Tafuta

Vatican News
Tarehe 7 Mei Baba Mtakatifu Francisko akiwa katika mkutano wa Kiekumene na kidini na vijana huko Macedonia Kaskazini Tarehe 7 Mei Baba Mtakatifu Francisko akiwa katika mkutano wa Kiekumene na kidini na vijana huko Macedonia Kaskazini  (Vatican Media)

Hija ya kitume:Vijana oteni ndoto na kuthubutu kama Mama Teresa!

Wakati wa mkutano wa kiekumene na kidini na vijana wa Macedonia ya Kaskazini,Baba Mtakatifu amewashauri kuwa wema kutazamana uso kwa uso kwa wote,zaidi kwa babu zao.Ametoa onyo kali dhidi ya ukoloni wa kiitakadi na kuwaelekeza vijana wawe na ujasiri wa kutazama wakati endelevu kwa mfano wa Mama Teresa.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Ni baba Mwema Francisko aliyekutana kwa tabasamu na vichekesho vijana wa Macedonia ya Kaskazini wa madhehebu yote ya kikristo na mengine, katika kituo cha kichungaji cha Skopje ikiwa ndiyo kituo cha mwisho wa ziara yake ya 29 ya kitume katika nchi hizi. "Haijawahi kuchelewa  katika kuota ndoto na hakuna umri wa kuota ndoto”, anasema Baba Mtakatifu Francisko na kwamba “moja ya matatizo ya vijana wengi leo hii wamepoteza uwezo wa kuota ndoto kidogo hata sana, lakini hawaoti”. Amethibitisha hayo  akijibu maswali ya vijana. "Iwapo mtu haoti ndoto, iwapo kijana haoti ndoto, nafasi hiyo inataliwa na malalamiko, kukata tamaa na huzuni. Hawa ni wale ambao wanafuata mawazo ya kulalamika! Huo ni ulaghai wa kukufanya huchukue njia potofu. Iwapo kila kitu utafikiri kimesimama na kupelea hapo, iwapo matatizo binafsi yanapiga kengele, matatizo ya kijamii hayapatiwi majibu, siyo vema kujiachia katika kushindwa, kwa maana huwezi kamwe kuota ndoto  na hivyo, Baba Mtakatifu Francisko anatola wito kutoka katika Wosia wa “Christus Vivit”.

Lazima  kutoa matumaini katika  dunia iliyo na uchovu

Kutoa matumaini katika dunia iliyochoka, pamoja na  wakristo wengine  na waslam, ndiyo ndoto ambayo Baba Mtakatifu Francisko amesisitizia huku akitaja ndoto akiwa na rafiki yake, Imam Mkuu wa Al-Azhar Ahmad Al-Tayyeb, ambaye amethibitisha kwa pamoja, walipendelea kuwa na msimamo mmoja wa  kutia sahini ya pamoja katika Hati ambayo inasema: imani lazima iwapeleke waamini kutazama ndugu wengine ambao tunapaswa kuwasaidia, kuwapenda bila kudanganywa na mambo binafsi, yasiyo kuwa na maana wala mshiko. Baba Mtakatifu amesema: “ninyi vijana mnapaswa kuota yaliyo makubwa. Katika dunia ambayo imechoka na imezeeka, dunia ambayo imegawanyika na utafikiri inapata faida kwa njia ya  kugawanya na kugawanyika zaidi na zaidi”. Kwa maana hiyo swali linakuja kutoka kwa Baba Mtakatifu: “je ni njia zipi kubwa za kuwajibika na kujitolea kila siku ili kuweza kuwa mafundi wa ndoto na wataalam wa matumaini?” kwa kutoa jibu anasema: Ndoto zinaweza kutusaidia kuendelea kuwa na uhakika wa kujua kwamba, ulimwengu mwingine unawezekana na kwamba, tunaitwa kuhusika ndani yake na kufanywa kuwa sehemu ya kazi yetu, kwa ahadi yetu na matendo yetu”.

Tunapaswa kuwa kama mafundi mawe wenye ujuzi wa kukata mawe na kutoa umbo zuri

 “Katika nchi hii kuna utamaduni mzuri, anathibitisha Baba Mtakatifu wa kuwa na  mafundi mawe, wenye ujuzi wa kukata mawe na kufanya kazi” kwa njia hiyo ni: “ lazima tufanye kama wasanii hao na kuwa na mawe mazuri ya ndoto zetu. Tunapaswa kuzifanyia kazi ndoto zetu".  Msanii wa  mawe huchukua jiwe mikononi mwake na huanza taratibu kulichonga na kulipatia muundo na  kulibadilisha, kwa kulitumia na jitihada, hasa kwa shauku kubwa ya kuliona jiwe hilo, ambalo hakuna mtu angeweza kutoa kitu chochote na linakuwa kazi ya kisanaa.

Baba Mtakatifu anawashauri wasiwe na woga kuwa mafundi wa kuota ndoto na matumaini

Msiwe na hofu ya kuwa mafundi wa kuota ndoto na kuwa na matumaini", ndiyo wito wa Baba Mtakatifu alio rudia kupendekeza kwa vijana ambapo ujumbe huo unaonekana tayari katika Wosia wa “Christus Vitit”. “Ndoto nzuri zaidi zinapatikana kwa njia ya matumaini, uvumilivu na jitahada kwa kujizuia kutaka kwa haraka”. Wakati huo huo, hatupaswi kukwama kutokana na usalama, hatupaswi kuogopa hatari na kufanya makosa. Badala yake tunapaswa kuwa na hofu ya kuishi kama vile watu waliopooza, wafu wanaoishi na wanao pungukiwa kwa sababu hawataki kujihatarisha, na kijana hasiye thubutu amekufa”. Hawataki hatari kwa sababu hawataki kufanya ahadi zao au wanaogopa kufanya makosa. Hata kama  unakosea, Baba Mtakatifu anabainisha kuwa: unaweza daima kuinua kichwa chako na kuanza kwa upya, kwa sababu hakuna mtu mwenye haki ya kuiba tumaini lako”, amesisitiza Baba Mtakatifu kwa vijana hawa!

 

08 May 2019, 09:00