana wewe huna mdudu anaye kula tumbo. Je unajua ni kitu kipo gani ndani? ni Mtoto!”...

Mtoto huyo mwenye utindio wa ubongo kusikia huivyo alijibu: aaah!  jamani ni vizuri!” … Kutokana na jibu hilo, Baba Mtakatifu amethibitisha kuwa, Hakimu hakuweza kuwapa ruhusa ya kutoa mimba, kwa maana mama yake alikuwa anamtaka mtoto wake. Baada ya muda mtoto  huyo alizaliwa, akakua, alisoma na baadaye mtoto huyo akawa Wakili. Kutokana na kwamba alisimuliwa historia yake, kila mwaka wakati wa fursa ya siku kuu yake ya kuzaliwa, alikuwa anamkaribisha Hakimu na kumshukuru kwa ajili ya zawadi ya kuzaliwa. Mambo ya maisha huwezi kujua Baba Mtatakatifu amesema na kuongeza kusema kuwa, baada ya kifo cha hakimu, mtoto huyo amekuwa mwahamasishaji wa haki. Baba Mtakatifu Francisko amesema na tazama mambo mazuri: utoaji mimba kamwe siyo jibu ambalo wanawake na familia wanatafuta.

Amehitimisha kwa kuwashukuru wote wanaojitoa kwa ajili ya kazi hiyo na kusema: “Ninawashukuru kwa namna ya pekee ninyi familia, mama na baba ambao mmekubali maisha madhaifu na ambayo sasa ninyi ni msaada na msaada wa mwingine kutoka katika familia nyingine. Ushuhuda wenu wa upendo ni zawadi kwa dunia”. Baba Mtakatifu amewabariki na kuwahikikishia sala zao. Pia wasali kwa ajili yake.

27 May 2019, 10:37