Tafuta

Vatican News
Sakramenti ya upatanisho kati ya  Mungu na binadamu Sakramenti ya upatanisho kati ya Mungu na binadamu 

Mons.Nykiel:Ni katika kuungamana ili kuhisi upendo wa Mungu!

Tarehe 29 Machi itahitimishwa kozi ya 30 kuhusu Sakramenti ya toba ambapo mwisho wa kozi hiyo washiriki watakutana na Papa Francisko baadaye kufuatia maadhimisho ya Sakramenti ya upatanisho yatakayoongozwa na Papa.Monsinyo Nykiel hakimu wa Idara ya Toba ya Kitume katika mahojiano na Vatican News,anaelezea maana ya kozi hiyo

Na Sr Angela Rwezaula- Vatican

Daima Kanisa linaendelea kujikita kwa ajili ya uongofu wa waamini wake, hasa kwa njia ya Sakramenti ya upatanisho ambayo ni muhimu  katika safari ya maisha ya kiroho. Ni katika Sakramenti ya Upatanisho, mahakama ya huruma ya Mungu, waamini wanaweza kweli kuonja na kufanya uzoefu wa huruma hiyo upendo na msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu; Mama Kanisa anapoweka vipindi maalum kama hiki cha Kwaresima kwa kujitafiri maisha ya undani, ili kuweza kweli kumfuasa Kristo, aliyeteseka, akafa na hatimaye kufufuka. Ni katika sakrameti ya upatanisho mahali ambapo waamini wanaweze kweli kuhisi ndani mwao wanakuguswa na kupyaishwa, tayari kujikita kwenye hija na  kuendelea mbele kama Baba Mtakatifu Francisko anavypenda kusisitizia na kuhamasisha maisha ya toba.

Na ndiyo maana kozi ya kuwaandaa mpadre na waseminari wanaotarajiwa kuwekwa wakfu ili waweze kuwa mapadre waungamishi wema na kuwa uwezo wa kisaidia watu wa Mungu wanao kabidhiwa. Ili kufanya hivyo imeandaliwa kozi ya 30 ya kuhusu sakramenti ya Toba iliyo andaliwa na Idara ya Toba ya Kitume kuanzia tarehe 25 Machi hadi  29 Machi 2019 na ambapo washiriki wote watapata fursa ya ku kutana na Baba Mtakatifu Francisko pia  kufuatia maadhimisho ya Sakramenti ya upatanisho. Hayo ni maadhimisho makubwa ya toba ambayo yataongozwa na Baba Mtakatifu Francisko katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Akielezea maana ya kozi hiyo katika  mahojiano na Vatican  News, Monsinyo  Krzysztof Josef Nykiel, Hakimu wa Idara ya Toba ya Kitume anafafanua juu ya jitahada  katika Idara ya toba ya Kitume kwa kuwafundisha mafunzo mapadre wapya, na waseminari wanaotarajiwa kuwekwa wakfu. Na kwamba leo hii kwa dhati kunahitajika wadumu wa kweli wa huruma na mabao zaidi wanahitaji maandalizi ya kitaalimungu, kitasaufi, kichungaji na kisheria. Kuanzishwa kwa hatua hii ni kutaka kuwasaidia mapadre waweze kuwa wema katika kutoa msamaha  na kuwa waalimu ambao wanaelekeza kwenda kwa Kristo. Ni umakini ambao katika huruma ya Baba Mtakatifu anahamasisha pia  ni mwaka wa 30 tangu waanzishe kozi hi ina ambayo kwa mwaka huu imewashirikisha wahudumu 700 ambao ni mashuhuda kutokana na kuongezeka utambuzi wa huduma hiyo. Katika kozi yao mada ambazo zimetolewa zinahusika na uendeshaji wakati wa kutoa huduma ya upatanisho na hata katika kesi maalum ambzo wakati wa Sakramenti, muungamishi anaweza kukumbana nazo.

Hata hivyo pia wameweze kutoa maelezo muhimu na mchakato wa kufanya au kutuma maswali katika Idara ya Toba ya Kitume kwa maana kuna wataalam zaidi wa maswala hayo. Vile vile amefafanua kuwa pamoja hayo, kozi haikuwa inatazama juu ya  masomo ya  kitaalimungu na kisheria lakini zaidi wameweza kutoa maelekezo muhimu kwa waungamisho  ili kuwasaidia kwa dhati waamini, wakiwa na uwezekano huo na kuhamasisha katika huruma ya kibaba ili kuweza kukutana na huruma ya Mungu. Monsinyo ameongeze kusema, ingekuwa vizuri iwapo kila muungamishi ameweza kuishi kipindi hiki kama neema maalum, muujiza wa kudumu wa huruma ya Mungu, kama alivyokumbusha hivi karibuni Baba Mtakatifu Francisko alipokutana na makleri wa Roma. Vile vile amesema kuungama ni moja ya changamoto leo hii na ambayo inataka kusaidia watu wajifungulie uzoefu wa upendo wa Mungu. Tunaishi katika mantiki ambayo kumtafuta Mungu ni shida, na kwa maana hiyo mtu anahisi kwa hakika kuwa msitari wa mbele wa kutafuta furaha, wakati huo hujidanganya mwenyewe bila kutafuta msaada wake. Lakini Mungu hashindani na mtu, bali yeye ni msaidizi mkubwa! Na huo ni uzoefu ambao unaweza kuhisi mara tu ukikaribia katika sakrementi ya upatanisho na kila mmoja anahisi kupendwa bila kikomo na Mungu.

Katika Wosiwa wa kitume wa Baba Mtakatifu Francisko 'Gaudete et exsultate', anawakumbusha waamini wote kuwa, mwisho wa maisha yetu yote ni utakatifu! Kwa kusoma makini wosia huo inagundua wazi kwamba sakrmenti ya upatanisho ni chombo msingi cha kuweza kusaidia katika safari ya waamni kuelekea utakatifu anathibitisha Monsinyo Nykiel. Kuungama kunaweza kugeuka msaada wa kusimama daima mara  tunapoanguka. Ni dawa dhidi ya sumu kali ya itikadi mbaya. Ni moja ya chombo cha kukuza unyenyekevu na wakati huo  huo ni kuleta furaha kwa yule mtoto anayefanya uzoefu wa kukumbatiwa kwa upendo wa Mungu. Maungamo yanaweza kuwa sehemu ya ukweli na kukuza kumbukumbu ya shukrani kwa historia binafsi na kung’amua kila siku. Kutokana na hiyo, imani katika huruma ya Mungu kwa kujikita mara kwa mara katika sakramenti ya upatanisho, mahali ambapo unatambua moyo unaotubu makosa yake , unaweza kweli kuhisi na kufanya uzoefu wa upendo mkuu wa Baba. Na zaidi Monsinyo Nykiel ametaka kukumbusha kuwa, Skarementi ya upatanisho ni njia ya utakatifu  wa ndani wa maisha na siyo tu kwa ajili anayeungama, bali hata muungamishi, mwenye kuwa na neema ya kutafakari kila siku miujiza ya maungamo ambayo Mungu anatenda ndani yake na kwa wengine.

 

28 March 2019, 10:29