Tafuta

Vatican News
Mkutano wa Papa na washiriki wa Kozi kuhusu sakramenti ya upatanisho Mkutano wa Papa na washiriki wa Kozi kuhusu sakramenti ya upatanisho  (ANSA)

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki wa kozi ya sakramenti ya upatanisho

Papa amekutana na washiriki zaidi ya 700 wa kozi kuhusu Toba ya kina ya Sakramenti ya Upatanisho,iliyoandaliwa na Idara ya Toba ya Kitume kuanzia tarehe 25-29 Machi 2019.Papa anatoa ushauri kwa waungamishaji watambue kuwa ni wadhambi,waheshimu hadhi ya kila mtu,japokuwa ni changamoto ya padre kuwapeleka katika uzuri wa huruma ya Mungu

Na Sr Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 29 Machi Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki zaidi ya 700 wa kozi kuhusu,(Foro Interno) yaani Toba ya kina ya Sakramenti ya upatanisho. Ni kozi iliyoandaliwa na Idara ya Toba ya Kitume kuanzia tarehe 25-29 Machi 2019. Baba Mtakatifu anatoa ushauri kwa waungamishaji na mbao pia ni wadhambi waliosamewa, waheshimu hadhi ya kila mtu na ambayo ni changamoto ya padre ili kuweza kuwapeleka waamini katika uzuri wa huruma ya Mungu. Baba Mtakatifu katika hotuba yake kwa washiriki wa Mkutano huo kuhusu sakramenti ya kutubio ambapo katika fursa hiyo ni mwaka wa 30 tangu kuanzishwa kwa kozi hiyo, anawakaribisha na kufafanua maana ya undani wa kina, na kwamba siyo nje na kinyume yake. Amethibitisha hayo kutokana na kwamba, amegutuka kusikia kuwa, baadhi ya makundi katika Kanisa, waliokabidhiwa madaraka, wakuu, wanasema hivyo kwa kuchanganya mambo mawili pamoja, kwani wanachukua suala la kina cha ndani ili kufanya maamuzi wakiwa nje na kumbe nje ni kitu kingine tofauti. Hakika hiyo ni dhambi, anasema.

Ni dhambi dhidi ya hadhi ya watu ambao wanawaamini mapadre na  wanaoona hali halisi yao ili kuomba msamaha na kumbe  baadaye wanawatumia ili kusawazisha mambo katika makundi au vyama na labda matukio, hadi kufikia kuanzisha  labda shirika, Baba Mtakatifu amesema. Kwa kufafanua zaidi  anasema ukina wa ndani ni wa ndani. Na ni jambo takatifu! anakazia. Hii ndiyo maana yake. Anaongeza kusema "ndiyo maana nimezungumzia hili". Hata hivyo ameendelea na salam zake kwa  Kardinali Mauro Piacenza,ambaye ni mhusika wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makleri kwa hotuba yake hata kuwasalimia familia nzima ya Idara ya Toba ya kitume. Baba Mtakatifu anasema kuwa, umuhimu wa huduma ya huruma yenye haki inatakiwa na inapendekeza mafunzo yanayo takiwa kwa sababu mkutano na waamini wanaoomba msamaha wa dhambi kwa Mungu uweze kuwa daima mkutano wa kweli wa wokovu na ambapo kwa kuguswa na mkono wa Bwana wanaweze kutambua nguvu zake, uweza wake na kuwabadilisha,kuwaongoa, kuwatibu na kuwasamehe!

Miaka 30 ya uzoefu wa kozi hiyo ya Toba ya kina ya sakramenti, siyo mingi kulinganisha na historia ya Kanisa na kulinganisha na Toba ya zamani ya Kitume Ambayo ni ya zamani  ya mahakama ya huduma ya Papa. Mahakama ya huruma ! “Ninapende sana iwe hivyo” ameongeza Baba Mtakatifu. Licha ya miaka hii 30 katika nyakati zetu, inayokimbia kwa haraka ni kipindi tosha kirefu cha kuweza kufanya tafakari  na kupimwa, zaidi ya kuwa na idadi kubwa ya washiriki zaidi ya 700 mwaka huu, Kardinali amesema wamejikita kuelezea sababu za uendeshaji, utafikiri ni mchezo ambao labda hakuna nafasi Vatican. Lakini inaonesha ni kwa namna gani kuna haja ya  kufanya mafunzo na usalama kulingana na suala muhimu hili kwa ajili ya maisha yenyewe ya Kanisa na utumilifu wa Bwana Yesu alioukadhi kwa Kanisa lake.

Yesu alikuja kutukomboa na kutuonesha uso wa huruma ya Mungu na kutuvutia kwake kwa njia ya sadaka ya upendo. Kwa mana hiyo tunapaswa daima kukumbuka kuwa Sakramenti ya Kitubio ni ya kweli na njia ya dhati ya utakatifu, ni ishara mwafaka ambayo Yesu aliachia Kanisa ili liweze kuwapeleka katika nyumba ya Baba na wabaki daima na ikiwezakana warudi watu wote kwake. Sakramenti ya toba ni njia ya utakatifu kwa maana ipo kwa aanaye ungama na anayeungamisha. Anayeungama kwa hakika ni njia ya utakatifu kwa sababu kama alivyosisitiza mara nyingi wakati wa Jubilei ya Huruma, anasema, sakramenti ya toba ina thamani katika kuadhimisha kwa maana inapyaisha ubatizo na kuwa na muungano kamili na Mungu. Ni muungano ule ambao Mungu hakatishi kamwe na mtu japokuwa mtu mwenyewe mara nyingi anatumia vibaya zwadi nzuri ya uhuru huo.

Baba Mtakatifu amewakumbusha kuwa katika Jimbo lako mwaka huu mapadre wamechangua kauli mbiu ya Upatanisho, dada wa Ubatizo. Baba Mtakatifu anathibitisha Sakramenti ya Toba ni dawa wa Ubatizo na Kaka wa Ubatizo. Kwa upande wa mapadre, sakrementi ya nne ni njia ya utakatifu hasa kwa unyenyekevu kama wote tulivyo wadhambi, tunapaswa kupiga magoti mbele ya muungamishi na kuomba kwa ajili yetu sisi huruma ya Mungu. Ni lazima kukumbukadaima, amehimiza, na kwamba, itawasaidia sana kabla ya kwenda kuungamisha. Baba Mtakatifu amewageukia mapadre na ambao watawekwa wakfu, waungamishi akiwashaur wasikilize waamini wanao kwenda kuungama. Wawe na uvumlivu lakini daima wakiwa na moyo wazi na roho ya ubaba. Aidha amewashuri watembee nao katika njia ya utakatifu   ambayo ni sakrementi, watafakari miujiza ya uongofu ambao kwa nema na siri ya maungamo, ni miujiza ambayo inatokana na wao na malaika watakuwa mashuhuda. Kwa kufanya hivyo wao kweli wanaweza kujitakatifuza hasa wao kwanza kwa njia ya unyenyekevu,na uaminifu katika zoezi la huduma ya upatanisho.

 

29 March 2019, 13:03