Tafuta

Vatican News
wafiadini 9 wa Jimbo Kuu la  Oviedo nchini Hispania ambao walikuwa ni waseminari waliouwawa kati ya mwaka 1936-1937 wafiadini 9 wa Jimbo Kuu la Oviedo nchini Hispania ambao walikuwa ni waseminari waliouwawa kati ya mwaka 1936-1937 

Papa:Wenyeheri 9 nchini Hispania ni wafiadini waseminari

Mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, kwa mahujaji na waamini wote katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,Baba Mtatifu amekumbusha wenyeheri wapya 9 waseminari ambao wametangazwa jimboni Oviedo nchini Hispania tarehe 9 Machi 2019

 Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu amekukumba ni kwa jinsi gani tarehe 9 Machi huko Jimbo Kuu la Oviedo nchini Hisipania, walitangazwa wenyeheri wapya waseminari Angelo Cuatas na wenzake nane wafiadini  wakitetea imani yao katika kipindi cha mateso ya wakristo. Vijana hawa walio kuwa katika mafunzo ya kikuhani, walimpenda Bwana upeo na kufuata njia ya msalaba. Baba Mtakatifu anabainisha kuwa ushujaa wao wa ushuhuda, uwasaidie waseminari, mapadre na maaskofu kubaki kidete na ukarimu kwa ajili ya kuhudumia kwa uaminfu Bwana na watu wa Mungu.

Wafia dini waseminari tisa kutangazwa wenye heri na Rais wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza watakatifu

 Wafia dini 9 waliuwawa kati ya mwaka 1936-1937. Na kwa niaba ya Baba Mtakatifu Francisko,maadhimisho hayo yameongozwa na Kardinali Angelo Becciu,Rais wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza Wenyeheri na Watakatifu. Leo hii tunahitaji kuwa na waseminari, mapadre na watu wote waliotiwa wakfu kuwa wachungaji wakarimu kama wafiadini hawa anasema Kardinali Becciu. Hawa walikuwa ni waseminari waliompenda Bwana na walikuwa wamefanya uchaguzi wao kwa hakika kutoa maisha yao kwa Bwana. Hawa walifanya uchaguzi huo hadi sadaka ya mwisho. Uchaguzi wa imani kwa Kristo na ambapo inapaswa iwe mafundisho makubwa kwa mapadre wote  na kuwajibika kwa dhati katika wito wao.

Ángel Cuartas Cristóbal na wenzake 8 waseminari waliuwawa kati ya mwaka  (1936-1937)

 

Ángel Cuartas Cristóbal na wenzake 8 waseminari waliuwawa kati ya mwaka  (1936-1937) Jimbo Kuu Oviado nchini Uhispania. Katika  historia ya hawa vijana wafiadini Kardinali Becciu anasema mwaka 1934 nchini Uhispania ulikuwa ni mwaka mgumu sana ambapo mashambulizi dhidi ya wakristo yalikuwa ni makubwa mno. Vilevile kwenye miaka hiyo  itakumbukwa kwa vita vya kispanyola kati ya mwaka 1936-1939 na baadaye pia vifo vya wengine katika Vita ya pili ya Dunia katika mji wa Asturie. Kulikuwa na mapambano kila sehemu na umwagaji damu katika miji mingine ya Oviedo, mahali ambapo watu wengi, hasa mapadre na watawa waliuwawa bila sababu. Baada ya vita  inahesabikiwa kuwa waliuwawa watu 6,832 na waathirika hawa wa vita vya wenyewe kwa wenyewe raia wa kispanyola  ambao kati yao walikuwa ni watawa, mapadre na walei walio uwawa kwa sababu ya kutetea imani ya dini katoliki, anathibitisha  Kardinali Becciu.

Ushuhuda wa waseminari hawa  

Waseminari wa Oviedo ni mashuhuda wa imani kwani mwisho wa kiangazi cha mwaka 1934, Angel Cuartas Cristóbal mmoja wa waseminari wengi alipomaliza likizo yake nyumbani alikuwa arudi katika Seminari kuu ya Oviedo mahali ambapo kwa miezi kadhaa alikuwa amepewa daraja la ushamasi. Mseminari huyo alikua ni mmoja kati ya watoto 9 wa familia yake ambayo ilimshauri hasirudi Oviedo, kwa maana kulikuwa na mambo mabaya yakitokea. Yeye lakini hakutii wazazi wake, kwa maana alikuwa na  utambuzi  kuwa ndipo Bwana anamtaka wito wake na  hata kama angeuwawa.

Uamuzi huo pia ndiyo ulikuwa sawa na wenzake watano ambao kama yeye walikuwa wameamua kurudi Seminarini. Wote hao walikuwa ni vijana wafiadini. Suárez Fernández, aliamua kuendelea na masomo kwani mwaka huo alikuwa afunge nadhiri, Jesús Prieto López, familia yake ilikuwa maskini na karo ilikuwa analipiwa na Parokoko wake;  César Gonzalo Zurro Fanjul, yeye alikufa akipaza sauti yake kuwa “Yesu ni hai, ukatoliki nchini Hispania hoyee! José María Fernández Martínez, alikuwa ni mtoto yatima wa mama yake na baba yake alikuwa anafanya kazi katika mashimo ya machimbo;Juan José Castaňon Fernández, ndiye aliyekuwa mdogo zaidi katika kundi hilo kwa maana alikuwa mehitimisha miaka 18 tu na aliyekuwa mkubwa kati yao alikuwa na umri wa miaka 24.

Salam Mbalimbali za Baba Mtakatifu kwa mahujaji toka pande za dunia

Baba Mtakatifu amewasalimia mahijaji wotye waliofika kutoka pande zote za dunia. Aidha amewatakia safari njema ya Kwaresima amabyo imeanza hivi karibuni , na kuwakumbusha wasali kwa ajili yake na wahumu wake ambao wanaaanza mafungo ya ya kiroho ya kwaresima wiki hii. Na wote wametakia mlo mwema.

11 March 2019, 09:50