Tafuta

Vatican News
Maadhimisho ya misa Takatifu wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa XXI wa Caritas Internationalis katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro tarehe 23 Mei 2019 Maadhimisho ya misa Takatifu wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa XXI wa Caritas Internationalis katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro tarehe 23 Mei 2019  (Vatican Media)

Baba Mtakatifu kwa Caritas Internationalis:Ni muhimu kutazama wadogo na wadhaifu!

Katika mahubiri ya Baba Mtakatifu wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa XXI wa Caritas Internationalis amejikita kutazama jumuiya ya wakristo wa kwanza walivyoishi kwa mujibu wa Somo la Matendo ya mitume.Anahimiza watu wawe kitovu kabla ya mipango yote hasa wadogo na wadhaifu.Iwapo hatuwatazami moja kwa moja tunashia kujitazama sisi wenyewe kwa kujiinua wakati tuna watumia wengine.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 23 Mei 2019 majira ya saa 11.00 jioni masaa ya Ulaya, Baba Mtakatifu Francisko ameadhimisha misa Takatifu ikiwa ni ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa XXI wa Caritas Internationalis katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Katika mahubiri yake amejikita kutazama Neno la Mungu kutoka katika Somo la Matendo ya Mitume mahali  ambapo wanazungumzia juu ya mkutano wa kwanza wa historia ya Kanisa. Baba Mtakatifu amesema, walikuwa wamethibitisha hali fulani ambayo hawakuwa wanatarajia, yani wapagani kuwa na imani. Kwa maana hiyo ilitokea maswali hata katika kanuni sheria ya zamani. Ilikuwa ni maamuzi magumu ya kuchukua na wakati huo huo Bwana hakuwapo tena.

Kwa nini Yesu hakuwaachia ushauri? Anatuma Roho Mtakatifu na kuja kama  moto

Baba Mtakatifu  akiendelea anabainisha kuwa, ndipo unaweza kujiuliza kwa nini Yesu hakuwa amewacchia ushauri wa kuweza angalau kutoa wakati wa kuwa na  majadiliano makubwa (At 15,7)? Ingetosha tu maelekezo madogo kwa Mitume ambao kwa miaka kadhaa walikuwa wanashinda na yeye. Kwa nini Yesu hakuwa amewapatia kanuni zilizo wazi na na za haraka katika kutatua? Katika kujibu maswali hayo, Baba Mtakatifu anabinisha kwamba, ndipo kuna kishawaishi ya kujitosholeza, cha kufikiria kwamba mambo yote yanakuwa  sawa iwapo kuna kila kitu na kuthibiti. Iwapo Kanisa linaisha bila kutetemeka kuwa na ratiba daima isiyokuwa na tatizo na hata kishawishi cha kupembua mema na mabaya. Lakini Bwana hakufanya namna namna hiyo na kwa hakika kutoka mbinguni hakuwatumia watu wake majibu, anatuma Roho Mtakatifu.

Na Roho hakuja kuleta utaratibu wa siku, bali  anakuja kama moto. Yesu hataki kwamba Kanisa lile mfano kamilifu, unaopenda utaratibu wa binadamu na wenye uwezo wa kulinda jina lake binafsi. Kwa kuongeza Baba Mtakatifu amesema: “ni maskini yake makanisa maalum yanayoangaikia sana utaratibu, mipango na kutafuta kila njia ili kita kutu kiwe wazi na kuwa na mgawanyiko wa kila kitu…ninateseka juu ya hilo”! Lakini Baba Mtakatifu anathibitisha: Yesu hakuishi namna hiyo bali aliishi katika mwendo bila kuogopa mtetemeko wa maisha. Injili ndiyo mpango wa maisha, ndani mwake kuna kila kitu. Inatufundisha kuwa, masuala hayakabiliwi na orodha ya  mambo yaliyo tayari na kwamba, imani siyo barabara iliyo na orodha ya hatua, bali ni maisha (Mdo 9,2) ya kutembea kwa pamoja daima na kwa roho ya imani.  Kutokana na simulizi la Matendo ya mitume, Baba Mtakatifu anabainisha, kuwa tunapata mambo matatu msingi kwa ajili ya Kanisa katika safari. Kwanza ni unyenyekevu wa  kusikiliza pili karama ya pamoja na tatu  ujasiri wa kujikana.

Lazima kutembea haraka na kuwa wepesi japokuwa hata kwa gharama

Akianza kufafanua, Baba mtakatifu ameanza na jambo la mwisho yaani ujasiri wa kujikana na kwamba majadiliano makubwa hayakuwa ni kutaka kupendekeza jambo ambao jipya lakini ilikuwa ni hasa kuaha mambo ya zamani. Lakini wakristo wa kwanza hawakuweza kuacha mambo hivi bure. Zile zilikuwa ni tamaduni muhimu   za kidini na zilizo kuwa zinapendwa na watu wateule. Hata hivyo kulikuwa na mchezo wa utambulisho wa kidini. Japokuwa walichagua kutangaza Bwana ndiyo iwe  kipaumbelecha thamani zaidi kuliko kila kitu. Kwa ajili ya wema wa utume, kumtangazia kila mtu yeyote, kwa njia ya uwazi na wa kuaminika, kwamba Mungu ni upendo, hata imani hizo na tamaduni za kibinadamu ambazo ni zenye kikwazo zaidi kuliko msaada, inaweza na lazima ziachwe amethibtisha Baba Mtakatifu.

Ufafanuzi wa sehemu ya ujasiri wa kujikana: Hata sisi ni muhimu kujikana

Akifafanua juu ya umuhimu wa ujasiri wa kujikana: Hata Sisi Baba Mtakatifu Francisko amesema pia tunahitaji kugundua kwa upya pamoja uzuri wa kujikana, awali ya yote sisi wenyewe. Mtakatifu Petro anasema kwamba Bwana “alitakasa mioyo na imani” (rej Mdo 15: 9). Mungu hutakasa, Mungu hurahisisha, mara nyingi hutufanya kukua huku akiondoa kitu, bila kuongeza kama tunavyoweza kufanya sisi. Imani ya kweli hutakasa kutokana na kushikilia sana. Ili kumfuata Bwana ni lazima kwenda kwa haraka na kutembea haraka na mtu lazima awe mwepesi hata kama kuna gharama. Kama Kanisa Baba Mtakatifu amesema hatujaalikwa kwa ahadi kama makampuni, kwa mwamko wa kiinjili. Kwa kujitakasa wenyewa, katika kubadilika sisi wenyewe lazika kupeka kujiinua, yaani ni kujifanya kuwa inabadilisha kitu lakini kiukweli hakuna mabadiliko. Hii hutokeza kwa mfano wakati, unatafuta kubaki katika hatua kwa kipindi kitefu, kupaka kidogo vipodozi katika uso wa mambo lakini ni kufanya tu ili kuangalia utafikiri vijana. Bwana hataki marekebisho ya vipodozi, anataka uongofu wa moyo, ambao unapatia kwa njia ya kujikatalia. Kutoka nje ya nafsi ndiyo mageuzi  msingi.

Kusikiliza kwa unyenyekevu

Wakristo wa kwanza walifikiwa ujisiri wa kujikana kwa kuanzia katika  kusikiliza kwa unyenyekevu. Walifanya mazoezi hayo bila kutafuta maslahi binafsi. Kwa kutazama na kuacha mwingi azungumze ndiyo uwezekano wa mabadiliko ya kuamini. Anajua kusikiliza yule anayeacha sauti ya mwingine iweze kuingia kwa dhati ndani yake, kwa maana ya kumpatia usikivu mwingine. Iwapo wema wa wingine unakua, unaongeza hata ustawi binafsi kwa yule anayesikiliza anasema Baba Mtakatifu. Unakuwa mnyenyekevu kwa kufuata njia ya kusikiliza na ambayo inataka kuthibitisha, kupelekwa mbele mawazo na kutafuta njia ya kupata zana za mwingine. Unyenyevu unazaliwa zaidi ya kuzungumza hasa kwa kuiskiliza na iwapo unaacha kujiweka katika kitovu. Pia unyenyekvu unakuwa kwa njia hiyo. Barabara ya huduma ya unyenyekevu ndiyo aliyopitia Yesu. Na ndiyo barabara  ya upendo ambayo Roho anawasha na kuelekeza!

Ni muhimu kusikiliza walio wadogo na wa mwisho: Kusikiliza kwa maisha

Ni muhimi sana kusikiliza sauti ya wote hasa walio wadogo na wa mwisho. Katika dunia ambayo inazo zana nyingh zaidi na kuzungumza, lakini kati yetu hatuwezi kufanya hivyo kwani Mungu anapenda kujionesha kwa njia ya wadogo na wa mwisho. Paulo na Barba wanasimulia uzoefu na siyo mawazo. Kanisa linafanya mang’muzi yake kwa namna hiyo; siyo mbele ya komputa, bali mbele ya hali halisi ya watu. Wanajadiliana mawazo, lakini hali hizi zinafanyiwa mang’amuzi. Ni watu ambao wanazingatiwa kwanza kabla ya mipango kwa mtazamo wa unyenyekevu kwa yule anayetafuta wengine ule  uwepo wa Mungu na ambao unapatikana katika udogo wa masikini tunaokutana nao. Iwapo hatutazami moja kwa moja kwao, tunashia kujitazama sisi wenyewe kwa kujiinua wakati unawatumia wengine; baba Mtakatifu ameonya.

Katika unyenyekevu wa kusikiliza, ujasiri wa kujikana vyote hivyo vinapitia katika karama ya pamoja. Kwa hakika katika majadilianao ya Kanisa la kwanza umoja ndiyo unachukua hatua ya kwanza juu ya tofauti. Kila mmoja awe katika nafasi ya kwanza na hakuna anayependelea na mikakati bali kuwa na kuhisi Kanisa la Yesu wanao unganika pamoja na Petro katika upendo ambao hauna upendeleo na ufananisho bali umoja. Hakuna aliyekuwa anajua yote, hakuna aliyekuwa na dhana ya karama  bali kila mmoja alikuwa na karama ile ya pamoja.  Ni muhimu kwa sababu huwezi kutenda wma  bila kuwa na kuwa na utashi wa wema.

Kaeni katika upendo wangu ndiyo wito wa Yesu katika Injili

Kaeni ndani ya upendo wangu (Yh 15,9): ndiyo Yesu anaomba katika Injili. Ni kwa namna gani ya kufanya  ili kubaki karibu naye, mkate uliomegeka. Tunasaidiwa kukaa mbele ya taberkuli na mbele ya tabenakuli nyingi zilizo hai ambazo ni watu maskini. Ekaristi na masikini, ni tabenakuli milele na tebernalili zinzotembea. Pale ni kubaki katika upendo, ndiyo uwezo wa kuelewa hisia ya mkate unaomegeka. Ni kuelewa kwa dhati jinsi gani Yesu anasema “Kama Baba alivyonipenda mimi hata mimi nina wapenda ninyi. Je ni kwa jinsi gani Baba alimpenda Yesu? Ni kwa kumpatia kila kitu bila kubaki. Tunatamka hili katika sala ya Nasadiki “ Mungu kutoka kwa Mungu, mwanga kwa mwanga “ alimpatia kila kitu. Badala yake tunaposhikilia bila kutoa, kwa ajili ya maslahi yetu, hatuwezi kuiga jinsi Mungu, alivyojitoa kwetu bure na kwa Kanisa na kwa uhuru. Yesu anaomba kubaki ndani yake, siyo katika mawazo yetu; kutoka nje ya udanganyifu wa kudhibiti na kujisimamia ; anatuomba tuwe na matumaini kwa wengine na kujitoa kwa wengine!

24 May 2019, 09:42