Cerca

Vatican News
Papa Francisko anawashukuru wananchi wa Morocco kwa mapokezi makubwa waliyomkirimia wakati wa hija yake ya kitume kuanzia tarehe 30-31 Machi 2019 Papa Francisko anawashukuru wananchi wa Morocco kwa mapokezi makubwa waliyomkirimia wakati wa hija yake ya kitume kuanzia tarehe 30-31 Machi 2019  (AFP or licensors)

Hija ya Papa Francisko Morocco: Viongozi wakuu wa nchi!

Papa Francisko akiwa njiani kurejea mjini Vatican amewatumia viongozi wa Morocco, Algeria na Italia ujumbe wa shukrani, salam, amani, maendeleo na ustawi kwa wananchi wao! Kwa namna ya pekee, Papa amemshukuru Mfalme Mohammed VI wa Morocco kwa ukarimu na mapokezi makubwa waliyompatia. Anawatakia heri na baraka; amani na ustawi wananchi wote wa Morocco.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumapili tarehe 31 Machi 2019 amehitimisha hija yake28 ya kimataifa nchini Morocco iliyoongozwa na kauli mbiu “Papa Francisko mhudumu wa matumaini Morocco 2019”. Akiwa njiani kurejea mjini Vatican amewatumia viongozi wa Morocco, Algeria na Italia ujumbe wa shukrani, salam, amani, ustawi na maendeleo na ustawi kwa wananchi wao! Kwa namna ya pekee, Baba Mtakatifu amemshukuru Mfalme Mohammed VI wa Morocco kwa ukarimu na mapokezi makubwa waliyompatia. Anawatakia heri na baraka; amani na ustawi wananchi wote wa Morocco.

Baba Mtakatifu wakati alipokuwa anaingia katika anga la Algeria, amemtumia salam na matashi mema Rais Abdelaziz Bouteflika, Rais wa Algeria na kuwaombea amani na nguvu ya kusonga mbele kwa ari na moyo mkuu. Papa Francisko alipoingia kwenye anga la Italia, amemtumia salam na matashi mema Rais Sergio Mattarella! Amemweleza Rais Mattarella kwamba, amebahatika kukutana na familia ya Mungu nchini Morocco! Baba Mtakatifu anasema, amekutana na Jumuiya ya Wakristo nchini humo na kuwatia shime kuendeleza mchakato wa amani, ustawi na maendeleo ya Morocco katika ujumla wake! Mwishoni mwa salam zake, amemtakia Rais Mattarella kwa niaba ya familia ya Mungu nchini Italia, heri na baraka na kuwataka kusonga mbele kwa ari na moyo mkuu, ili kuweza kukabiliana na ya mbeleni kwa ujasiri zaidi!

Papa: Salam kwa Viongozi
01 April 2019, 11:24