Tafuta

Vatican News
Theodore Edgar McCarrick Theodore Edgar McCarrick  (AFP or licensors)

Vatican:McCarrick amevuliwa huduma ya upadre

Askofu wa zamani wa Marekani Theodore McCarrick amevulia huduma ya upadre baada ya Mkutano wa Baraza la Kipapa la mafundisho Tanzu ya Kanisa kuthibitisha kuwa na hatia ya kuwanyanyasa kingono watoto na watu wazima

Na Sr Angela Rwezaula – Vatican

Baraza la Mafundisho Tanzu ya Kanisa limetoa taarifa kuhusu McCarrick ambaye alijitangaza adharani  kuwa ni mwenye hatia dhidi ya kukiuka Amri ya Sita ya Mungu ya kuwanyanyasa kijinsia watoto na watu wazima. Baba Mtakatifu Francisko ameridhia asili ya uamuzi wa mwisho. Theodore Edgar McCarrick wa Marekani,  mwenye umri wa miaka 88 amevuliwa huduma zote za kipadre. Ni taarifa iliyotolewa rasmi na Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa katika maandiko haya kwamba, tarehe 11 Januari 2019, Baraza la Kipapa la Mafudisho Tanzu ya Kanisa kwa  uaminifu limetoa hati ya mwisho wa mchakato wa hatia juu ya Theodore Edgar McCarrick, aliyekuwa Askofu Mkuu Mstaafu wa Washington, D.C., na mabaye aliye kuwa amehukumiwa kwa madai kadhaa ya uhalifu wa unyanyasaji kijinsia aliouweka hadharani kuhusu Amri ya Sita ya Mungu. Na tangu wakati alikuwa amesimamishwa katika huduma yake na kuwa katika hali ya kilei.

Historia ya mchakato

Tarehe 13 Februari 2019, katika mkutano wa kawaida wa IV, Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa ilijadili kuhusu masuala hayo yaliyo wakilishwa katika mchakato huo na  kutoa uamuzi kwa hati ya Mkutano. Uamuzi huo umefikishwa kuwa Theodore McCarrick tarehe, 15 Februari 20 19. Na Baba Mtakatrifu Francisko ametambua asili ya mwisho wa mchakato huo na kanuni ya sheria ya maamuzi hayo ambayo  yanatambua na kumsimamisha kutoka katika shughuli zote upadre. Mwezi Septemba 2017 Jimbo Kuu la New York lilitoa taarifa katika Baraza la Mafundisho Tanzu ya Kanisa kuhusu madai ya mtu huyo, McCarrick kuhusiana na manyanyaso yaliyotokea miaka ya sabini akiwa kijana.

Na Baba Mtakatifu aliomba waendeshe mchakato wa upelelezi kwa kina, uliofanyika katika Jimbo Kuu la New York na katika hitimisho walitoa nyaraka zilizopelekwa katika Baraza la Kipapa la Mafundisho tanzu ya Kanisa. Juni 2018, Kardinali Pietro Parolin kwa mwongozo wa Baba Mtakatifu alitoa maelekezo ili McCarrick hasiendelee na huduma ya kikuhani hadharani. Wakati huohuo wa mchakato uchunguzi uliweza kubaini mambo mengine na ambapo tarehe 28 Julai 2018, Baba Mtakatifu Francisko aliliridhia Maombi yake ya kujiuzuru katika Baraza la Makardinali na kumzuia hasiendelee na  zoezi lolote lile la utoaji wa huduma wazi  wakati huo akamwomba  aweze kujikita katika maisha yake kwa sala na toba.

Mtazamo wa Mkutano wa Marais wa Mabaraza ya maaskofu duniani

Tarehe 6 Oktoba 2018, katika tangazo la vyombo vya habari walithibitha kuwa iwe manyanyaso au kuhusika kufikicha inawezekana kufikiriwa kama hatia na haikubaliki! Na Baba Mtakatifu Francisko alito mwaliko wa kunganisha nguvu zote ili kupambana na janga kubwa la manyanyaso iwe ndani na nje ya Kanisa na ili kuweza kuzuia uhalifu huo usiweze kuendele na kusababisha majanga makubwa kwa wasio na hatia na zaidi waaathirika wa kijamii. Na katika mtazamio wa Mkutano wa Marais wa Mabaraza yote ya maaskofu duniani kuanzia tarehe 21-24 Februari 2019 alisisitiza katika barua yake kwa “Watu wa Mungu”, kwamba: "ndiyo moja ya njia ya kuweza kujibu suala hili la ubaya ambalo limewakumba maisha ya wengi, ni kuishi kama zoezi ambalo linawahusisha watu wote kama watu wa Mungu. Katika utambuzi huo, wote tunapaswa kuhisi kama  sehemu ya watu na historia ya pamoja ambayo itatusaidia kutambua dhambi zetu na makosa ya wakati uliopita,ili kuweza kujipyaisha ndani" (tarehe20 Agosti 2018).

16 February 2019, 16:19