Tafuta

Vatican News
Papa amekutana na Mwenyekiti wa nchi ya Bosnia na Herzegovina  Bwana Milorad Dodik Papa amekutana na Mwenyekiti wa nchi ya Bosnia na Herzegovina Bwana Milorad Dodik  (ANSA)

Papa amekutana na Mwenyekiti Milorad Dodik wa Bosnia na Herzegovina

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 26 Aprili amekutana na Mwenyekiti wa nchi ya Bosnia na Herzegovina Bwana Miloradn Dodik na baadaye kukutana Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican akisindikizwa na Monsinyo Antoine Camilleri,Katibu msaidizi,Vatican wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Tarehe 26 Aprili 2019 Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Mwenyekiti Milorad Dodik wa Bosnia na Erzegovina, ambapo baadaye amekutana na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican akisindikizwa na Monsinyo Antoine Camilleri, Katibu msaidizi wa Vatican wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa.  

Mahusiano ya nchi mbili, changamoto na matarajio

Katika mazungumzo yao wameonesha mahusiano mema kati ya nchi hizi mbili na uhai wa jumuiya Katoliki nchini Bosnia na Erzegovina, pia kugusia hali halisi ya nchi na changamoto zake za kiuchumi na kijamii wanazokabiliana nasi. Zaidi wamegusia hata dharura ya kuhakikisha matokeo ya usawa wa watu wake, hasa juu ya michakato ya mapatano kati yao na kusisitizia umuhimu wa mazungumzo katika mantiki ya katiba na ili kuweza kushinda migawanyiko na kutafuta amani. Hatimaye mada nyingine za pamoja zilizogusiwa ni mantiki ya kimataifa kwanamna ya pekee wakiwa na matarajio ya kupanuka kwa Umoja wa Ulaya kwa njia za Nchi za kibaltiki.

26 April 2019, 13:24