Cerca

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Tafakari ya Jumapili 19 Mei 2019 ameuliza swali:Je mimi ninauwezo wa kupenda adui? Kila mmoja ajibu nafsini mwake Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Tafakari ya Jumapili 19 Mei 2019 ameuliza swali:Je mimi ninauwezo wa kupenda adui? Kila mmoja ajibu nafsini mwake  (ANSA)

Papa Francisko:Upendo wa Yesu unafungua upeo wa matumaini!

Wakati wa Tafakari ya Malkia wa Mbingu,Baba Mtakatifu Francisko anakumbusha kuwa:Yesu anatuomba kupendana sisi kwa sisi na si kwa upendo wetu bali kwa upendo wake ambao unatufanya tuwe watu wapya.Upendo huo kwa dhati unatafanya tuwe na uwezo wa kusamehe,kupenda maadui,kujenga madaraja,kufundisha njia mpya na kushinda vizingiti.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika mwanzo wa  tafakari ya Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Sala ya Malkia wa Mbingu tarehe 19 Mei 2019 kwa waamini na mahujaji waliofika mjini Vatican kushiriki naye sala hiyo amesema: Injili ya leo inatupeleka katika karamu ya mwisho ili kutufanya tusikilize baadhi ya maneno ambayo Yesu aliwambia wafuasi wake katika hotuba yake ya mwisho kabla ya mateso yake. Akiendelea na tafakari hiyo Baba Mtakatifu Francisko amesema, baada ya kuwaosha miguu Mitume kumi na mbili, Yeye alisema:“Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo”. (Yh13,34).  Lakini Yesu ana maana gani kuiita “amri mpya”, Baba Mtakatifu anasema na kuongeza, kwa sababu tunatambua tayari kuwa katika Agano la Kale Mungu alikuwa ametoa amri kwa watu wake kupenda jirani kama wanavyo jipenda wenyewe (Walawi19,18). Yeyote aliyekuwa akimwomba Yesu ni amri gani katika Sheria, Yeye alikuwa akijibu kuwa ya kwanza ni “kumpenda Mungu kwa moyo wote” na ya pili ni “kumpenda jirani kama unavyojipenda nafsi yako” (Mt 22,38-39).

Je ni jipya gani la Amri ambayo Yesu anawakabidhi wafuasi wake?

Baba Mtakatifu akiendelea anaulizwa maswali kuwa: kwa maana hiyo ni  jipya gani la amri ambayo Yesu anawakabidhi wafuasi wake? Na kwa sababu gani anaiita “ amri mpya”? kwa kujibu mesema: Amri ya zamani ya upendo imegeuka kuwa mpya kwa sababu ilipata utimilifu na kuongezwa kwa neno hili “ kama nilivyo wapenda ninyi” nanyi pendaneni vivyo hivyo”. Kwa njia hiyo  upya upo katika upendo wote wa Yesu Kristo, upendo ambao yeye alitoa maisha yake kwa ajili yetu. Huo ndiyo pendo wa Mungu kwa ulimwengu mzima bila masharti na bila kikwazo,mbao unapatikana katika ncha ya msalaba.

Ni katika kipindi cha kuinama, Baba Mtakatifu anasisitiza, ni katika kipindi cha kujikabidhi kwa Baba, Mwana wa Mungu alijionesha na kutoa utimilifu wa upendo katika dunia hii. Kwa kufikiria mateso na uchungu wa Kristo, wafuasi wake walielewa maana ya maneno yake ya: “kama mimi nilivyo wapenda ninyi, ndivyo hivyo nanyi mpendane ninyi kwa ninyi”.

Yesu alitupenda akiwa wa kwanza

Yesu alitupenda akiwa wa kwanza, alitupenda licha ya udhaifu wetu, vizingiti vyetu na udhaifu wetu kibindamu. Ni yeye aliyetufanya tuwe na hadhi ya upendo wake ambao haujuhi mipaka na ambao haishi kamwe. Kwa kutupatia amri mpya Yeye anaomba sisi tupendane kati yetu na si tu kwa ajili ya upendo wetu, bali kupenda kwa upendo wake na ambao ni Roho Mtakatifu anayeingia ndani ya mioyo yetu iwao tunaomba kwa imani. Ni kwa namna hiyo tu sisi tunaweza kupendana kati yetu na siyo tu kwa jinsi tunavyopenda sisi wenyewe, bali kama Yeye  alivyotupenda, yaani kwa kina zaidi. Kwa hakika Mungu anatupenda sana kuliko sisi tunavyojipenda, amesisitiza Baba Mtakatifu!

Upendo wake unatufanya kuwa watu wapya na kuwa na upeo wa matumaini

Na kwa namna hiyo tunaweza kueneza kila mahali mbegu ya upendo ambayo inapayaisha uhusiano kati ya watu na kufungua upeo wa matumaini. Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa Yesu daima anafungua upeo wa matumani na upendo wake unafungua upeo wa matumaini. Upendo huo unatufanya kuwa watu wapya yaani ndugu kaka na dada katika Bwana na kutufanya kuwa watu wa Mungu yaani Kanisa, ambalo wote tunaalikwa kupenda Kristo na kupendana sisi kwa sisi. Upendo uliojionesha katika msalaba wa Kristo na ndiyo Yeye anatualika kuuishi, na ndiyo moja ya nguvu ambayo inabadili mioyo yetu migumu kama mawe ili iweze kuwa ya nyama; moja ya nguvu yenye uwezo wa kubadili mioyo yetu ni upendo wa Yesu,lakini   iwapo na sisi tunapenda kwa moyo huo. Na upendo huo unatufanya kuwa na uwezo wa kupenda maadui na kuwasamehe wanaotukosea.

Maswali ya kujibu kila mmoja katika nafsi yake: je una uwezo wa kumpenda adui?

Baba Mtakatifu Francisko ameuliza swali na kuomba kila mmoja ajibu ndani ya moyo wake: Je mimi ninauwezo wa kupenda adui? Sisi sote tuna watu, lakini hatujuhi kama ni marafiki, lakini watu hao hawaelewani na sisi ambao tupo upande mwingine; au mwingine anaye mtu ambaye alimtendea mabaya… Je mimi ninao uwezo wa kupenda yule mtu? yule mwanaume , au yule mwanamke aliyenitenda mabaya? Ninao uwezo wa kumsamehe?  Baba Mtakatifu amerudia kusema: "kila mmoja ajibu maswali hayo katika moyo binafsi. Upendo wa Yesu unatufanya kumtazama mwingine kama mshiriki wa sasa au wa wakati ujao katika jumuiya ya marafiki wa Yesu; ushiriki unaotoa chachu ya mazungumzo na kutusaidia kusikilizana na  kujitambua kwa pamoja.

Upendo unajifungua kwa mwingine

Upendo unajifungulia kwa mwingine, na kugeuka kuwa msingi wa mahusiano ya kibinadamu amesema Baba Mtakatifu Francisko. Unatuwezesha kushinda vizingiti binafsi na hukumu zisizo na maana. Upendo wa Yesu kwetu sisi unajenga madaraja, unafundisha njia mpya na kusuka muungano wa kindugu. Naye Bikira Maria atusaidie kwa njia ya maombezi  yake ya kimama  ili  tuweze kupokea kutoka kwa Mwanae Yesu Kristo zawadi ya amri yake na nguvu ya Roho Mtakatifu ya kuweza kujikita katika maisha ya kila siku.

 

19 May 2019, 14:26