Tafuta

Vatican News
Katika mashambulizi ya kigaidi,huko New Zealand Baba Mtakatifu Francisko anawaombea  majeruhi na roho za marehemu wapumzika katika huruma ya Mungu Katika mashambulizi ya kigaidi,huko New Zealand Baba Mtakatifu Francisko anawaombea majeruhi na roho za marehemu wapumzika katika huruma ya Mungu  

New Zealand:Papa ametuma salam za rambi rambi

Telegram iliyotiwa sahini na katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin ambapo Baba Mtakatifu Francisko anaelezea uchungu kufuatia na mashambulizi ya misikiti katika mji Christchurch New Zealand ambapo Watu 49 wameuawa katika shambulio la kigaidi

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baba Mtakatifu Francisko anasikitika sana kwa majeruhi na kupoteza maisha ya binadamu yaliyotokana na vitendo vibaya vya kigaidi katika misikiti ya Christchurch, huko New Zealand. Hayo yanaoneshwa katika telegram yake iliyotiwa sahini na Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin.

Anawawakikishia wazalendo wote wa New Zealand,  kwa namna ya pekee jumuiya nzima ya kiislam,mshikamano wake wa  dhati katika mashambulizi haya. Kwa utambuzi wa nguvu za vyombo vya madola vya usalama na dharura katika kipindi kigumu, anasali kwa ajili ya majeruhi ili wapone haraka na faraja kwa wale ambao wanaoomboleza kwa ajili ya wapendwa wao, kwa wote ambao wameguswa na janga hili na kuwakabidhi marehemu wote katika huruma ya Mungu mwenyezi. Mwisho anawatia moyo na nguvu Taifa zima.

Taarifa kutoka vyombo vya habari vinasema kuwa aliyesababisha shabulizi hili wakati wa swalah kwenye Msikiti wa Al Noor, ambapo walikuwa  ni watu wanne wakiongozwa na kijana mwenye umri wa miaka 28 wa Australia, Brenton Tarrant, aliyejieleza kuwa ni mtu mweupe wa kawaida lakini anataka kuwauwa wageni wavamizi. Ni hofu, na mashaka kwa nchi nzima. Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern anasema watu 49 wameuawa na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa vibaya baada ya kuzuka mashambulio katika misikiti miwili katika mji wa Christchurch, huko New Zealand.

Waziri mkuu huyo amelitaja shambulio hilo kuwa mojawapo lililotanda kiza kikubwa kwa siku hiyo nchini humo. Hata hivyo wanaume watatu na mwanamke mmoja wamekamatwa, na kamishna wa polisi Mike Bush, lakini ameonya kwamba huenda washukiwa zaidi wapo. Inaarifiwa kwamba washambuliaji hao hawakuwa kwenye orodha ya magaidi wanaosakwa, lakini ni wazi kwamba wana itikadi kali!

 

15 March 2019, 14:24