Tafuta

Vatican News
Mara baada ya Misa Takatifu huko Mcedonia ya Kaskazini, Baba Mtakatifu ametoa shukrani Mara baada ya Misa Takatifu huko Mcedonia ya Kaskazini, Baba Mtakatifu ametoa shukrani   (Vatican Media)

Hija ya kitume:Shukrani za mwisho:Mungu atawakirimia!

Mara baada ya misa Takatifu, Baba Mtakatifu akiwa katika uwanja wa Macendonia ametoa shukrani zake kuanzia kwa Askofu wa Jimbo la Skopje, mapadre,watawa na waamini walei na viongozi wa nchi na watu wa kujitolea kwa kufanikisha siku hii.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Misa Takatifu huko Skopje katika uwanja wa Macendonia ametoa shukrani zake kuanzia kwa Askofu wa Jimbo la Skopje kwa maneno yake na hasa kwa ajili ya kazi iliyofanyika kuandaa siku hiyo. Pamoja na yeye amechukua fursa ya kuwashukuru wote walioshiriki yaani, mapadre, watawa na waamini walei. Anawashukuru kwa moyo wote.

Anawashukuru hawa viongozi wakuu wa nchi na vikosi mbalimbali

Aidha baba Mtakatifu  amependa kupyaisha utambuzi wake na shukurani  hata kwa viongozi wote wakuu nchi, vikosi mbalimbali vya ulinzi na watu wa kujitolea. Baba Mtakatifu anasema kuwa “Bwana atatambua namna ya kuwakirimia”. Kwa upande wake,ameahidi kuwaweka katika sala zake, pia wao wasali kwa ajili yake!

07 May 2019, 13:40