Tafuta

Unahitajika utamaduni ambao unatambua kila sura hata ile ndogo ya uso wa Yesu:"anayempokea mdogo kama huyo kwa jina langu ananipokea mimi". Unahitajika utamaduni ambao unatambua kila sura hata ile ndogo ya uso wa Yesu:"anayempokea mdogo kama huyo kwa jina langu ananipokea mimi". 

Baba Mtakatifu:Tunahitaji utamaduni unaotambua kila sura ya udogo kama Yesu!

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wakuu,wahudumu na watoto wa Taasisi ya Innocent huko Firenze.Hii ni taasisi inayotoa huduma tangu miaka 600 iliyopita kwa kukaribisha,kuwasaidia na kuhamasisha utoto.Unahitajika utamaduni ambao unatambua kila sura hata ile ndogo ya uso wa Yesu:"anayempokea mdogo kama huyo kwa jina langu ananipokea mimi".

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Tarehe 24 Mei 2019, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wajumbe wa Taasisi ya Hospitali ya Innocent huko Firenze Italia ambapo amewakaribisha  wakuu na wahusika wa hospitali hiyo wakiwa pamoja na watoto ambao anasema ndiyo wako mstari wa mbele katika taasisi hiyo ambayo kwa miaka 600, taasisi hiyo imewapokea na kuhamasisha utoto. Baba Mtakatifu hakusoma hotuba aliyoiandaa bali amewakabidhi ili wajisomeee na kupendelea kuzungumza nao kawaida. Katika hotuba aliyo wakabidha Baba Mtakatifu Francisko amekumbuka ziara yhake ya kitume huko Firenze kunako 2015 katika fursa ya Kongamano la kikanisa nchini Italia wakati akizungumza juu ya mji na kwamba hakuweza kusahau kuwa mji ule umeweza kuwapo vile hata kwa njia ya upendo akitajia Hospitali ya Inocenti kama mfano. Na alikumbusha  kuwa moja ya tabia ya kukua kwa mji na kuulinda ni kwa njia ya huduma ya watoto wanaliokuwa wameachwa na mama wengi waliokuwa wanasumbuka (Hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko katika Kongamano la tano la Kikanisa Firenze 10 Novemba 2015).

Miaka 600 ya mapokezi wa watoto

Ni miaka 600 Taasisi ya Innocent inajikita katika kusaidia watoto kwa kila mahitaji ili kukua kwa hadhi. Kiukweli leo hii ni lazima kusema kwa nguvu kuhusu maskini, kwa viumbe wadhaifu, anayeishi pembezoni ili kujitoa kwa kile tulicho nacho. Na kati ya watu walio wadhaifu ambao tunapaswa kuwatunza kuna watoto wengi waliotelekezwa, walio ibiwa udogo wao na wakati wao endelevu. Wadogo ambao wanakabiliana na safari nguvu ili kukimbia njaa au vita.

Watoto ambao hawaoni mwanga kwa sababu mama zao wanaishi hali mbaya kiuchumi, kijamii, kiutamaduni, hadi kufikia kushindwa kutoa mtoto katika mwanga wa ajabu. Ni mahitaji mangapi baba Mtakatifu Francisko anasema ambayo yanahitajika na utamaduni ambao unapaswa kujua thamani ya maisha, hasa kwa wale wadhatifu, walio hatarini. Wasio kuwa na ulinzi, badala ya kufikiria kuwaweka pembeni na kuwabagua huku wakijenga kuta na kujifungia binafsi, ikawa kuwaangaikia na kutoa utunzaji na uzuri! Unahitajika utamaduni ambao unatambua kila sura hata ile ndogo ya uso wa Yesu kwa maana “anayempokea hata mdogo kama huyo kwa jina langu ananipokea mimi” (Mt 18,5).

Taasisi hiyo ni sehemu ya historia ndogo na kubwa ya kushangaza

Baba Mtakatifu anasema kuwa taasisi ya Innocent ni sehemu ya historia, lakini hata historia ndogo zaidi,na za kushangaza zaidi. Ni historia ya mamia elfu ya watoto ambao wamepitia katika kuta zile. Akikumbuka wakati wa hotuba yake wakati wa kongamano Firenze, amekumbusha jinsi alivyotaja mantiki maalumu hasa ile ya wa mama ambao walikuwa wakiacha watoto wao wamewavalisha medali iliyo nusu kwa matumaini ya kuweza kuwatambua watoto wao wakati wakiwa na wakati mzuri. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anasema, lazima kuwafikia maskini hao kama vile waliovaa nusu medali. “Na sisi tunayo medali nusu. Kwa sababu Kanisa ni Mama ambalo linabeba Italia likiwa na nusu medali ya watoto na inatambua watoto wote walioachwa na walioelemewa.

Lengo hasa leo hii la kufanya kwa kila ngazi zote za wahusika pasiwepo mama hata mmoja wa kuweza kumtupa mtoto wake. Badala yake tunapaswa kufanya kila njia ya kukabiliana na tukio hili la kutisha, na ambalo linaweza kutengenisha watoto na wazazi wao. Baba Mtakatifu anashauri kuwa yawepo majengo na michakato ya kupokea na watoto walindwe na kutunzwa kwa namna ya hadhi, kwa kuwapatia watoto hali bora kwa ajili yao. Kwa kukumbuka maneno ya Yesu ambaye anatualika kugeuka wote kuwa watoto ili kuweza kuingia katika ufalme wa Mbingu. Katika Taasisis inatufundisha historia ya mchanganyiko na maelfu ya wageni waliopitia hapo na historia ambayo leo hii watoto wako pamoja na tabasamu zao. Amewashukuru na kwa huduma yao ya ukarimu, upole na upendo, taaluma na kujitoa, amawabariki.

24 May 2019, 13:30