Tafuta

Vatican News
Malaika wa Bwana Malaika wa Bwana  (Vatican Media)

Papa awakumbuka wafiadini wamisionari!

Mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana,Baba Mtakatifu amekumbusha mahujaji na wamini kuhusu kutangazwa kwa mwenyeheri mpya,Siku ya kumbu kumbu ya wafia dini,sala kwa waathirika wa Nigeria na Mali na ziara katika Madhabahu ya Loreto,tarehe 25 machi ikiwa ni Siku ya Kupashwa habari Bikira Maria

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu Francisko, mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Dominka ya tatu ya Kwaresima tarehe 24 Machi 2019, akikumbuka kwa namna ya pekee nchi Nicaragua ambayo inapitia kipindi kigumu cha machafuko kijamii na kisiasa amesema: Ndugu wapendwa, kaka na dada, tangu tarehe 27 Februari, upo mchakato wa mazungumzo ya kutoa suluhisho la kipeo cha jamii kisiasa, kinacho ikumba nchi ya Nicaragua. Ninawasindikiza kwa sala katika shughuli hii na kuwatia moyo ili waweze kupata sululu la amani kwa haraka kwa ajili ya wema wa wote.

Mwenyeheri mpya Mariano Mullerat I soldevila,Hispania

Aidha Baba Mtakatifu Francisko amewakumbusha watu ya kwamba tarehe 23 Machi 2019 huko Arragona nchini Hispania, ametangazwa mwenye heri Mariano Mullerat I soldevila, Baba wa familia na daktari, kijana aliyefariki akiwa na umri wa miaka 39 na ambaye alijikita kuwatunza ndugu wanaoteseka kimwili na kiroho kwa kushuhudia na maisha yake yake ya kifo dini cha ukuu wa upendo na msamaha. Ni mfano kwa ajili ya sisi sote ambao ni vigumu kusamehe, anasema Baba Mtakatifu. Yeye ananatuombea na kutusaidia ili tutembee katika njia ya upendo na udugu licha ya matatizo na mahangaiko. Tumshangilie Mwenyeheri mpya!....

Siku ya kumbu kumbu ya wafia dini

Leo hii Baba Mtakatifu Francisko anasema ni maadhimisho ya kukumbuku wamisionari wafia dini. Kwa mwaka 2018 duniani  kote, idadi kubwa ya maaskofu, mapadre,watawa na waamini walei wameathiriwa kwa nguvu; wakati huo huo, wameuwawa wamisonari karibu mara mbili zaidi ya mwaka uliotangulia. Kukumbuka karvari ya wakati huu kwa kaka na dada wanaoteswa au kuwawa kwa sababu ya imani yao kwa Yesu ni wajibu kwa Kanisa lote, lakini pia ni chachu ya kushuhudia kwa ujasiri wa imani yetu na matumaini kwa Yule ambaye juu ya msalaba alishinda daima chuki na vurugu kwa njia ya upendo.

Sala kwa ajili ya waathirika Nigeria na Mali

Baba Mtakatifu anawaombea idadi kubwa ya waathrika wa mashambuzi yasiyo ya kibindamu ambayo yametokea huko Nigeria na Mali. Bwana awapokee waathrika ha ona kuwaponya majeruhi, awafariji familia za ona kuongoa mioyo ya wakatili. Ameomba kusala sala ya Salam Maria….

 Ziara yake katika Madhabahu ya Mama Maria Loreto

Baba Mtakatifu Francisko amewataarifu juu ya Sikukuu ya kupashwa habari kwa BIkira Maria tarehe 25 Machi na ambapo anakwenda Loreto nyumba ya Bikira Maria. “ Nimechangua sehemu hii kutia sahini ya Hati ya Kutume inayohusu Vijana. Ninaomba sala zenu ili “tazama mimi” ya Maria igeuke kuwa “tazama mimi” kwa ajili ya wengi.

24 March 2019, 14:31