Tafuta

Vatican News
Papa Francisko asema, ni ndugu na hujaji wa amani kwenye Umoja wa Falme za Kiarabu! Papa Francisko asema, ni ndugu na hujaji wa amani kwenye Umoja wa Falme za Kiarabu!  (AFP or licensors)

Umoja wa Falme za Kiarabu: Papa! Niko kati yenu kama ndugu!

“Ninapenda kuchukua fursa hii kushuruku kwa mapokezi makubwa mliyonipatia. Nitaendelea kuwakumbuka katika sala zangu. Ninawaombea baraka na neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu wananchi wote wa Umoja wa Falme za Kiarabu amani na mshikamano wa kidugu! Francisko. 4.2.2019”.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu, tarehe 4 Februari 2019, baada ya kukutana na kusalimiana na Mfalme Mrithi  Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan alipewa kitabu cha wageni maarufu na kuandika humo ujumbe ufuatao: “Ninapenda kuchukua fursa hii kushuruku kwa  mapokezi makubwa mliyonipatia. Nitaendelea kuwakumbuka katika sala zangu. Ninawaombea baraka na neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu wananchi wote wa Umoja wa Falme za Kiarabu amani na mshikamano wa kidugu! Francis 4.2.2019”.

Viongozi hawa walipata pia nafasi ya kubadilishana zawadi kama kumbu kumbu ya hija hii ya kitume kwenye Umoja wa Falme za Kiarabu. Baba Mtakatifu katika ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii anasema, anafanya hija ya kitume kwenye Umoja wa Falme za Kiarabu kama ndugu, ili kuweza kuandika pamoja na viongozi wengine wa kidini ukurasa wa majadiliano ya kidini ili kudumisha amani! Baba Mtakatifu anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kumwombea ili mkutano huu uweze kuzaa matunda yanayokusudiwa, yaani: haki, amani, maridhiano na udugu kati ya watu wa Mataifa!

Kitabu cha Wageni
04 February 2019, 13:59