Tafuta

Vatican News
Tarehe 20 Mei Baba Mtakatifu Francisko akihutubia maaskofu wa Italia wakati wa  ufunguzi wa Mkutano wao wa 73 wa mwaka mjini Vatican Tarehe 20 Mei Baba Mtakatifu Francisko akihutubia maaskofu wa Italia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wao wa 73 wa mwaka mjini Vatican   (ANSA)

Baba Mtakatifu na CEI:Maaskofu wawe karibu na mapadre na watu wa Mungu!

Upamoja na baraza,mchakato wa kubatilishwa ndoa na uhusiano kati ya maaskofu na mapadre wao,ndizo mada kuu ambazo Baba Mtakatifu Francisko amewaelekeza maaskofu wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 73 wa Baraza la Maaskofu Italia uliofunguliwa tarehe 20 na utahitimishwa 23 Mei 2019 mjini Vatican.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake bila kusoma tarehe 20 Mei 2019 ameshukuru kupewa nafasi ya kuzungumza katika Mkutano, mbapo ameonesha shauku yake kwamba Mkutano huo uwe labda mwafaka wa kufanya mang’amuzi ya kichungaji katika maisha  na utume wa Kanisa la Italia. Upamoja na baraza; mageuzi ya mchakato wa kubatilisha ndoa; uhusiano kati ya maakofu na makuhani. Ndiyo mada kuu msingi na miongozo ambayo Baba Mtakatifu Francisko ameelekeza maaskofu kuifuata wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 73 wa Baraza la Maaskofu nchini Italia unaoongozwa na tema: “mbinu na zana za uwepo mpya wa wamisionari”;  ni katika mkutano ambao utafungwa tarehe 23 Mei 2019. Baba Mtakatifu Francisko anawashukuru maaskofu kwa juhudi zao za kila siku katika  kupeleka mbele utume wao wakati  huo wakikabiliana na baadhi ya masuala nyeti katika wakati endelevu wa Kanisa la Italia  hasa kuanzia na uhusiano kati ya maaskofu kati yao na waamini!

Upamoja na baraza

Tema ya “upamoja” na “baraza” kwa upande wa Baba Mtakatifu anasisitiza kwamba ndiyo kitambulisho cha Kliniki ya afya ya Kanisa la Italia na katika huduma yake ya kichungaji na ya kikanisa. Kwa maana hiyo, kwa  kutambua kwa ngazi ya ushiriki wa Watu wote wa Mungu katika maisha na katika utume wa Kanisa na ushirikiano wa maaaskofu kati yao, katika umbu la umoja na Kanisa lote la ulimwengu la Kristo, ndiyo mantiki muhimu kwa mtazamo wa uwezekano wa kufanya Sinodi kwa ajili ya Kanisa la Italia. Baba Mtakatifu Francisko akifafanua zaidi anasema: ili kuweza kufanya Sinodi kubwa, lazima kuanzia na upamoja yaani baraza  dogo la chini kwa  maana ya kuwahusisha majimbo, maparokia na walei kama njia ya upamoja kama alivyokuwa amethibitisha hata huko Firenze kunako mwaka 2005.  Lakini hiyo anasema, itachukua muda japokuwa  itakuwa ni njia ya utembea kwa uhakika na  wala siyo mawazo tu.

Mageuzi ya mchakato wa kubatilisha ndoa

Hata hiyo Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na hotuba yake, amerudi kugusia juu ya utekelezaji wa mchakato wa kubatilishwa ndoa kama unavyo elekezwa kwa Waraka wake wa  na Motu Proprio ya mwaka 2015 ( Mitis Iudex Dominus Iesus na Mitis et Misericors Iesus ) hizi ni nyaraka mbili  ambazo zinagusa kwa undani Mafundisho tanzu ya Kanisa kuhusu Ndoa na neema na baraka inayotolewa na Sakramenti hii kwa wanandoa. Inahusu michakato hiyo na kuonesha wazo kwa namna yakuweza kujikita katika  kesi ambazo zinaonesha kubatilishwa. Hata hivyo katika michakato hiyo ni kutaka kuoneshaKanisa kuwa na msimamo mmoja kwa kuzingatia kwamba, Sakramenti ya Ndoa inaweka madhubuti fungamano la kudumu na la pekee kati ya wanaharusi. Kwa maana hiyo michakato mifupi na ina uwezekano wa kuelekea Askofu. Baba Mtakatifu amesema Mageuzi haya ya mchakato kiutaratibu yanajikita juu ya ukaribu na juu ya kutoa msamaha wa bure.Ukaribu wa familia zilizo jeruhiwa  ambazo zipo katika hukumu, na kama inavyo wezekana, zifanyika  katika Jimbo na bila kuchelewa na bila kukaa muda mrefu usio kuwa na maana.

Kutoa bure kunaamanisha juu ya utubitisho kwa mujibu wa kiinjili unayosema, utoe bure kwa maana tumepewa bure, hivyo inahitaji utangazaji wa Kanisa juu ya kubatilisha na ambapo hakuhitaji gharama kubwa ambayo watu masikini hawawezi kuifikia, Anasema Baba Mtakatifu. Hata hivyo Baba Mtakatifu Francisko ameonesha masikitiko yake kuhusiana na Mageuzi hayo tangu kutangazwa kwake miaka minne iliyopita, na kwamba, bado inaonesha hatua hiyo kuwa mbali katika matendo hasa katika sehemu kubwa za majimbo ya Italia.  Msukumo wa mageuzi anasema, “unaonesha kuwa Kanisa ni mama na lenye moyo kwa ajili ya wema wa watoto wake hasa wale ambao wamejeruhiwa na upendo uliovunjika”. Mafanikio ya mageuzi kwa mujibu wa Baba Mtakatifu Francisko anasema  ni kupitia katika uongofu wa miundo na watu,na zaidi anaonya: “Tusiruhusu maslahi ya kiuchumi kwa baadhi ya wanasheria wengine au kwamba hofu ya kupoteza nguvu ya baadhi ya Vika wa Mahakama katika kusimamisha au au kuchelewesha mageuzi hayo”.

Uhusiano kati ya maaskofu na mapadre

Mada ya tatu ambayo Baba Mtakatifu Francisko amejikita nayo ni kuhusu uangalizi wa maaskofu ambao wanapaswa kuwa nao mbele ya mapadre wao, na ambao wanapaswa wawe bila “ubaguzi na upendeleo”. Kwa mujibu wa Baba Mtakatifu amesema baadhi ya maaskofu wanakuwa na ugumu wa kudumisha uhusiano unaokubalika na kwa maana hiyo huhatarisha na kuharibi utume wao, hata kudhoofisha kazi ya Kanisa. Kutokana na hiyo, Baba Mtakatifu Francisko anasisitiza kuwa, uhusiano kati ya maaskofu na mapdre wao unapaswa kutegemea juu ya upendo usio na masharti ulio shuhudiwa na Yesu msalabani, unaowakilisha kanuni ya kweli  na  ya kitabia. Utawala wa  juu  anasisitiza unaanguka  iwapo unaambukizwa na kila mtindo wa madaraka au kujifurahisha kibinafsi japokuwa  kinyume chake, unaimarishwa na kukua wakati unapokumbatiwa na roho ya kujiachia kwa jumla na huduma kwa watu wa Mungu”.

Tusiangukie katika kishawishi cha kuwakaribia mapadre ambao labda ni wachangamfu na kuwahepuka wale ambao, kwa mujibu wa askofu, hawapendi na hawakubali; kuwapa majukumu yote kwa makuhani wenye kujitoa kwa haraka au wenye kimbele mbele na kukatisha tamaa makuhani vigeugeu, au wapole au wanyonge  na zaidi labda mapadre wenye matatizo. Kutokana na hiyo ni lazima askofu awe baba wa makuhani wote, kujihusisha na kuwatafuta wote; kuwatembelea wote; kujua namna ya kutafuta muda wa kuweza kwasikiliza mara moja wanapoomba au wanapokuwa na mahitaji: na ili kila mmoja ahisi kujali na kutiwa moyo na askofu wake. Na ili kufafanua juu ya hili , Baba Mtakatifu ametoa mfano: iwapo askofu anapokea simu kutoka kwa padre wake, lazima ajibu haraka siku hiyo,angalau hata siku inayofuata na kwa kufanya hivyo itamsaidia angalua padre huyo kujua kwamba anaye baba.

“Mkuhani wetu, anaendelea kusema,  wanahisi kuwa  chini ya mashambulizi ya vyombo vya habari na mara nyingi huchekwa, au kuhukumiwa kwa sababu ya makosa au uhalifu” uliofanywa na wengine yaani wenzao”. Kwa maana hiyo makuhani wanahitaji kupata kutoka kwa maaskofu wao mfano wa kaka yao na baba ambaye anawatia moyo katika kipindi kigumu: anawamotisha katika kukua kiroho na kibinadamu; anawatia moyo katika kipindi cha kushindwa, anawakosoa kwa upendo wanapokosea; anawatuliza wanapohisi upweke na  anawainua wanapo anguka. Lakini hiyo inahitaji awali ya yote ukaribu  kwa mapadre wetu, ambao wanahitaji kukuta mlango wa askofu uko wazi  na moyo wake umefunguka. Kuwa Askofu –baba – askofu kaka! . Amehitimisha kwa kusema amependa ashirikishane nao mada hizo tatu kama nyenzo ya tafakari. Na kwa muda huo amewachia walendelee, lakini amewashukuru kwa upya!

21 May 2019, 09:30