Tafuta

Baba Mtakatifu anathibtisha kuwa kila masikini anasutahili msaada bila kujali dini au kabila.Amezungumza hayo wakati alipokutana na chama cha Mtakatifu Petro Baba Mtakatifu anathibtisha kuwa kila masikini anasutahili msaada bila kujali dini au kabila.Amezungumza hayo wakati alipokutana na chama cha Mtakatifu Petro 

Papa anasema ni kusaidia masikini bila kujali dini au kabila!

Alhamisi 28 Februari 2019,Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wanachama cha Mtakatifu Petro mjini Vatican wakiwa wanaadhimisha miaka 150 tangu kuanzishwa kwake mjini Roma kunako mwaka 1969 kwa njia ya kikundi cha vijana kutaka kusaidia masikini wa Roma.Amehimiza umuhimu wa kutoa huduma bila kujali dini au kabila

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Alhamisi tarehe 28 Februari 2019, Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wanachama cha Mtakatifu Petro mjini Vatican na kuwakaribisha kwa sangwe kuu wakati huo akiwakumbuka hata familia zao na wote ambao wanashirikiana mipango mingi ya upendo. Amemshukuru Mwenyekiti wa Chama hicho Leopoldo Torlonia, kwa maneno ya hotuba yake. Baba Mtakatifu anasema mkutano huo unawadia katika fursa ya kipindi  maalum cha kumbukumbu ya miaka 150 tangu kuanzishwa kwa chama chao kunako mwaka 1869 na baadhi ya vijana wa Roma. Wao walikuwa wanakiongozwa na shauku ya ushuhuda wa kusaidia na kwa  uaminifu wa Papa Pio IX katika kipindi ambacho kilikuwa hakuna maelewano kati ya Kanisa na serikali.

Mambo muhimu matatu:sala,matendo ya upendo na sadaka

Pamoja nao, Baba Mtakatifu Fracisko anasema anamsifu Bwana kwa wema uliotimizwa kwa kipindi cha miaka 150 katika wazo kuu la shukrani kwa wadau wote wa chama wa jana na leo.  Katika kipindi hiho kirefu  cha uwepo wake  anathibtisha kwamba hapakukosekana kamwe mpango wake asili wa chama ambao unajifafanua kwa misingi mitatu ya sala, matendo ya dhati ya upendo na sadaka. Mambo hayo yamekuwa msingi wa ajabu katika kuchanua shughuli, kwa mantiki ya upendo w kuakaribisha walio wa mwisho. Mambo hayo ndiyo yana tabia ya uhai wa kitume wa wakati endelevu wa chama chao. Anawatia moyo  wa kuendela na kupyaisha kwa uhai wake. Kwa namna ya pekee kati ya mambo hayo msingi ni sala!

Iwapo katika ndugu ni kukutana na uwepo wa Yesu

Baba Mtakatifu anasema, iwapo katika ndugu tunakutana na Yesu, ina maana ya kwamba shughuli ya kujitolewa inageuka kuwa uzoefu wa Mungu na sala. Kwa maana hiyo anawashuri wasisahau nguvu na umuhimu wa sala kwa ajili yao na wale ambao wanashirikiana katika kazi ya upendo wa dhati. Maombi hayo yanahitaji kumwilishwa katika  kusali na kusikiliza Neno la Mungu. Siri mwafaka ya kila mapango anabainisha kuwa  ni uaminifu kwa Kristo na uhusiano binafsi na Yeye katika sala. Wao watakuwa tayari kukimbilia wale ambaleo  hii wanaishi katika hali mbaya au wametupwa pembezoni. Maisha ya kila siku kwa hakika yanahitaji uwepo wa Yesu  ambamo chini ya mtazamo huo wote wanapaswa  kumkabidhi hata mateso ya wagonjwa, wapweke, wazee, hofu ya masikini na wadhaifu waliobaguliwa.

Hata katika nyakati hizi huduma yao ni yenye thamani

Baba Mtakatifu anathibitisha kwamba hata katika siku zetu, huduma yao ya thamani iliyojikita katika Tume tofauti inataka kuwa kielelezo mwafaka na ushuhuda hai wa upendo  ambao ni wa Kanisa na kwa namna ya pekee Vatican inavyotoa nafasi ya kwanza kwa masikini na wanaoteseka . Kila masikini anayo hadhi ya kutambuliwa dini na bila kujali kabila na kila hali yoyote aliyo nayo.  Kwenda kukutana na masikini, kuwafariji wagonjwa na wanaoteseka, ndiyo kuhudumia Yesu anaye thibitisha kwamba: “Yote mliyo watendea mmoja wa ndugu hawa walio wadogo, mlinitendea mimi" (Mt 25,40).

Shukrani kubwa kwa sadaka yao ya Mtakatifu Petro

Anawashukuru kwa yote wanayofanya na kwa kupyaisha kwa kutoa sadaka ya  Chama cha Mtakatifu Petro ambayo kila mwaka wanfika kumkabidhi . Hiyo ni ishara ya nguvu kwa watu wenye matatatizo. Na wakati hu huo ni ushiriki wa hai wa kuhamasishwaji katika Makao makuu ya Kitume ili kuweza  kujibu ongezeko la dharura katika Kanisa kwa namna ya pekee katika nchi zilizo masikini. Baba Mtakatifu amependa kwa mara nyingine tena kuwapongeza kwa jitihada zao na uamonifu kwa Mfuasi wa Mtume Petro. Bikira Maria awasindikiza na kuwasaidia chini ya ulinzi wa umama wake katika mapendekezo na mipango yao ya wema. Amewapa Baraka ya kitume na iwafikie hata failimilia zao, bila kusahau wasali kwa ajili yake!

28 February 2019, 15:30