Tafuta

Vatican News
Papa anasema kutoa viungo vya mwili bure ni zawadi ya ajabu lakini ya bure.Ni ishara ya upendo mkarimu ambao unapinga hatari dhidi ya maisha ya utoaji mimba na eutanasia Papa anasema kutoa viungo vya mwili bure ni zawadi ya ajabu lakini ya bure.Ni ishara ya upendo mkarimu ambao unapinga hatari dhidi ya maisha ya utoaji mimba na eutanasia  (ANSA)

Utoaji bure wa viungo kwa mujibu wa Papa ni ishara ya udugu na zawadi kwa Mungu!

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wajumbe 400 wa chama cha kujitolea cha Italia (AIDO) kwa ajili ya utoaji bure wa viungo ambapo amewakumbusha kuwa,kutoa bure siyo tendo la uwajibikaji tu kijamii,lakini ni kielelezo cha udugu duniani,ni ishara ya upendo mkarimu ambao unapinga hatari dhidi ya maisha ya utoaji mimba na eutanasia.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko, asubuhi tarehe 13 Aprili 2019 amekutana mjini Vatican na  wajumbe 400 wa Chama cha Kujitolea nchini Italia cha utoaji wa sehemu za viungo vya mwili, (AIDO). Katika hotuba yake anawashukuru kufika kwao, na kwamba wanawakilisha maelfu ya watu ambao wamechagua kushuhudia na kueneza thamani ya kushirikisha na kutoa zawadi, bila kuomba lolote la ziada. Aidha amewasalimu wote na kumshukuru Rais wao, Dk. Flavia Petrini kwa maneno ya hotuba yake wakati wa utangulizi wa mkutano huo. Baba Mtakatifu anasema, maendeleo ya madawa ya upandikizaji wa viungo imewezekana baada ya vifo vya mtu husika na katika baadhi ya kesi hata maisha (kwa mfano kesi ya figo) na viungo vingine ambavyo vimewezesha kuokoa maisha ya binadamu; kwa kuhifadhi na kutunza ubora wa afya ya watu wengine wagonjwa, ambao hawana tena fursa nyingine.

Utoaji bure wa viungo, unatoa jibu katika ulazima wa kijamii, kwa sababu, licha ya maendeleo ya tiba nyingi za madawa, mahitaji ya viungo hivyo bado yanabaki kuwa makubwa zaidi. Lakini licha ya maana ya kutoa viungu bure kwa mtoaji,na kwa yule anayepokea, kwa ajili ya jamii, haiwezi kuondolea kabisa msaada wake na ambao ni uzoefu wa binadamu wa kina  uliojaa upendo na ujasiri. Kutoa bure maana yake ni kutazama na kwenda zaidi ya  zaidi ya mahitaji binafsi na kujifungulia ukarimu wa kuelekeza wema ambao ni mkubwa. Katika mantiki ya kutoa bure viungo, si tu kama tendo la uwajibikaji kijamii tu, lakini pia ni kielelezo cha undugu duniani, ambao unafungamanisha kati ya watu wote, wanaume na wanawake.

Utoaji wa viungo baada ya kofi ni tendo bora na alama ya mshikamano

Wa mtazamo huo, Baba Mtakatifu anasisitiza akitaja kuwa katika Katekisimu ya Kanisa Katoliki inafundisha kwamba: “Utoaji wa kiungo baada ya kifo ni tendo bora na lenye mastahili na lihimizwe kama alama ya mshikamano wa ukarimu….”(n. 2296. Kulinganana ukuu wa uhusiano wa kibinadamu  wa kila mmoja, hasiweze kujikamilisha yeye mwenyewe tu, badala yake  hata kwa njia ya kushiriki katika ukamilifu wa wema wa wengine. Kila mtu hajiwakilishi yeye mwenyewe  kwa ajili yake bali kwa ajili ya jamii nzima; na kuanzia hapo, ndipo kuna maana kubwa ya jitihada za kufuatilia kwa ajili ya wema wa jirani. Katika Barua ya Waraka wa “Evangelium Vitae” wa Mtakatifu Yohane Paulo II, Baba Mtakatifu Francisko anasema, alitukubusha kwamba, kati ya ishara ambazo zinahusiana na kukuza utamaduni wa maisha wa  dhati na ambao unastahili kwa namna ya pekee kusifiwa ni utoaji wa viungo unaotimizwa kwa njia ya  mitindo inayokubalika ya kimaadili na inayopaswa kusisitizwa, kwa ajili ya kutoa uwezekano wa afya, hadi maisha ya wagonjwa ambao wakati mwingine wanakosa matumaini” (n 86).

Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu ameongeza kusema, ni muhimu kuendelea kudumisha suala la utoaji wa viungo kama tendo la ukarimu. Kwa dhati kila mtindo wa biashara ya mwili au sehemu yake ni kinyume na hadhi ya binadamu. Katika utoaji damu na kiungo cha mwili, ni lazima kufuata maadili na dini. Baba Mtakatifu akifafanua kuhusu wale ambao hawana dini anabainisha kwamba: kwa wote ambao hawana imani katika dini, ishara inayohitajika kitimizwa ni ile misingi ya mawazo ya kujitolea kimshikamano wa binadamu. Na kwa upande wa waamini wanaalikwa kushiriki kama sadaka ya Bwana, ambaye anajielezea kwa wale wanaoteseka, kwa sababu ya wagonjwa na ajali barabarani au kazini. Ni vema kwa ajili ya wafuasi wa Yesu kutoa viungo katika sheria inayokubaliwa na maadili, kwa maana hili ni tendo la zawadi iliyo tolewa na Bwana mteswa, ambaye alisema kila chochote mlicho fanya kwa ajili ya ndugu mwenye kuhitaji, mlimtendea Yeye ( Mt 25,40).

Umuhimu wa kuhamsisha utamaduni wa kutoa

Kadhalika Baba Mtakatifu Francisko amekazia kwamba ni muhimu kwa maana hiyo kuhamasisha utamaduni wa kutoa na ambao kwa njia ya habari, kukuza na kazi yao bila kuchoka,ambayo inasifiwa jitahada hizo na kupongezwa kwa sadaka kwa upande wa mwili binafsi na bila kuwa na hatari au matokeo mabaya, katika utoaji wa kiungo kwa mtu anayeishi, na viungo vyote vilivyo hai, baada ya mtu kufariki. Hata hivyo Baba Mtakatifu hakuficha hatari zilizopo kwamba: “Mbele ya hatari dhidi ya maisha, kwa bahati mbaya tunawaona kila siku, kwa mfano kesi ya utoaji mimba, na eutanasia,na hivyo katika jamii tunahitaji kwa dhati ishara hizi za mshikamano na upendo mkarimu ili kutambua kuwa maisha ni kitu kitakatifu”.

Baba Mtakatifu Francisko anawatia moyo wa kuendelea na jitihada za kulinda na kuhamasisha maisha kwa njia ya vyombo muhimu vya kufanya opereshi hiyo ya  kutoa viungo. Aidha amependa kukumbusha maneno ya Yesu;“Toeni nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwa-sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu” (Lk 6,38). Tutapokea zawadi kutoka kwa Mungu kwa mujibu wa upendo wa dhati ambao tuliuonesha kwa jirani. Na Bwana awabariki katika mapendekezo ya wema. Kwa upande wake,anawasindikiza kwa ubinadamu wake na Baraka zake na kuwashukuru.

13 April 2019, 13:30