Baba Mtakatifu na PIME:Uinjilishaji ni ushuhuda na ndiyo uwe kitovu!
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Tarehe 20 Mei 2019 Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Taasisi ya Kipapa ya Utume wa Kimisionari wa Nje kwa jina wanajulikana PIME. Ni katika fursa ya mkutano Mkuu wa XV wa mwaka ambao ulianza tangu tarehe 28 Aprili na utahitimishwa tarehe 23 Mei 2019 katika Kituo cha Kimataifa cha uhamasishaji wa kimisionari (CIAM), Roma. Katika hotuba yake Baba Mtakatifu amesema kwamba, anakutana nao wakiwa katika fursa ya mkutano wao. Anamshukuru Mkuu wa PIME na wamisionari wote. Anamshukuru Bwana kwa safari ndefu ambayo wamefanya kwa ajili ya Taasisi yao na karibu kwa miaka 170 tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo huko Milano Italia, ulipoanza kama seminari ya Umisionari wa Nje. Anamkumbuka kiongozi aliye kuwa mstari wa mbele, Askofu Angelo Ramazzotti aliyekuwa wa jimbo la Pavia Italia. Yeye aliupokea kwa ukarimu na shauku wito wa Papa Pio IX na kuwa na furaha ya kushirikisha wazo lake la kuanzishwa chombo hiki kwa maaskofu wa Mkoa wa Lombardia katika misingi ya uwajibikaji wa majimbo yote kwa ajili ya kueneza Injili kwa watu ambao walikuwa bado hawajuhi Yesu Kristo.
Nyakati zile zilikuwa ni habari mpya; Wamisionari wa PIME
Nyakati zile Baba Mtakatifu Francisko amesema, ilikuwa ni habari mpya iliyo tanguliwa na kuanzishwa kwa Taasisi ya Utume wa Nje wa Paris. Hadi wakati ule,utume wa kimisionari ulikuwa mikononi mwa Mashirika ya kitawa tu. Na kwa njia ya Taasisi za Paris na Milano pamoja walianza kuwajibika katika Makanisa maalum ambayo yalikuwa yanajikita katika kujifungulia duniani kote na kuwatuma mapadre katika kila kona ya dunia. Kadri miaka ilivyopita, PIME imeweza kujitegemea na kwa upande mwingine imeendelea kujikita katika huduma kama vile mashirika mengine ya kitawa japokuwa bila kujichanganyanya. Baba Mtakatifu akitoa ufafanuzi kuhusu wamisionari wa PIME amesema: kwa hakika wao hawafungi nadhiri kama watawa wengine, lakini wanawekwa wakfu katika maisha yao yote kwa kujikita katika shughuli za kimisionari na nadhiri ya milele. Na kambi zao za kwanza za kimisionari, zilikuwa huko Pacific, India, Bangladesh, Myanmar, Hong Kong China. Mbegu iliyo fichika chini ya ardhi imeweza kuzaa matunda mengi na mapya ya jumuiya, kama pia majimbo yaliyo anzishwa bila kuwa na kitu, miito ya mapadre na watawa ambao wanaendelea kutoa huduma ya Kanisa mahalia. Baada ya vita ya Pili ya Dunia, wao waliweza kupanua wigo wao hadi nchini Brazil na Amazoni, Marekani, Japan, Guinea-Bissau, Ufilippini, Camerun, Ivory Cost, Thailand, Cambodia, Papua New Guinea, Mexico, Algeria Chad.
Wapo Watakatifu wafiadini na wenye heri wa PIME
Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa, historia yao inajikita katika mwanga wa utakatifu kwa wanachama wengi wa PIME ambao wanajulikana rasmi na Kanisa. Akiwataja ni wafiadini kama vile Mtakatifu Alberico Crescitelli, Mwenyeheri Giovanni Battista Mazzucconi, Mwenyeheri Mario Vergara; na waungamishi Mwenyeheri Paolo Manna na Mwenyeheri Clemente Vismara. Aidha ameongeza kusema kwamba, kati yao wamisionari wapo wafiadini 19 ambao walitoa maisha kwa Yesu kwa ajili ya watu wao, bila kujibakiza na bila kuhesabu. Wao ni familia ya mitume, jumuiya ya kimataifa ya mapadre na walei ambao wanaishi na muungano wa maisha na huduma. Maneno ya Mtakatifu Paulo VI alisema akiwa huko Manila kunako mwaka 1970, yanatoa mwangwi kwao kwa namna ya pekee katika maana ya maisha yao na maisha ya wito wao! Yeye alisema kuwa: “Iwapo mimi ninahisi ulazima wa kutangaza Yesu Kristo, siwezi kunyamaza (…). Mimi lazima nikiri jina lake: Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai (…) Sitoweza kamwe kumalizia kuzungumza juu yake: Yeye ni mwanga, ni ukweli, (…) Yeye ni Mkate ni kisima cha maji kwa ajili ya njaa zetu na kwa ajili ya kiu zetu; Yeye ni Mchungaji, kiongozi wetu, mfano wetu, nguvu yetu, ndugu yetu”. Baba Mtakatifu ameongeza kusema, kwa namna alivyo sema Papa Paulo VI kwa hakika ni kutoka kwa Yesu Kristo tunapata maana ya maisha na utume wetu kwa sababu hakuna uinjilishaji wa kweli iwapo hakuna tangazo la jina lake , mafundisho,ahadi ya maisha , Ufalme, utume wa Yesu wa Nazareth na Mwana wa Mungu, (Esort. ap. Evangelii nuntiandi, 22).
Kuinjilisha ni neema na wito wa Taasisi ya PIME;hakuna shule ya uinjilishaji
Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kwamba kuinjilisha ni neema na wito wake wa Taasisi ya PIME na utambulisho wa kina zaidi. Utume huo lakini lazima na daima kuusisitizia kuwa siyo wa kwao, kwa sababu wito wenyewe unatokana na neema ya Mungu. Hakuna shule ya kujifunxa kuwa mwinjilishaji. Kuna masaada, lakini hakuna kitu kingine: Ni wito ambao wameupokea kutoka kwa Mungu kwa maana hiyo unaweza kuwa au huwezi kuwa mwinjilishaji, au kama hukupokea neema ya wito huo ubaki nyumbani. Hili ni jambo kubwa ambalo linakupeleka mbele. Baba Mtakatifu amethibitisha. Kuanzishwa kwa utume wa shughuli hiyo kwanza unatokana na Mungu na kwa kujikita katika shughuli hii ya Mungu na kuomba kutoka kwake, inawezekana, hata wao kugeuka kuwa kama Yeye katika Yeye, kwa njia ya uinjilishaji (Esort. ap. Evangelii gaudium, 112).
Waraka wa Kitume wa Maximum Illud unatimiza miaka 100 mwaka huu
Baba Mtakatifu Francisko aidha amekumbusha kuwa mwaka huu Waraka wa Kitume wa Maximum Illud wa Papa Benedikto XV unatimiza miaka 100. Na kama wanavyotambua katika maadhimisho ya tukio hili, yanakwenda sambamba na Mwezi Maalum wa Kimisionari Oktoba 2019 kwa kuongozwa na tema:"Tumebatizwa na kutumwa; Kanisa la Kristo katika utume duniani”. Lengo kuu la kuanzishwa kwake ni kutoa uamsho kwa kiasi kikubwa juu ya utambuzi wa Missio ad gentes na kujikita kwa upya uamsho wa mapinduzi ya kimisionari katika maisha na ya kichungaji (Barua kuhusu tukio hili, 22 Oktoba 2017). Hatari hivyo Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kwamba kuna hatari inayorudi kuchomoza, na ambayo utafikiri ilikuwa imekwisha lakini inarudi kuchomoza tena; hatari hii ni ile ya kuchanganya uinjilishaji na propaganda. Baba Mtakatifu Francisko amewasihi sana kwamba wasichanganye, kwa maana Uinjilishaiji ni ushuhda wa Kristo Yesu, aliyekufa na kufufuka. Yeye ndiye anashamiri na kwa sababu hiyo Kanisa linakua kwa ajili ya kushamiri kwake lakini si katik kufanya propaganda,na hiyo alikuwa amesema hata Papa Benedikto XVI amethibtisha Baba Mtakatifu Francisko. Lakini mchanganyo huo kidogo umezaliwa kutokana na uelewa wa kisiasa na kiuchumi katika uinjilishaji japokuwa kwa hakika siyo uinjilishaji. Aidha amebainsha kuwa iwapo unaulizwa kwanini huko hivi. Jibu la kuwambia ni kwamba ni Yesu Kristo! Usitafuta wanachama wapya katika jamii hii katoliki, hapana , bali wewe uwafanya watazame Yesu na Yeye anajionesha katika nafsi yetu, katika mwenendo wetu; kujifungulia maisha yetu na kumpa nafasi Yesu. Huo ndiyo uinjilishaji Baba Mtakatifu anasisitiza na kuongeza: huo ndiyo mtindo walio kuwa nao moyoni waanzilishi wao.
Wamisionari wa PIME ndiyo wako mstari wa mbele wa mwamko wa ad gentes
Akiendelea Baba Mtakatifu Francisko amesema wao kama wamisionari ndiyo wako mstari wa mbele wa tukio hili la mwezi wa kimisionari ili liweze kuwa fursa ya kupyaisha mwamko wa kimisionari wa ad gentes, hivyo kwa ajili ya maisha yao yote, mipango yao yote, kazi yao, hata majengo yao yaliyopo katika utume na kutaka kutangaza Injili kiini cha maisha na mantiki ya dhana hiyo. Kwa hakika katika mantiki ya maandalizi ya Mwezi Maalum, wao wameunganisha kwa ajili ya Mkutano wao Mkuu wa XV, kwa kuongozwa na tema “ ole wangu nisipo tangaza Injili: watu, mahali na mitindo ya utume wa PIME wa leo na kesho”. Hii ina maana ya kutafuta kadiri ya uwezekano wao kwamba utume wao uwe kitovu, kwa sababu ndiyo dharura ya umisionari ambao umeanzishwa na Taasisi yao na kuendelea kuundwa. Wao wanaamini hili na wakachagua kielelezo cha Mtakatifu Paulo asemaye: Ole wangu nisipo tangaza Injili (19,16) kama kingozi na wa kuiga. Upendo na dharura kwa ajili ya utume, ambao Mtakatifu Paulo alikuwa anahidi kama utume wake, ndiyo matashi yao pia kwa ajili ya wote. Na zaidi kama mwanga wa Neno hili lenye ufunguo, wao wamefanya kazi ya kuelewa kwa upya, katika Taasisi yao na katika dunia ya sasa, utume wa ad gentes; ili kuthibitisha ukuu wa wito mmoja wa kimisionari ambao uwe kwa walei na kwa makleri; kuchagua mantiki za kimisionari; kuweza kuunda namna ya kuhamasisha miito kama shughuli za kimisionari; kuhakikisha namna yao ya kuwa jumuiya na kufikiria kwa upya namna ya kupangilia PIME ya leo na endelevu.
Tusiogope kuanza kwa upya na kuchagua umisionari wenye uwezo wa kuleta mapinduzi
Kutokana na hiyo, Baba Mtakatifu amewambia: “tusiogope kuanza kwa upya na katika matumaini kwa Mungu na kwa ujasiri mkubwa, kuchagua umisionari, wenye uwezo wa kuleta mapinduzi ya kila kitu, na ili ukawaida, mtindo, masaa, lugha na kila aina ya muundo wa kikanisa uweze kugeukw kuwa mkondo unaofaa kwa ajili ya uijilishaji katika dunia ya sasa. (Barua kuhusu mwezi maalum wa kimisionario 2019). Baba Mtakatifu amehitimisha aliwashukuru tena kwa ajili ya mkutano huo na zaidi katika kazi yao ya huduma ya Injili. Kwa njia ya maombezi ya Bikira Maria, Bwana awawezeshe kufanya kazi hiyo kwa furaha daima na katika ugumu. Na hiyo imempa fursa ya kuwakumbusha watazama kuraza za mwisho katika Waraka wa Evangelii nuntiandi . Na kwamba wao wanatambua kuwa Evangelii nuntiandi ni Waraka wa kichungaji ulio mkubwa baada ya Mtaguso: Na bado ni wa karibu na zaidi unatoa angalisho kwa maana haujapoteza nguvu yake. Katika kurasa za mwisho mahali ambapo wanaandika ni kwa jinsi gani mwinjilishaji anapaswa kuwa: furaha ya ujinilishaji; ni mahali ambapo Mtakatifu Paulo anapozungumza juu ya dhambi za mwinjilishaji: namba nne na tano katika kurasa za mwisho, Baba Mtakatifu ameshauri kusoma vizuri, kwa kufikirika furaha ambayo inasahuriwa. Amewabariki na kuomba wamkumbuke katika sala zao!