Tafuta

Vatican News
Papa anasema Neno la Mungu ni zawadi ambayo Mfufuka anapenda kutoa na kuigawanya ili kweli maisha yawepo kwa jina lake Papa anasema Neno la Mungu ni zawadi ambayo Mfufuka anapenda kutoa na kuigawanya ili kweli maisha yawepo kwa jina lake  (ANSA)

Papa anahimiza ili Neno la Mungu liweze kukimbia kila kona ya Dunia!

Baba Mtakatifu amekutana na washiriki wa Mkutano wa Kimataifa,uliondaliwa na Shirikisho la Biblia Katoliki.Katika hotuba yake anasema,Biblia siyo mkusanyiko wa vitabu tu vitakatifu vya kujifunza,kwa maana ni Neno la Maisha ya kupanda.Ni zawadi ambayo Mfufuka anapenda kutoa na kuigawanya ili kweli maisha yawepo kwa jina lake!

Na Sr.Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 25 Aprili 2019, mchana katika Hotel ya Ergife mjini Roma ulifunguliwa Mkutano wa Kimataifa wa Shirikisho la Biblia Katoliki (CBF) na ambao umehitimishwa tarehe 26 Aprili 2019 ambapo washiriki hao wamekutana na Baba Mtakatifu Francisko. Tema ya Mkutano wao imeongozwa na Biblia na Maisha: msukumo wa kibiblia wa maisha yote ya kichungaji na utume wa Kanisa.  Na katika hotuba ya Baba Mtakatifu Francisko ameanza na maneno ya Mtume Paulo kwa kuwakaribisha wao walio Roma na wapendwa wa Mungu akiwatakia neema na amani (Rm 1,7).

Shirikisho la Biblia kuadhimisha miaka 50

Baba Mtakatifu anamshukuru Kardinali Tagle kwa salam zake, kwa niaba ya washiriki wote na kwa wote waliounganika katika fursa ya kuadhimisha miaka 50 ya Shirikisho la Biblia Katoliki. Jubilei hii imewapatia fursa ya kutazama kwa kina shughuli yao ya kikanisa na kujihakikishia uwajibikaji katika  kueneza Neno la Mungu. Katika tafakari yao wamezungukia maneno mawili yanahusu Biblia na maisha. Baba Mtakatifu Francisko amependa kusema kitu juu ya mambo hayo mawili. Neno la Mungu ni hai (Eb,4,12): halifi wala kuzeeka, bali linadumu milele (1Pt 1,25) Kwa maana nyingine linabaki kijana: “Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe” (Mt 24,35). Huhifadhi wale ambao wanazeeka ndani na kukua. Neno ni hai na kutoa maisha. Ni muhimu kumbuka kwamba Roho Mtakatifu na mtoaji wa Maisha, anapenda kufanya kazi kupitia Maandiko. Neno kwa hakika linapeleka pumzi ya Mungu duniani na kupasha joto la Bwana ndani ya moyo. Michango yote ya kitaaluma, vitabu ambavyo vimechapishwa, haviwezi kutokuwa katika huduma ya namna hii, Baba Mtakatifu amekazia.

Mfano wa kuni ziwashavyo moto, ndivyo wataalam wa utafiti wawe hivyo

Baba Mtakatifu Francisko anasema: kama kuni zilizokusanywa hata kwa shida ili ziweze kusaidia kupasha joto, japokuwa kuni hizo haziwezi kutoa joto zenyewe, ndivyo sawa na wataalam bora wa utafiti. Inahitajika joto la Roho ili Biblia iweze kuwaka ndani ya moyo na kugeuka maisha! Na kwa maana hiyo kuni njema zinaweza kuwasaidia kuongeza moto huo. Japokuwa Biblia siyo mkusanyiko wa vitabu tu vitakatifu vya kujifunza, kwa maana ni Neno la Maisha ya kupanda. Ni zawadi ambayo Mfufuka anapenda kutoa na kuigawanya ili kweli maisha yawepo kwa jina lake(Yh 20,23). Katika Kanisa Neno ni kama sindano ya maisha isiyoweza kubadilishwa. Kwa njia hiyo mahubiri ni msingi. Kuhubiri siyo mazoezi ya kusema, hata upamoja wa mawazo ya hekima ya kibinadamu, kama ingekuwa hivyo,ingekuwa kama kuni anasema Baba Mtakatifu. Lakini kinyume chake ni ushirikishwaji wa Roho (rej, 1 Kor 2,4). Ni Neno la Mungu ambalo limegusa moyo wa mhubiri, ambaye anaelezea lile joto na ule upako. Mara nyingi Baba Mtakatifu anabainisha kwamba, maneno mengi yanasikika katika masikio yetu kwa kutupatia habari na kutoa vigezo vingi; labda ni mengi zaidi hadi kushinda kiwango cha uwezo wetu wa kuyapokea. Lakini hatuwezi kukataa Neno la Yesu, ambalo ni moja ya Neno la Maisha ya Milele (Rej, Yh 6,68) ambayo sisi tunahitaji kila siku!

Ingekuwa vizuri kuona uchanuzi wa kipindi kipya cha upendo wa Maandiko Matakatifu

Baba Mtakatifu akiendelea kusisitiza juu ya Neno, anabainisha kuwa, ingekuwa vizuri kuona uchanuzi wa kipindi kipya cha upendo mkuu wa Maandiko Matakatifu kwa upande wa wote yaani watu wa Mungu na ili kujiimarisha kwa kina katika uhusiano na mtu mwenyewe yaani  Yesu (Wosia: Verbum Domini, 72). Ingekuwa vizuri Neno la Mungu kugeuka daima kuwa moyo wa kila shughuli ya Kanisa (Wosia: Evangelii gaudium,174); Moyo unaodunda na ambao unaimarisha viungo vya mwili.  Ni shauku ya Roho kututengeneza sisi kama Kanisa “lililoundwa na Neno”. Liwe ni Kanisa ambalo halizungumzi peke yake au lenyewe, lakini lenye kuwajibika ndani ya moyo na katika midomo ya Bwana ambaye kila siku kwake  linachota Neno lake.  Hata hivyo amesema kuwa, kinyume na hilo daima upo umakini wa kujikana sisi wenyewe na kuzungumza maendeleo yetu binafsi! Lakini kwa kufanya hivyo hatuwezi kuonesha maisha duniani!

Neno linatoa maisha kwa kila mwamini na kufundisha kujikana binafsi kwa ajili yake. Katika maana hiyo, ni kama vile upanga ambap unachoma na kuingia kwa kina nafsini, unang’amua mawazo, hisia na kupeleka mwanga wa ukweli, kwani yeye huumiza, lakini tena huuguza; Yeye hutia jeraha na mikono yake kwa maana anatia jeraha ili kuponya (rej Eb 4,12; Ay 5,18). Neno linakupeleka ili uliishi kwa namna ya Pasaka. Kama mbegu ikifa inatoa maisha; kama zabibu itoavyo divai, kama zeituni zitoavyo mafuta baada ya kukamuliwa. Kwa njia ya kuchochea zawadi kubwa za uzima. Neno linasaidia kuishi. Haiwezi kukuacha na utulivu, badala yake linakuweka katika mjadala wa kujiuliza. Kanisa ambalo linaishi kwa kusikiliza Neno haliwezi kamwe kubaki katika usalama wake. Linakupeleka pale mahali penye mambo mapya ya roho na yasiyo tarajiwa. Halichoki kutangaza na wala kukata tamaa, haliachi kamwe kuhamasisha na kuimarisha kwa kila ngazi juu ya muungano, kwa sababu Neno linaita umoja na kualika kila mmoja kusikiliza mwingine na  kushinda kila aina ya vigezo maalum.

Kanisa linalomwilishwa kwa Neno linaishi kwa ajili ya kutangaza Neno

Kanisa linalomwilishwa kwa Neno linaishi kwa ajili ya kutangaza Neno. Halizungumzi nyuma yake, bali linashuka katika barabara za dunia. Si kwa sababu hupenda  wao au ni rahisi, lakini ni kwa sababu ndiyo sehemu za kutoa tangazo. Kanisa aminifu katika Neno, halijibakizi bila kutangaza Kergma na wala kusubiri kusifiwa. Neno la Mungu litokalo kwa Bwana linaingia duniani na kusukumwa hadi kufikia kila kona ya dunia. Ni Neno la Mungu, syio letu na linatuondoa na tabia ya kujiweka katikati;litulinda dhidi ya kujitosheleza na kutaka ushindi na linaendelea kutualika daima  kutoka ndani yetu binafsi. Neno la Mungu lina nguvu ya katikati, isiyo pembeni: halisababishi ujikunyate ndani, badala yake ni kukusukuma kutoka ndani ili kuwafikia wale ambao bado hawajafikiwa. Halihakikishi joto la uvuguvugu, kwa sababu ni moto na upepo na ni Roho ambayo huwasha moyo na kuleta mabadiliko ya upeo kwa kupanua ubunifu wake.

Biblia na maisha

Baba Mtakatifu Francisko, anawasihii wajitahidi katika maneno mawili ya Biblia na maisha ambayo yanakumbatiana ili moja lisiweze kukaa bila mwenzake. Amehitimisha kama alivyoanza na salam ya Mtume Paulo anapohitimisha barua yake: Mengineyo ndugu salini. “Kama  yeye hata mimi ninawaomba msali. Lakini Mtakatifu Paulo anabainisha sababu yak usali: ili Neno la Mungu liweze kukimbia (2Ts 3,1). Tusali na kuwajibika ili Biblia isibaki katika Makataba kati ya vitabu vingi vinavyozungumza, badala yake ikimbie katika barabara za dunia hii, mahali ambapo watu wanaishi na kusubiri. Anawataka wote wawe wachukuzi wa Neno, kwa shauku ile ile ambayo inasomwa katika siku hizi za Pasaka, mahali ambapo wote wanakimbia: wanawake, Petro, Yohane na wafuasi wa Emau… wanakimbia uli kukutana na kutangaza Neno hai. Ndiyo matashi yake ya moyo kwao na kuwashukuru kwa yote wanayofanya!

 

26 April 2019, 13:46